Uvamizi wa Ukraine: Warusi wahisi makali ya vikwazo

Iliyochapishwa

"Ningekuwa na uwezo ningehama Urusi sasa hivi, Ningefanya hivyo. Lakini siwezi kuacha kazi yangu," anasema Andrey.

Hataweza kumudu mpango wa kununua nyumba kwa mkopo wa malipo ya pole pole huko Moscow baaada ya viwango vya riba kuongezwa.

Mamilioni ya Warusi kama yeye wameanza kuhisi athari za vikwazo vya kiuchumi vya nchi za Magharibi vilivyowekwa kuadhibu nchi hiyo kwa kuvamia taifa jirani la Ukraine.

"Napanga kutafuta wateja wapya nje ya nchi haraka iwezekanavyo na kuhama Urusi kwa pesa nilizokuwa nikihifadhi kwa awamu ya kwanza," anasema mbunifu huyo wa viwanda mwenye umri wa miaka 31.

"Naogopa kuwa hapa - watu wamekamatwa kwa kuongea dhidi ya 'msimamo wa chama'. Naona aibu na hata sikuwapigia kura walio madarakani."

Sawa na watu wengine waliohojiwa katika makala hii hatutatumia majina yao kamili au kuonesha sura kutokana na sababu za kiusalama. Baadhi ya majina yamemadilishawa.

Vikwazo vya sasa vinavyoikumba Urusi vinaelezewa kuwa vita vya kiuchumi - vinalenga kuitenga nchi hiyo na kusababisha mdororo mkubwa wa uchumi. Viongozi wa Magharibi wanatumai hatua ambazo hazijawahi kushuhudiwa zitaleta mabadiliko katika fikra huko Kremlin.

Warusi wa kawaida wanakabiliwa na kuona akiba yao ikifutwa. Maisha yao tayari yanavurugika.

Vikwazo dhidi ya baadhi ya benki za Urusi ni pamoja na kuzikata kwenye Visa na Mastercard, na hivyo basi Apple Pay na Google Pay.

Daria, 35, meneja wa mradi huko Moscow, alisema hii inamaanisha kuwa hangeweza kutumia metro.

"Huwa nalipa kupitia simu yangu lakini haikufanya kazi. Kuna baadhi ya watu waliokabiliwa na tatizo hilo.

Ilibainika kuwa vizuizi hivyo vinaendeshwa na benki ya VTB ambayo iko chini ya vikwazo na haiwezi kukubali Google Pay na Apple Pay.

"Ilinibidi kununua kadi ya metro badala kama njia mbadala," aliambia BBC. "Pia sikuweza kulipa katika duka leo - kwa sababu hiyo hiyo."

Siku ya Jumatatu Urusi iliongeza maradufu kiwango chake cha riba hadi 20% katika juhudi za kukabiliana na vikwazo baada ya thamani ya sarafu yake kushuka kwa viwango vya juu. Soko la hisa bado limefungwa huku kukiwa na hofu ya kuuzwa kwa hisa nyingi.

Kremlin inasema ina rasilimali za kutosha kukabiliana na vikwazo, lakini hilo linatiliwa shaka.

Mwishoni mwa juma benki kuu watu kuwa watulivu kutokana na hofu iliyowafanya watu kukimbilia benki, kutoa pesa.

"Hakuna sarafu ya dola, wala roubles - hakuna kitu! Hata kama hakuna roubles sio hoja kwasababu sina haja nazo," alisema Anton (jina limemadilishwa), ambaye yuko na umri ya miaka na ambaye alikuwa anapiga foleni katika mashine za ATM mjini Moscow.

"Sijui kitakachotokea baadaye. Nahofia huenda tukakabiliwa na hali ya Korea Kaskazini na Iran."

Kununua sarafu za kigeni kunaigharimu Urusi karibu asilimia 50 zaidi ya ilivyokuwa wiki moja iliyopita - ikiwa zitapatikana.

Mwanzoni mwa mwaka 2022 dola moja iliuzwa kwa karibu roubles 75 na euro kwa 80. Lakini vita hivi vipya vimeweka rekodi mpya - wakati mmoja siku ya juma tatu dola moja iligarimu roubles 113 na euro moja kwa roubles127.

Kwa Warusi, kiwango cha dola dhidi ya ruble imekuwa suala nyeti kwa muda mrefu.

Katika miaka ya 1990 kufuatia kuanguka kwa Umoja wa Kisovyeti, dola ilikuwa sarafu pekee imara ambayo Warusi walitumia kuweka akiba yao - dau salama zaidi lilikuwa chini ya godoro.

Wakati serikali ya Rais Boris Yeltsin iliposhindwa kulipa deni lake mnamo 1998, wale ambao walikuwa wakilala na pesa za chini ya godoro walihisi kuwa salama.

Hata hivyo, katika muongo uliofuata hatua mbalimbali za benki kuu zilisaidia kuwahakikishia Warusi kuhusu ruble. Amana zilizowekwa katika sarafu ya Kirusi zilianza kukua na ndivyo pia kiasi cha fedha ambacho Warusi waliwekeza katika hisa za makampuni ya Kirusi.

Hata hivyo, wakati wowote kunapotokea hali ya kutokuwa na uhakika Warusi kila wakati hukimbilia mashine ya ATM iliyo karibu ili kutoa dola.

Wakati huu hali haikuwa tofauti.

Mara tu vita vilipoanzishwa nchini Ukraini wiki iliyopita, Warusi walimiminika kwenye vituo vya fedha, kutokana na funzo walilopata katika katika mizozo ya awali.

Ilya (jina limebadilishwa), ambaye yuko katika miaka yake 30, amemaliza tu kulipa deni la kununua nyumba kwa mkopo huko Moscow. Anasema hawezi kuhama "wakati wowote hivi karibuni".

"Wakati operesheni ya Donbas ilipoanza nilienda kwa ATM na kutoa akiba niliyokuwa nayo Sberbank kwa dola. Sasa ninaiweka chini ya mto wangu.

"Akiba yangu iliyobaki bado iko kwenye benki: nusu kwa dola na iliyobaki kwa sarafu ya rubles. Mambo yakizidi kuwa mabaya, nitazitoa zote. Naogopa kwa sababu natarajia kutokea kwawimbi la wizi. Lakini hali ndivyo ilivyo. ."

Picha kwenye mitandao ya kijamii zimeonyesha milolongo mirefu kwenye mashine za ATM na maeneo yaubadilishanaji wa fedha kote nchini katika siku za hivi karibuni, huku watu wakiwa na wasiwasi kwamba kadi zao za benki zinaweza kuacha kufanya kazi au kwamba kikomo kitawekwa kwa kiasi cha pesa wanachoweza kutoa.

Dola na euro zilianza kuisha ndani ya saa chache baada ya uvamizi huo. Tangu wakati huo, kiasi kidogo sana cha sarafu hizo zimepatikana na kuna kiwango cha juu cha rubles ngapi unaweza kutondoa.

Akiwa amesimama katika moja wapo wa foleni mjini Moscow, Evgeny (jina limebadilishwa), 45,alisema anataka kutoa pesa zake zote alipe mkopo wa nyumba alioyonunua.

"Kila mmoja ninayemjua anawasiwasi. Kila mtu ana msongo wa mawazo. Sina shaka hali itakuwa mbaya zaidi. Vita ni mbaya War .

"Nadhani 'nchi kubwa' zinapima nguvu za kila mmoja, kuamua ni ipi iliyo na uwezo. Na kila mtu anateseka."

Marat, 35, alisema: "Leo ni siku ya kwanza niliamua kutoa pesa, na sikupata shida yoyote. Nilitoa rubles zilizokuwa tu.

"Mimi sio mzuri wa kutabiri yatakyofanyika isku zijazo lakini nashuku maisha yetu yakuwa magumu sana. Wacha tusubiri."

Tatizo la pesa taslimu haliko Moscow pekee: watu wamekuwa wakikimbia kuzunguka Perm, Kostroma, Belgorod na miji mingine ya mkoa ili kupata dola au euro, BBC Idhaa ya Kirusi inaripoti.

Urusi yaishambulia Ukraine:Mengi zaidi