Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Chris Brown atuhumiwa kumlewesha na kumbaka mwanamke katika boti la kifahari
Chris Brown ameshtakiwa kwa kumlewesha na kumbaka mwanamke mmoja na sasa anadaiwa dola milioni 20.
Kisa hicho kinadaiwa kutokea kwenye mashua ya kifahari mnamo Desemba 30 mwaka 2020 huko Miami, Florida.
Radio 1 Newsbeat imewasiliana na mameneja wa Chris Brown kutoa maoni yao lakini bado hawajajibu.
Chris Brown ameonekana kujibu kwenye akaunti yake ya Instagram, akidai kuwa anashitakiwa kwa sababu anatoa muziki mpya.
Kesi hiyo imewasilishwa na mcheza densi na mwanamuziki ambaye hakutambulika, ambaye ametajwa tu kama 'Jane Doe' katika nyaraka za mahakama.
Hati hizo zinaangazia madai matano tofauti dhidi ya mwimbaji huyo yakiemo unyanyasaji wa kijinsia, na ukiukaji wa Sheria ya Unyanyasaji wa Kijinsia.
Mwanamke huyo anadai "anahofia maisha na kazi yake".
Anasema alialikwa kwenye meli na rapa na produsa Diddy, ambapo kisa hicho kinadaiwa kilifa
Kulingana na nyaraka moja, mwanamke huyo anadai kuwa alipewa vinywaji na Brown baada ya kuwasili, na baadaye akahisi "badiliko la ghafla, lisiloelezekala ufahamu".
Nyaraka hiyo inadai kuwa "alichanganyikiwa na akaanza kuhusi usingizini", kabla ya kupelekwa hadi chumbani ambako Brown anadaiwa kumvua nguo na kumbaka.
Inasemekana Brown aliwasiliana na mwanamke huyo siku iliyofuata, na kumwambia akunywe vidonge vya kuzuia ujauzito.
Kitengo cha Newsbeat pia kimejaribu kuwasiliana na wawakilishi wa Diddy, lakini bado haijapokea jibu.