Ni kwanini unahitaji kuwa makini na ukubwa wa kiuno chako?

কোমরের আকার বেড়ে যাচ্ছে কি না সেদিকে নজর রাখুন।

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Chunga iwapo uzito wa kiuno chako unaongezeka au la
Iliyochapishwa

Watalamu wa afya wanashauri kuwa makini na kiuno chako ili kuendelea kuwa mwenye afya. Wanasema kwama kama kiasi cha mafuta hatari ya ziada kitaendelea kujilimbikiza katikati mwa mwili wako, yanaweza kusababisha hatari za kiafya.

Hiyo ndio maana watu watu wanatshauriwa kuchukua vipimo vya kiuno mara kwa mara.

Upana wa kiuno unatakiwa kuwa vipi

Madaktari wanasema ukubwa wa kiuno cha mtu mzima unapaswa kuwa chini zaidi kuliko nusu ya urefu wake wa mwili ili kupunguza hatari za kiafya.

Kwa mfano, kama una urefu wa sentimita 165 au futi 5 na inchi 9 , badi ukubwa wa kiuno chako unapaswa kuwa sentimita 8.5 au chini ya inchi 34.

Taasisi ya taifa ya afya na hurduma bora, au NICE, ni shirika la afya la Uingereza.

Syeda Sharmin Akhter, muasisi wa kituo kinachotoa ushauri nasaha kuhusu lishe, ambaye hutoa huduma za utaalamu wa lishe na huduma na afya mjini Dhaka, anasema ukubwa unaofaa wa kiuno kwa wanawake ni inchi 35 au sentimita 6 huku kwa wanaume wakitakiwa kuwa na ukubwa wa inchi 40 au sentimita 101.

"Iwapo utakuwa ni zaidi ya huo, ni hatari. Kama ni mpana kuliko kiuno, inaweza kusababisha kisukari aina ya 2, shinikizo la damu, saratani, ugonjwa wa moyo, na matatizo mengine ya kiafya.," alisema.

অস্বাস্থ্যকর খাবার

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Vyakula visivyo vya kiafya pia vinaweza kusababisha kuongezeka kwa uzito wa mwili

Ukokotoaji wa BMI

NICE inasema kwamba mbinu ya kipimo cha ukubwa wa mwili au BMI kwa ajili ya kupima unene kupita kiasi pia ni cha maana, lakini hakiwezi kugundua kuongezeka kwa uzito katika eneo la chini la tumbo.

Matokeo yake, wale ambao wako katika kitengo cha afya cha BMI wanaweza kuwa na mafuta ya mwili ya ziada kwenye kiuno chao.

BMI hupimwa kwa kukokotoa urefu wa mwili na uzito.

Mtaalamu wa lishe Syeda Sharmin Akhter amekuja na njia nyingine ya kukokotoa ambayo inaweza kutumiwa kupima iwapo uzito wa kiuno wa mtu umepungua au uko juu ya mstari hatari.

Njia hii huhesabiwa kwa uwiano wa kiuno hati kwenye nyonga. Kwa maana hii, ukubwa wa kiuno hugawanywa na ukubwa wa nyonga.

Iwapo kipimo hiki ni 0.7 hadi 0.8 basi itachukuliwa kama kitu cha kawaida. Lakini kama kikizidi kipimo hiki, hatari itaongezeka.

Bi Akhtar alisema ukubwa wa kiuno unaweza kuongezeka kwa wakati mmoja kwa wasichana na kwa wakati mwingine kwa wavulana. Inahusisha tabia za kula, mazoezi, na kadhalika.

"Jinsi tunavyokaa na kufany akazi pia kunaweza kusababisha mkusanyiko wa mafuta katika sehemu ya chini ya tumbo letu ," alisema.

"Tunafanya na uzito katika sehemu ya chini ya tumbo letu. Halafu katika kipindi cha miezi mitatu au minne kiuno kinaweza kuwa kipanana."

Ndio maana alisisitiza juu ya kuamka mapema na kutembea katikati ya saa za kazi badala ya kukaa kwa muda mrefu.

Alisema kwamba kuna aina mbili za mafuta katika sehemu ya kiuno. Aina ya mafuta ambayo hukaa ndani na kutoka ndani husababisha shinikizo upande wa nje , ili unene wa mafuta uweze kuonekana nje.

Kukabiliana na aina hii, aina ya mafuta hukusanyika katika sehemu ya chini ya tumbo.

ডাক্তাররা কোমরের ওপর নজর রাখার পরামর্শ দিচ্ছেন।

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Madaktari wanashauri kufuatilia ukubwa wa kiuno chako

Alisema kwamba ulaji zaidi wa mafuta ya kutengenezwa viwandani, hata kama unapata usingizi wa kutosha, mafuta ya mwili yanaweza kukusanyika katika eneo la kiuno.

Pale inapokuwa vigumu

"Pia unapokuwa na umri wa zaidi ya miaka 40, uwe mwanaume au mwanamke, mafuta ya mwili hukusanyika polepole katika sehemu ya chini ya tumbo.

Matokeo yake umbo la mwili hubadilika. Eneo la juu la mwili huwa jembamba na sehemu ya pili huwa pana."

"Halafu unapata matatizo ya kongosho, maumivu ya viungo( arthritis), na uti wa mgongo," alisema.

Wataalamu waasema hii inaongeza hatari ya kupata ugonjwa wa kisukari cha aian ya 2, shinikizo la juu la damu, magonjwa ya moyo na kiharusi.

Mwongozo mpya wa NICE unasema kwamba baadhi ya watu wa jamii ya Asia na Afrika wanakabiliwa na uwezekano mkubwa wa kuwa na ongezeko la mafuta ya mwili kwenye eneo la kiuno.

Syeda Sharmin Akhter alisema, tatizo hili pia linaongezeka katika maeneo mbali mbali ya dunia. Watu wengi wamekuwa wakifika hospitali wakiwa na matatizo haya ya kiafya.

"Kuna watu wengi ambao wanaweza kuwa na seli nyingi za mafuta katika miili yao, ambao huja kwetu kwa ajili ya kupata ushauri wa jinsi ya kupunguza uzito wa mwili.

"Mwanamke anaweza kutokuw ana uzito wa mwili wa kupindukia, lakini sehemu ya chini ya tumbo lake inaweza kusababisha ukosefu wa uwiano wa homoni, maumivu ya mgongo, maumivu ya magoti, na matatizo ya ujauzito.

Matatizo ya wanaume ambao hawana uwezo wa kuzalisha pia yanaongezeka kutokana na kupanuka kwa viuno vyao ," alisema.

Hatahivyo, watalamu wanasema njia hii ya kupima kiuno haifanyi kazi kwa kila mtu. Kwa wale ambao wana kimo kifupi cha mwili au wenye umri mdogo sana au wenye zaidi ya umri wa miaka 60, kipimo hiki huenda kisiwe namba sahihi ambao uzito wao umepungua kutokana na umri.