Urusi na Ukraine: Moscow yaonyesha kwa mara ya kwanza "manusura" wa Moskva, meli ya kivita ya Bahari Nyeusi the iliyolipuka na kuzama

Iliyochapishwa

Limekuwa ni mojawapo ya maswali makubwa tangu kuzama kwa meli ya kikosi cha majini cha Urusi inayofahamika kama Moskva, ikiwa ndio meli kuu ya jeshi la majini la Urusi katika Bahari nyeusi, iliyolipuka na kuzama wiki hii : Nini kilichotokea kwa zaidi ya wanajeshi 500 waliokuwa wakisafiri ndani yake?

Wizara ya ulinzi ya Urusi ilithibitisha Jumatano wiki iliyopita kulipuka kwa "moto" ikatika boti na kuhakikisha kuwa ilikuwa imewaokoa wanajeshi wake.

Siku moja baadaye, aliripoti kwamba meli hiyo ilikuwa imezama kutokana na "hali mbaya ya hewa."

Hakuelezea zaidi juu ya sababu, lakini Ukraine ilihakikishiwa kabla ya Urusi kuthibitisha taarifa kwamba ilikuwa imepigwa na makombora mawili aina ya Neptune.

Tangu wakati ule , hatma ya wahudumu ya meli muhimu zaidi ya Urusi katika Bahari nyeusi iliibua kila aina za dhana.

Jumamosi, wizara ya ulinzi ya Urusi ilichapisha picha zinazoonyesha kile inachosema ni abiria wanajeshi wa kikosi cha majini wanaohudumu katikameli ya Moskva.

Haijulikani ni lini picha hizi zilichukuliwa au iwapo kweli walikuwa ni wafanyakazi wa meli hiyo, lakini ni mara ya kwanza kwamba Urusi imewaonyesha wanajeshi kama manusura wa kile kilichotokea katika meli.

Kuzama kwa Moskva kumeelezewa kama pigo kubwa kwa ari ya jeshi la Urusi, kutokana na umuhimu wake na kuwa nembo ya uwezo wa kijeshi wa kikosi cha wanamaji cha nchi hiyo.

Urusi ilionyesha nini?

Picha ilionyesha kikundi cha wanajeshi katika sherehe katika kile kilichoonekana kuwa ni makao makuu ya ngombe ya jeshi la majini katika mji wa mwambao wa Crimea wa Sevastopol, wakisalimiwa na Kamanda mkuu Nikol ái Yevmenov.

Video hiyo ilionyesha mkuu huyo wa majeshi Yevmenov na maafisa wengine wakiwa wamesimama mbele ya mabaharia 100. Hainajafanuliwa ni nini kilichotokea kwa waliosalia ambao walikuwa katika meli.

Katika hotuba iliyoonyeshwa katika mwisho wa video, Yevmenov anasema kwamba maafisa na mabaharia kwa sasa wanaishi katika ngome yao iliyopo Sevastopol na wataendelea kufanya kazi katika kikosi cha majini.

Urusi iliripoti kuwa hapakuwa na majeruhi wa vifo katika ajali ya moto na kuzama kwa meli hiyo.

Hatahivyo, afisa wa Marekani alinukuliwa na shirika la habari la Reuters, ambaye utambulisho wake haujatambuliwa, akisema idara ya ujasusi ya Marekani inaamini kuwaliwa na waathiriwa.

Ukraine inasisitiza kwamba nahodha wa meli hiyo, Anton Kuprin, alikufa ndani yake, lakini BBC haikuweza kuthibitisha dai hili.

Moskva

Moska, meli yenye uwezo wa kubeba tani 12,490- ndio meli kubwa zaidi ya kivita ya Urusi kuwahi kuzama ikiwa vitani tangu Vita vya II vya dunia.

Katika siku ya kwanza ya uvamizi wa Ukraine, Februari 24, meli hiyo ilipata umaarufu baada ya kufuatilia mawasiliano ya kikosi kidogo cha walinzi wa mpaka wa Ukraine uliopo kwenye kisiwa cha Nyoka -Snake Island kilichopo kwenye Bahari Nyeusi ambao waliamrishwa kuisalimisha.

Meli hiyo iliundwa katika mji wa kusini mwa Ukraine wa Mikolaiv, ambao umekuwa ukikumbwa na mashambulio makali ya makombora ya Urusi katika siku za hivi karibuni.

Meli hiyo ambayo ni mtambo unaoongoza makombora awali iliripotiwa kupelekwa na Moscow katika mzozo wa Syria ambako vikosi vya Urusi katika nchi hiyo ikiwa na ulinzi mkali wa vikozi vya majini kutoka Mediterranean.

Pia ni meli ya pili kwa ukubwa ambayo Urusi imeipoteza tangu kuanza kwa uvamizi wake wa Ukraine.

Unaweza pia kusoma