Mfahamu Negaawo Jimmaa, kijana aliyeaibishwa na kimo cha urefu wake wa mwili

Negaawo wuxuu sheegay markasta oo ay da'diisu kororto inuu dhererkiisana uu kordho

Chanzo cha picha, FIB TV

Maelezo ya picha, Negaawo (Katikati)anasema urefu wake unaendelea kuongezeka kadri anavyokuwa w
Iliyochapishwa

Negawo Jimma, ni kijana ambaye ambaye anaishi katika mji wa Maqii uliopo katika jimbo la Oromia nchini Ethiopia, anasema kimo cha urefu wake kimeyatatiza maisha yake.

Negawo, mwenye umri wa miaka 24, anasema miongoni mwa changamoto ambazo anakabiliana nazo ni pamoja na kukosa nguo za kuvaa na viatu na kupata ugumu wa kutumia usafiri wa umma.

Nagaawo huvaa kiatu chenye ukubwa wa 54. Umbo na urefu wa mwili wake huwa humpatia changamoto anapokwenda kushonewa nguo na fundi au kutumia usafiri wa umma ambapo nauli yake huwa mara dufu ya wasafiri wengine.

"Hata kama mimi ni mtu mzima wa kutosha kuweza kujitegemea, hakuna mtu yeyite ambaye atakuwa tayari kuniajiri kwasababu ya urefu wangu ," anasema.

Nagaawo, ambaye alianza masomo yake ya elimu ya shule ya msingi mwaka 2006, alisema: "masomo yake hayakudumu kwa muda mrefu."

"Huu urefu wangu wa kupindukia ulianza kujitokeza mwaka 2013, na umeongezeka sana katika kipindi cha miaka mitatu iliyopita'' alisema.

Kijana huyo mwenye umri wa miaka 24, kwa sasa ana urefu wa mita 2.25, lakini kadri anavyoendelea kukua anazidi kuwa mrefu zaidi.

"Nilibaini urefu wangu ni tofauti na urefu wa marafiki zangu, nilipoanza kujipima mwenyewe urefu ,"alisema.

Negaawo Jimmaa

Chanzo cha picha, FIB TV

Maelezo ya picha, Negaawo Jimmaa

Mitizamo ya watu kumuhusu

Urefu wa kupindukia wa Nagaawo ulipoonekana kuwa tofauti na urefu wa marafiki zake na vijana wengine wa umri wake, alianza kujulikana sana na kuwa maarufu katika eneo alikoishi.

"Ninapoona watu wananishangaa, huaibika sana, na mtizamo wa watu kuhusu urefu wangu umenilazimisha kukaa ndani ya nyumba na kuwaepuka marafiki zangu," alisema.

Alikatiza masomo yake akiwa darasa la 8 baada ya kuugua kichwa kwa miaka kadhaa.

"Uvimbe wa urithi ulinifanya nisiweze kutembea tena, nilikuwa mgonjwa kwa miaka miwili na hatimaye mwaka 2018, nikaenda kwa daktarin kupata matibabu ."

Bada ya matibabu, anasema kujiamini kwake kumeongezeka na sasa hana hofu na urefu wake na wala haumuaibishi kama awali.

"Sasa ninakutana na watu, ninacheza na marafiki zangu, na sasa hali yangu imekuwa ya utulivu," alisema.

Negaawo Jimma

Chanzo cha picha, Nagawo Facebook Page

"Mavazi ninayovaa hutengenezwa hapa nchini na ninaweza kuweka akiba ya pesa nyingi kwa ajili ya kununua nguo zangu, lakini kwasababu ninavaa viatu vyenye ukubwa wa 54, siwezi kuvipata hapa nchini ," alisema Nagaawo.

Anasema kuna watu binafsi ambao humsaidia kumpatia nguo na viatu.

Negawoo ndio mwanaume mrefu nchini Ethiopia?

"Nimewaona watu warefu. Lakini sijawahi kumuna mtu mrefu kuliko mimi. Nimekwisha sikia kuwa mwanaume mrefu zaidi nchini Ethiopia anaitwa Asrat , akiwa na urefu wa mita 2.22 , lakini mimi nina urefu wa mita 2.25 . Inaonekana kwamba urefu wangu unaendelea kuongezeka," alisema.

Je ana mipango gani kwa siku zijazo?

Nagaawo anasema mpango wake ni kuendelea na masomo yake katika darasa la 8, na sasa amerejea tena shuleni.

"Huku nikisoma, ninajaribu kufanya kazi katika sekta ya utalii na utamaduni. Kwani watu hunishauri kutumia kimo cha urefu wangu kufanya matangazo ya biashara. Ingawa hakuna mtu yeyote aliyewahi kuwasiliana nami bado, ninamatumaini iwapo nitapata fursa nitafanya hivyo. "

Nagaawo anasema katika familia yao wamezaliwa watoto 9 , 5 wa kike na wa 4 wa kiume, lakini ndugu zake wote wana kimo cha kawaida cha urefu.

Unaweza pia kusoma:

''Katika familia yetu kwa ujumla hakuna aliye mrefu kama mimi, kwahiyo ni nini kinachonifanya kuwa wa kipekee?.'', ni swali ambalo anajiuliza kila siku , lakini bado hajapata jibu.