Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Vita vya Ukraine: Je, madai ya Putin kuhusu Ukraine yana ukweli au hayana msingi kiasi gani?
Rais wa Urusi Vladimir Putin ametambua uhuru wa maeneo mawili yanayodhibitiwa na waasi mashariki mwa Ukraine kama taifa huru.
Katika hotuba yake kwa televisheni kwa Ikulu ya Kremlin, Bw Putin alijaribu kuhalalisha matendo yake kwa msururu wa shutuma kuhusu Ukraine.
"Ulimwengu unaoitwa ustaarabu ... utisho huu wa karibu watu milioni nne unapendelea kupuuza mauaji ya halaiki."
Akimzungumzia Donbass mashariki mwa Ukraine, Rais Putin alidai kuwa watu wanaozungumza Kirusi huko walikuwa wakikabiliwa na "mauaji ya halaiki," neno ambalo alikuwa ametumia hapo awali na alirudia kwenye televisheni ya serikali ya Urusi.
Mkataba wa Umoja wa Mataifa wa Mauaji ya Kimbari, ulioidhinishwa na nchi 152, ikiwa ni pamoja na Urusi, unafafanua mauaji ya halaiki kama "kitendo kinacholenga uharibifu kamili au sehemu ya kikundi cha kitaifa, kikabila, rangi au kidini."
Mifano ni pamoja na mauaji ya Rwanda na Srebrenica.
Lakini hakuna ushahidi wa mauaji ya kimbari mashariki mwa Ukraine. Kansela wa Ujerumani Olaf Scholz amepuuzilia mbali kauli ya Bw Putin na kusema "upuuzi".
Umoja wa Mataifa unasema mataifa "wakati fulani huelezea matukio fulani au vitendo vya unyanyasaji kama mauaji ya halaiki," lakini kwamba "kauli hizi haziwezi kuchukuliwa kama mamlaka au uamuzi."
Lakini mzozo wa mashariki mwa Ukraine unaendelea.
Kulingana na makadirio ya Umoja wa Mataifa, kati ya Aprili 14, 2014 na Februari 21, 2022, watu 14200-14400 waliuawa mashariki mwa Ukraine, ikiwa ni pamoja na:
• Takribani raia 3,407
• Wanajeshi 4,400 wa Jeshi la Kiukreni
• Wanachama 6,500 wa vikundi vyenye silaha
Takriban watu 39,000 walijeruhiwa, wakiwemo raia kati ya 7,000 na 9,000.
Mnamo mwaka wa 2018, kituo cha uchambuzi cha International Crisis Group kiligundua kuwa takriban watu 600,000 katika pande zote mbili za mzozo walikuwa wakiishi katika "maeneo hatari ambapo ufyatuaji risasi wa kila siku, mabomu ya ardhini na uhuru wa kutembea na huduma za kimsingi zimewekewa vikwazo vikali."
"Tayari kumekuwa na taarifa kwamba Ukraine inataka kutengeneza silaha zake za nyuklia ... Ukraine kweli ina teknolojia ya nyuklia ya Usovieti na njia za kuwasilisha silaha kama hizo."
"Hatuna silaha kama hizo," Rais wa Ukraine Vladimir Zelensky alisema katika mkutano wa usalama wa viongozi wa dunia wiki iliyopita.
Ukraine, ambayo ilikuwa na silaha ya nyuklia ya tatu kwa ukubwa duniani wakati wa Vita Baridi, ilitoa silaha zake za nyuklia katika miaka ya 1990 kwa kubadilishana na dhamana ya usalama kutoka kwa Marekani, Uingereza na Urusi.
Kwa mujibu wa wataalamu wa masuala ya ulinzi, nchi hiyo kwa sasa haina vichwa vya nyuklia vinavyoweza kutolewa kwa ndege au makombora.
Balozi wa Ukraine nchini Ujerumani, Andrei Melnik, alisema mwaka jana kwamba Ukraine italazimika kufikiria upya hali yake ya kutokuwa na silaha za nyuklia ikiwa haitajiunga na NATO.
Suala hilo limeripotiwa kuwa mjadala mkubwa wa umma tangu mzozo wa mashariki mwa Ukraine na kunyakuliwa kwa Crimea na Urusi mnamo 2014.
Lakini serikali haijasema inakusudia kurejea kwenye silaha za nyuklia, na mkakati wa kijeshi uliorekebishwa uliochapishwa mwaka jana hautaji kukamata silaha hizo.
Shirika la Kimataifa la Nishati ya Atomiki (IAEA) limetuambia kwamba halioni dalili zozote nchini Ukraine za "kuelekeza nyenzo za nyuklia kwa malengo ya amani."
"Bila shaka, rushwa, ambayo imekuwa tatizo na mtihani kwa nchi nyingi, ikiwa ni pamoja na Urusi, imechukua mkondo wa pekee nchini Ukraine."
Urusi ndiyo nchi iliyo na nafasi ya chini kabisa ya Ulaya katika Fahirisi ya Mitazamo ya Ufisadi ya 2021 ya Transparency International, ya 136 kati ya nchi 180 duniani, na 122 nchini Ukraini.
Kulingana na shirika hilo, utendaji wa Ukraine umeimarika kwa kiasi kikubwa katika muongo mmoja uliopita.
Lakini Ilya Shumanov, msemaji wa Transparency International nchini Urusi, alisema: "Ukadiriaji wa Urusi ... unaonyesha ukosefu wa mabadiliko chanya ya kimfumo katika vita dhidi ya ufisadi."
"Wakati wa janga hili, zaidi ya madaktari 60,000 na wafanyakazi wengine wa afya waliondoka nchini."
Kesi hiyo inatokana na ripoti iliyotolewa Machi 2021 na Kituo cha Razumkov cha Utafiti wa Kijamii nchini Ukraine, ambacho kinasema kwamba "wataalamu wanakadiria kuwa madaktari na wahudumu wa afya 66,000 wameondoka Ukraine tangu mwanzoni mwa 2020."
Kulingana na Waziri wa zamani wa Afya wa Ukrainia Maxim Stepanov, kufikia Februari 2021, takriban 34,000 kati yao wamesajiliwa katika mfumo wa huduma ya afya ya Kiukreni na wamejiuzulu tangu janga hilo kuanza.
Kulingana na Taasisi ya Utafiti wa Kiuchumi, daktari huko Kyiv anapata $ 23,000 kwa mwaka, ikilinganishwa na $ 61,000 katika nchi jirani ya Poland.
Takwimu rasmi hazifuatilii madaktari wa Kiukreni huenda kufanya kazi, lakini waajiri wa huduma ya afya wanasema idadi ya waombaji kazi nchini Poland, Jamhuri ya Czech na Slovakia inaongezeka kwa kasi.
Unaweza pia kusoma
- YA MSINGI:Mzozo wa Ukraine: Kwanini Urusi inaivamia Ukraine na Putin anataka nini?
- UFAFANUZI:Mzozo wa Ukraine: Swift ni nini na kwa nini kuipiga marufuku Urusi ni muhimu sana?
- UCHAMBUZI:Mzozo wa Ukraine: Putin humsikiliza nani?
- KWENYE RAMANI:Uvamizi wa Ukraine: Shambulio la Urusi kwenye ramani
- ZELENSKY:Volodymyr Zelensky: Mfahamu rais wa Ukraine aliyeacha umaarufu wake wa TV na kuingia kwenye siasa
- PUTIN:Vladimir Putin: Rais wa Urusi aliyeagiza shambulio Ukraine
- SILAHA:Mzozo wa Ukraine:Makombora ya stinger na silaha nyingine kali zinazotumiwa Ukraine