Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Mzozo wa Tigray Ethiopia: Makumi wauawa katika shambulio la anga katika kambi, asema mhudumu wa misaada
Watu hamsini na sita wameuawa na wengine makumi kadhaa zaidi kujeruhiwa katika shambulio la ndege kwenye kambi ya wakimbizi wa ndani kaskazini mwa Ethiopia , anasema mhudumu wa misaada.
Picha zilizotumwa kwenye mitandao ya kijamii zinaonyesha watu wapkipokea matibabu baada ya shambulizi kwenye shule moja iliyopo katika mji wa Dedebit, katika jimbo la Ethiopia la Tigray.
Hakuna ripoti huru zinazothibitisha shambalio hilo.
Vikosi vya serikali ya Ethiopia vimekuwa vikipigana na wasi wa katiak jimbo la Tigray katika vita vya zaidi ya mwaka mmoja ambavyo vimewauwa maelfu ya watu.
Taarifa ya mashambulio ya hivi karibuni inajiri huku Serikali ya Ethiopia ikisema kuwa itawaachilia huru viongozi maarifu wa kadhaa wa upinzani kama sehemu ya sherehe ya taifa ya Krismasi ya dini ya Orthodox.
Akizungumza Ijumaa, Waziri mkuu Abiy Ahmed alisema kuwa hatua hiyo inalenga kufikia maridhiano na kuboresha "umoja " wa taifa.
Viongozi wa waasi wa Tigrayan People's Liberation Front (TPLF) atakuwa miongoni mwa wale watakaopewa msamaha.
Vikosi vya serikali vimekuwa vikipambana na waasi kwa zaidi ya mwaka katika vita ambavyo vimegarimu maelfu ya maisha.
Msamaha wa kushitukiza umekuja huku kukiwa hali ya wasi wasi kutokana na mzozo wa miezi 15, ambapo hivi karibuni vikosi vya serikali vilishuhudiwa vikuchukua miji kadhaa iliyodhibitiwa na waasi.
Ikitangaza msamaha mpya, huduma ya serikali ya mawasiliano ilisema katika taarifa kwamba "ufunguo wa mazungumzo ya kudumu ni mazungumzo. Ethiopia itafanya kila liwezekanalo kumaliza hili ".
"Lengo lake ni kutoa njia kwa ajili ya suluhu la kutosha kwa mmatatizo ya Ethiopia kwa amani, njia isiyo ya ghasia... hususan kwa lengo la kufanikisha mazungumzo yote ya kitaifa," ilisema taarifa.
Lakini haikuelezewa zaidi kuhuhu mazungumzo na waasi wa TPLF, ambao mwezi uliopita walisema kuwa walikuwa tayari kwa mazungumzo iwapo serikali itawaachilia wafungwa wa kisiasa na kumaliza mapigano ya miezi saba ya Tigray ambayo yamezuwia miaasa na madawa kupelekwa katika jimbo hilo.
Kulingana na vyombo vya habari vya kitaifa , miongoni mwa viongozi maarufu wa TPLF watakaoachiliwa chini ya msamaha ni Sibhat Nega, mjumbe muasisi wa chama , na Abay Weldu, rais wa zamani wa jimbo la Tigray.
Viongozi kutoka makundi mengine ya kikabila pia wameachiliwa, akiwemo mwandishi wa habari Eskender Nega na kiongozi wa upinzani Jawar Mohammed.
Msamaha huo umekuja wakati ziara ya mjumbe maalum wa Marekani nchini humo Envoy Jeffrey Feltman, ambaye mara kwa mara amekuwa akisisitizia kufanyika kwa mazungumzo ili kumaliza mzozo ambao umeliyumbisha taifa la pili kwa umaarufu zaidi Afrika.
Bw Feltman, ambaye alitangaza mapema wiki hii kwamba ataacha kazi yake kufikia mwishoni mwa mwezi huu, alifanya kile ambacho wizara ya mambo yan je ya Marekani ilikiita "mazungumzo yanayojenga, nay a maana"na maafisa wa serikali mjini Adis Ababa siku ya Alhamisi.
Vikosi vya TPLF ambavyo vimesonga hadi katika eneo la kilomita 300 (maili 186 ) kutoka mji mkuu, Addis Ababa, viekuwa vikilazimishwa kurejea nyuma katika wiki za hivi karibunibaada ya mashambulizi kutoka vikosi vya serikali.
Mzozo wa Tigray uliibuka Novemba 2020 baada ay Bw Abiy kuamrisha mahsmbulio ya kijeshi dhidi ya vikosi vya kikanda katika eneo hilo.
Alisema alifanya hivyo kujibu shambulio walilofanya kwenye ngome ya jeshi yenye wanajeshi wa serikali.
Unaweza pia kusoma:
- Jinsi Waziri Mkuu Abiy alivyoongoza vita kuwasukuma nyuma waasi
- Waziri mkuu wa Ethiopia akiri vikosi vya Eritrea vipo Tigray
- Ethiopia yatwaa tena mji wa urithi wa dunia-Serikali
- 'Nimepoteza mkono wangu mwanajeshi akijaribu kunibaka'
- Waziri Mkuu wa Ethiopia atoa idhini ya kushambuliwa kwa mji mkuu wa Tigray
- Ushahidi unaoonesha jinsi jeshi la Ethiopia lilivyofanya mauaji Tigray
Mapigano yaliongezeka baada ya miezi ya uhasama baina ya serikali ya Bw Abiy na viongozi wa TPLF.