Jinsi Msichana wa miaka 19 alivyoweka historia ya tiba kumuokoa mama yake

Iliyochapishwa

Wakati alipokuwa na umri wa miaka 19 tu, Aliana Deveza alipanga na kupitia upasuaji wa kihistoria kwa ajili ya kuyaokoa maisha ya mama yake.

Aliishawishi hospitali kufanya ubadilishanaji wa kwanza wa kiungo nchini Marekani ambapo viungo vya mwili vilibadilishwa kwa watoaji ambao hawakuwa na uhusiano wowote wa undu wa damu.

"Kitu cha kwanza ambacho niliulizia kilikuwa ni mama yangu ana hali gani? Yuko sawa? Je ameweza kuwa salama?

"Kusema ukweli sikuwa na wasi wasi kuhusu mimi mwenyewe tena, Nilikuwa nafikiria jinsi ya kuondokana na maumivu niliyokuwa ninayahisi. Kusikia tu kwamba kila mtu ameweza kupona, Niliweza kupumua tena ."

Wakati aliana anaposema mtu mwingine yeyote, hamaanishi yeye binafsi na mama yake, kwasababu wanawake wengine wawili - madada - pia walifanyiwa upasuaji .

Moja ya viungo vya Aliana kilitakiwa kuwekwa kwa mmoja wa madada zake, na kingine kilitakiwa kwenda kwa mama yake Aliana. Maisha ya watu wawili yalikuwa yanaokolewa , huku watu wawili wakitoa viungo vyao kwa watu wasio wajua ili kuyaokoma maisha ya mwana familia wao.

Upasuaji ulikuwa ni matokeo ya miaka miwili ya kazi kubwa ambayo ilikuwa na manufaa. Aliana alikuwa amemuaoko mama yake Erosalyn dhidi ya miaka mingi ya matibabu ya -dialysis, ugonjwa na uwezekano wa kufa- na mtu ambaye hamfuhamu kabisa andeendelea na maisha mapya.

Mafigo ni viungo pekee ambavyo mtu hai anaweza kumpatia mtu mwingine kama msaada, kwani wengi wetu tumezaliwa na mafigo mawili, lakini tunahitaji figo moja tu kufanya kazi mwilini mwetu.

Lakini watu wanaohitaji figo mara nyingi huwa hawawezi kuchukua figo kutoka kwa mtu wanayempenda, hata kama mtu yule yuko tayari kuwapatia.

Kote duniani mafigo 150,000 yalipandikizwa kwenye wagonjwa mwaka 2019-idadi hii ikiwa ni sehemu ndogo tu ya wale wanaohitaji kiungo hicho.

Alvin Roth alipokea tuzo ya uchumi kutoka Wakfu wa Nobel mwaka 2012 kwa kazi yake ya kutengeneza kifaa cha mfumo wa kusaidia watu wengi kutoa na kupokea mafigo.

"Tofauti na viungo vingi, inawezekana kwa mtu kutoa figo yake kwa mtu ampendaye na kuyanusuru maisha yake ," anaelezea.

"Lakini wakati mwingine hawawezi kuchukua figo yako hata kama afya yako inatosha kutoa figo moja. Na labda Mimi ni mtoaji mwenye figo sawa na yako, Ningependa kutoa figo kwa mtu fulani nimpendaye lakini siwezi.

"Lakini labda figo yangu inaweza kufanya kazi kwa mgonjwa wako na figo yako inaweza kufanya kazi kwa mgonjwa wangu. Hiyo ndio aina ya ubadilishanaji wa figo ambapo watoaji wawili wasio fahamiana wa figo hukutana , na kila mmoja kupata figo inayoendana na kila mmoja wa wagonjwa wao."

Kazi ya Alvin Roth na wenzake iliweza kutengeneza mfumo ambao umeweza kusaidia ubadilishanaji wa figo, kwa hiyo kwa sasa kila mwaka maelfu ya maisha yanaokolewa.

Aliana hakuweza kubadilishana figo na ama yake kwasababu madaktari walihofia kuwa matatizo ya figo aliyo nayo mama yake huenda yakawa ni ya urithi, kwahiyo Aliana huenda akawa nayo pia.

Alitaka bado kumsaidia mama yake kupata figo mpya lakini muda ulikuwa unayoyoma, kwahiyo alianza kufanya utafiti na kubani kuwa inawezekana kubadilishana seehmu ya ini kwa figo.

"Nilianza kufanya utafiti, aina za viungo ambavyo vinaweza kutolewa wakati mtu akiwa hai. Na ini ndilo lililojitokeza sana."

Unaweza pia kusoma:

Aliana hakujua kwamba huu ulikuwa ni uwezekano wa kinadharia tu na haukua upasuaji wa mara kwa mara. Alianza kupigia simu hospitali kuona iwapo anaweza kutoa sehemu ya ini lake kwa mtu fulani ili mtu huyo ampe figo mama yake.

Aliana anasema hospitali chache hazikuelewa alikuwa ana maanisha nini : "Hospitali chache zilinielekeza niende kwenye nyumba za kuhifadhia maiti, kwasababu hawakujua nilikuwa ninazungumza kuhusu nini."

Hatimaye alimpata mtu sahihi kwa ajili ya kazi hiyo. John Roberts daktari wa upasuaji katika Chuo kikuu cha San Francisco kilichopo California Marekani.

Kwa msaada wa hospitali waliwapata madada wawili ambao wangekutanishwa na Aliana na mama yake.

Mmoja wa madada hao angepata sehemu ya figo ya Aliana, na Mama yake Aliana angepata figo mpya kutoka kwa dada mwingine.

Aliana hajuti, na ni kwanini anafikiria ni kwanini wengi wetu hatufanyi hivyo? "Ninafikiria watu hawapendi wazo la kutoa msaada wa kiungo, kwasababu ya hofu.

Unaweza pia kutazama: