Machafuko Kazakhstan: Kwanini kumekuwa na fujo na vifo?

Iliyochapishwa

Vikosi vya usalama nchini Kazakhstan vinasema vimewauwa makumi ya waandamanaji katika mji mku , Almaty, ili kuzima ghasia kubwa za waandamanaji.

Maafisa 13 wa usalama wameuawa, huku mamia zaidi wakijeruhiwa katika ghasia.

Maandamano yalifuatia kupanda juu kwa bei ya mafuta.

Kazakhstan iko wapi nani aina gani ya nchi?

Kazakhstanni nchi kubwa, yenye ukubwa sawa na eneo zima la Ulaya magharibi, ikiwa katikati ya Asia inapakana na Ueusi pamoja na Uchina.

Ni nchi yenye milima mingi na ardhi kavu, yenye watu milioni 19 pekee.

Ilipata uhuru wake mwaka 1991, kufuatia kuvunjika kwa Muungano wa Usovieti.

Nchi hii ina baadhi ya hifadhi kubwa zaidi za utajiri wa mafuta duniani. Huzalisha mapipa milioni 1.6 ya mafuta kila siku na imevutia uwekezaji wa kigeni wa mabilioni ya dola.

Hatahivyo, utajiri wake bado haujawafikia watu wa kawaida , wenye wastani wa kipato cha chini ya pauni 2,500 kwa mwaka.

Kwa miaka 18, Kazakhstan iliongozwa na Rais Nursultan Nazarbayev - mjumbe wa zamani wa chama cha Kikomunisti ambaye amekuwa na mahusiano makubwa na rai swa Urusi Vladimir Putin.

Sanamu ya Bw Nazarbayev ilisimamishwa na alijenga mji mkuu mpya Astana, ambao baadaye ulipewa jina jipya la Nur-Sultan kwa heshima yake.

Aliondoka mamlakani mwaka 2019, na kutoa fursa kwa rais wa sasa Kassym-Jomart Tokayev.

Maandamano ya umma katika nchi a Kazakhstan ni kinyume cha sheria bila idhini a serikali, na migomo ya awali na maandamano ilishugulikiwa vikali.

Nini kimetokea nchini Kazakhstan?

Maandamano yalianza tarehe 2 Januari katika mji Zhanaozen, kitovu cha mafuta na eneo ambalo limekuwa la makabiliano makali baina ya waandamanaji na polisi kwa zaidi ya siku 10.

Maandamano hayo baadaye yalisambaa kote katika maneo mengine ya nchi.

Vikosi vya usalama vinasema viliwauwa waandamanaji wenye fujo katika mji wa Almaty walipokuwa wakijaribu kurejesha usalama. Polisi inasema waandamanaji walijaribu kuchukua udhibiti wa vituo vya polisi katika mji huo.

Takriban maafisa 12 wa usalma wameuawa na wengine 353 walijeruhiwa, kulingana na polisi.

Takriban watu wapatao 1,000 wameripotiwa kujeruhiwa katika nchi nzima, huku 400 wakiendelea kutibiwa katika hospitali na makumi kadhaa wakilazwa katika vyumba vya wagonjwa mahututi.

Ni kwanini ghasia ziliibuka?

Maandamano yalianza wakati serikali ilipoongeza bei mafuta ya (LPG).

Wakazakhistan wengu waliyageuza magari yao kutumia mafuta ya LPG kwasababu nafuu kuliko petroli nyingine.

Hatahivyo, serikali ilisema haiwezi kupunguza bei ya mafuta aina ya LPG na uamuzi hauwezi kubadilika kwakuwa mchakato wa kuyatengeneza umeifanya bei yake iongezeke mara dufu.

Hatahivyo, waandamanaji walionekana kuwa na malalamiko mengine. Baadhi walipaza sauti zao huku wakitaja jina la Bw Nazarbayev na kujaribu kuangusha sanamu yake ya shaba.

Baada ya kuondoka madarakani, Bw Nazarbayev aliendelea kushikilia wadhifa wadhifa wenye mamlaka katika seikali kama mkuu wa baraza la usalama la Kazakhstan.

Pia alionekana kumuandaa binti yake Dariga kama kiongozi ajaye, kulingana waangalizi.

Katika kujibu waandamanaji, Bw Nazarbayev ameondolewa kwenye wadhifa wake

Kwanini Urusi inahusika?

Vikosi vya Urusi vya uingiliaji kati vya Urusi vimetumwa nchini Kazakhstan kwa ombi la rais wa Kazakhistan kusaidia''kuimarisha'' nchi.

Walitumwa chini ya mamlaka ya shirika la Mkataba wa pamoja (CSTO).

Hiki ni kikundi cha nchi zinazojumuisha, Kazakhstan, Belarus, Tajikistan, Kyrgyzstan na Armenia, kilichoundwa baada ya kuvunjika kwa Muungano wa Usoviet.

CSTO, ambacho kwa sasa kinaongozwa na Armenia, amelaumu tatizo katika Almaty kutokana na "uvamisi wa ujambazi uliobuniwa na kupewa mafunzo kutoka ng'ambo ".

Urusi iko makini kuongeza uwepo wa jeshi lake uliopo tayari Kazakhstan kulinda malik ama vile mabomba ya gesi, ngome za jeshi la Urusi na kituo cha anga za mbali cha urusi kilichopo katika Baikonur.

Nini kitakachofuatia?

Serikali ya Kazakhstan inafanya makubaliano.

Imesitisha mpango wa kuondoa viwango vyake vya bei kweney mafuta LPG - na kuagiza bei mafuta yote ya magari kudhibitiwa kwa miezi sita.

Mawaziri pia wamejiuzulu.

Rais Kassym-Jomart Tokayev alisema kuwa serikali ilishindwa kufanya "moja ya majukumu yake makuu-kufuatilia na kudhibiti viwango vya bei".

Rais amemteua Alikhan Smailov kama kaimu waziri mkuu.

Marekani imewataka maafisa wa kazakhistan kuonyesha "subra", akisema waandamanaji wanapaswa "kujieleza kwa njia ya amani ".