François Beya: Tunayofahamu kuhusu kukamatwa kwa mshauri maalumu wa Rais Tshisekedi anayeshutumiw akuyumbisha usalama

Chanzo cha picha, Présidence RDC
Anachukuliwa kama mmoja wa watu mwenye ushawishi zaidi katika DRC. Kukamatwa kwake kuliwashitua wengi nchini humo. Haya ndio tunayoyafahamu kumuhusu.
Kuhusu kukamatwa kwa Francois Beya, wachunguzi wana "wana viashiria vyenye ushuhuda mkubwa wa vitendo dhidi ya usalama usalama wa taifa ", alitangaza msemaji war ais wa DRC Jumanne.
Katika taarifa iliyosomwa kwenye televisheni ya taifa Jumanne jioni, Kasongo Mwema alisema uchunguzi unaendelea lakini hakutoa maenelezo zaidi kuhusu hasa mashitaka yanayomkabili mshauri huyo maalumu wa Rais Felix Tshisekedi
Mkala hii imebeba madhui yaliyotoka kwenye mitandao ya kijamii. Tunaomba ruhusa yako kabla kitu chochote hakija pakiwa, sababu wanaweza wakawa wanatumia Cookies na tekinolojia nyingine. Unaweza ukasoma sera sera ya kutumia cookies katika mitandao ya kijamii kabla ya kukubali. Kutazama maudhui haya chagua accept and continue
Mwisho wa X ujumbe, 1
Haya ni mawasiliano ya kwanza rasmi tangu kukamatwa kwake siku ya Jumamosi
Je rançois Beya alijibu?
Bw Beya hakutoa taarifa kwa umma kujibu kukamatwa kwake .Georges Kapiamba, ambaye ni rais wa chama cha mawakili cha DRC Congolese Association for Access to Justice, aliiambia BBC kwamba Francois Beya bado hajamteua wakili.
Beya anaaminiwa kuwa anashikiliwa na Shirika la taifa la ujasusi la DRC (ANR), ambacho ni kitengo cha huduma kilicho chini ya mamlaka yar ais wa januhuri ambacho kazi yake ni kuhakikisha usalama wa ndani na nje ya nchi wa taifa unalindwa.
Katika ukurasa wa Twitter , Georges Kapiamba alisema alimtembelea Beya pale mwishoni mwa juma,
Mkala hii imebeba madhui yaliyotoka kwenye mitandao ya kijamii. Tunaomba ruhusa yako kabla kitu chochote hakija pakiwa, sababu wanaweza wakawa wanatumia Cookies na tekinolojia nyingine. Unaweza ukasoma sera sera ya kutumia cookies katika mitandao ya kijamii kabla ya kukubali. Kutazama maudhui haya chagua accept and continue
Mwisho wa X ujumbe, 2
Francois Beya ni nani?
François Beya ni wakala wa zamani wa shirika la ujasusi la taifa la DRC ambako alihudumu kwa miaka kadhaa.
Mkurugenzi mkuu wa zamani wa uhamiaji (DGM) chini ya utawala wa zamani wa Rais Joseph Kabila kati ya mwaka 2001 na 2019, aliteuliwa kama Mshauri maaalumu wa masuala ya usalama na R ais Félix Tshisekedi katika mwaka 2019.
Rafiki huyu wa karibu wa rais wa zamani aliendelea kushikilia wadhifa wake kama mshauri wa rais wa masuala ya usalama wa rais wa Jamuhuri, licha ya kumalizika kwa muungao baina ya Rais Félix Tshisekedi na mtangulizi wake, Joseph Kabila mwkaa 2020.
François Beya amefahamika katika karibu tawala zote za kisiasa za Congo, kuanzia Rais Mobutu, Marais Kabila baba na Kabila mwana pamoja na ule wa rais wa sasa Felix Tshisekedi.
Kulingana na Mchambuzi na mtaalamu wa masuala Jean-Jacques Wondo, "Tangu Tshisekedi aingie madarakani, François Beya alikuwa muhimu na alikuwa mtu aliyetegemewa sana katika siasa za Tshisekedi na katika kuchukua maamuzi ya kiusalama, na alionekana ndiye mtu muhimu zaidi kwa rais, ndani na nje ya nchi.
Ni kama hakuna chochote ambacho kingefanyika bila kupitia kwake''
Ni kwanini kukamatwa kwake ni muhimu?
Kukamatwa kwake kulikuja kama jambo la kushangaza kwa watu wengi.
Kukamatwa kwake kulitokea wakati rais Tshisekedi alipokuwa akihudhuria kikao cha Muungano wa Afrika katika mji mkuu wa Ethiopia, Addis Ababa.
Ukimya wa serikali na ofisi ya- rais tangu Jumamosi umechochea uvumi kuhusu kuyumba kwa taifa.
Uvumi huo uliibua maandamano siku ya Jumapili, huku wafuasi wa rais wakiandamana mitaani ya Limete, katika mji mkuu Kinshasa.
Jumanne, msemaji wa rais alisema kuwa hali imedhibitiwa, na akaonya dhidi ya uvumi unaosambaa.













