Macron alikataa kufanyiwa vipimo vya corona vya Urusi

Iliyochapishwa

Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron alikataa kufanyiwa vipimo vya Covid nchini Urusi kabla ya mkutano wake na Rais Vladimir Putin wa Urusi, Kremlin imethibitisha.

Uchunguzi huo ulihitaji itifaki ya afya ambayo haikubaliki na haiendani na ratiba ya kiongozi huyo wa Ufaransa, chanzo cha Ufaransa kiliambia BBC.

Hatua hiyo nafuatia ripoti kwamba Bw Macron alikataa kipimo cha PCR kwa hofu kwamba Warusi wangepata DNA yake.

Viongozi hao baadaye walifanya mkutano huku wakiwa wamekaa mbali kijamii siku ya Jumatatu.

Hawakusaliamia kwa mikono na kukaa na meza yenye urefu wa mita nne kati yao, huku waangalizi wakishangaa iwapo Bw Putin alikuwa akiitumia njia hiyo kutuma ujumbe wa kidiplomasia.

Lakini vyanzo vya kidiplomasia vya Ufaransa viliiambia Reuters kwamba Bw Macron alikuwa ameambiwa achague kati ya kukubali vipimo vya PCR vya Urusi ili kuwa karibu na Putin au kutii sheria kali za kukaa mbalimbali.

Tulijua vizuri kwamba hatua hiyo ilimaanisha kwamba hakutakuwa na kusalimiana kwa mkono katika meza hiyo ndefu. Lakini hatukubali waweze kupata DNA ya rais, mmoja ya vyanzo hivyo aliambia Reuters.

Chanzo hicho hakikuelezea jinsi huduma hiyo ya ujasusi wa Urusi ingetumia DNA ya bwana Macron.

Chanzo hicho katika Jumba la Elysee aliambia BBC: Masharti yaliowekewa mkutano huo kufanyika bila ya kuwepo kwa masharti ya corona itifaki ya kiafya ambayo isingekubalika na ratiba ya rais.

Kremlin ilihiboitisha kwamba bwana Macron alikaa mbali na kionhozi huyo wa Urusi kwasababu alikataa kufanyiwa vipimo Urusi.

Msemaji wa Kremlin Dmitry Peskov alisema kwamba Urusi inaelewa uamuzi huo huo wa Ufaransa na haikuathiri mazungumzo.

Bwana Macron alifanya vipimo vya PCR kabla ya ya kuondoka Ufaransa na daktari wake alifanya vipimo walipofika Mosvow , chanzo chengine cha kidiplomasia kiliambia Reuters.

Warusi walituambia kwamba Putin alihitajika kufauta sheria kali za kiafya , chanzo cha pili kilisema.

DNA - 'kitu cha thamani zaidi unachomiliki'

Kwa miongo kadhaa, majasusi wamewaorodhesha viongozi wa kigeni - wakijaribu kuelewa utu wao, jinsi wanavyoweza kuitikia hali fulani na muda gani wanaweza kudumu madarakani. Sehemu ya hayo ni kuelewa afya zao.

Lakini maendeleo katika sayansi yanamaanisha kuwa sampuli moja ya DNA sasa inaweza kufungua kubaini siku za nyuma, za sasa na hata za siku zijazo za mtu - je, ni kiongozi huyo wa kigeni anaficha ugonjwa au hali fulani au anaweza kukabiliwaje siku zijazo?

Bw Macron sio kiongozi pekee aliyepewa diplomasia ya "meza ndefu" ya Kremlin - mapema mwaka huu, Waziri Mkuu wa Hungary Viktor Orban na Rais wa Irani Ebrahim Raisi pia walionekana wameketi mbali na Bw Putin wakati wa ziara yao huko Moscow. .

Ikulu ya Kremlin imechukua hatua za tahadhari zaidi kumlinda Bw Putin, ambaye baadaye mwaka huu anafikisha miaka 70 na ambaye amepewa chanjo ya Urusi ya Sputnik V, asiambukizwe.

Hata hivyo, siku tatu tu baada ya kukutana na Bw Macron, Bw Putin alimkaribisha Rais wa Kazakhstan Kassym-Jomart Tokayev. Wawili hao walipeana mikono na kukaa kando ya meza ndogo ya kahawa kati yao.

Wakati wa mkutano wao Bw Macron na Bw Putin walizungumza kwa saa tano kuhusu mvutano kuhusu Ukraine.

Nchi za Magharibi zinasema Urusi inaweza kuivamia Ukraine lakini Urusi inakanusha kupanga kufanya hivyo licha ya kuwa imekusanya wanajeshi zaidi ya 100,000 kwenye mpaka wa Ukraine.

Wizara ya mambo ya nje ya Marekani imewataka Wamarekani nchini Ukraine kuondoka mara moja.