Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Fats Timbo: 'Nilidhani nimelaaniwa'
Dada huyu mwenye umri wa miaka 25 ni mwigizaji, mwanamitindo na ana zaidi ya mashabiki milioni mbili kwenye TikTok.
Pia ana urefu wa mita 1.21, na ilimbidi kushinda uonevu na hofu ili kufikia mafanikio yake.
"Kwa muda mrefu nilifikiri nimelaaniwa," aliiambia BBC Radio 1Xtra.
"Nilipokuwa mdogo, kila nilipotoka nje na mtu kunitazama, nilijisikia vibaya sana."
Hata alipokuwa akinunua vitu, alikumbana na watu waliomtazama, waliomcheka na wa waliomdhihaki".
Lakini Fats amepata ujasiri kupitia mitandao ya kijamii, ambapo anashiriki michezo ya vichekesho na machapisho ya mitindo wa maisha.
"Nilipokuwa mtandaoni, na watu kuona ujasiri wangu walipenda kazi yangu, hiyo ndiyo iliyonifanya kuwa tofauti," anasema.
"Niligundua kuwa nilipokuwa nikipitia magumu yote na watu walikuwa wakinionea, nilihisi kuwa nilipitia yote kwa sababu.
"Napenda kuitwa mtu"
Fats alizaliwa mbilikimo, lakini anapendelea neno "watu wadogo."
"Umbilikimo ni neno la kimatibabu kwa ajili ya hali hiyo," anaeleza, "lakini sipendi kuitwa dwarf kwa sababu napenda kuitwa binadamu ".
Neno "umbilikimo karibu linanifanya nionekane kama kiumbe fulani," anaongeza.
"Neno hili kwangu, mara zote limekuwa likitumika kwa njia isiyo nzuri, ndiyo maana sipendi kulisikia au watu wakilitumia kwangu."
Alipokuwa mdogo, Fats "alibembelezwa" na watu waliomkaribia na kugusa mwili wake.
"Sikuelewa na sikuwa na mchumba au uzoefu wa uhusiano. Kwa hivyo nilidhani ninapaswa kubembelezwa, lakini sasa ninapoangalia nyuma, nikiwa mtu mzima na kuwaona watu wakinifanyia hivi nikiwa mtu mzima, najisikia vibaya tu, najihisi kama kitu.
"Siwezi kushindwa"
Lakini Fats anaamini kuwa "amebadilisha maoni ya watu kuhusu 'watu wadogo,' kwa kuelimisha watu."
Nyota huyo wa mitandao ya kijamii - ambaye alijizolea mashabiki baada ya kuonekana kwenye kipindi cha The Undateables cha Channel 4 mwaka 2018 - sasa ana zaidi ya mashabiki 240,000 kwenye Instagram.
"Ninashukuru kuwa na jukwaa langu," anasema, "Ilinifundisha kwamba naweza kufanya chochote. Siwezi kushindwa."
Fats hufanya kazi na kampuni za urembo na mtindo wa maisha kuunda maudhui yake - jambo ambalo lilionekana kutowekezekana wakati akikua.
"Mambo yanapobadilika na kampuni zinajaribu kubadilisha jinsi wanavyowakilisha watu, ninafurahi sababu kampuni zinanitumia," anasema.
"Ninawapa matumaini vijana ambao kama mimi, wana ngozi nyeusi na wanaweza kuwa na ulemavu."
"Hakukuwa na uwakilishi kwangu, nilihisi mpweke nilipokuwa mdogo," anaongeza Fats.
"Lakini sasa nawakilisha, mtoto!".