Shambulio la Capitol Marekani: Waandamanaji wenye ghasia walishikilia sime kwenye koo la Marekani - Biden

Rais Joe Biden wa Marekani amemkosoa vikali rais wa zamani Donald Trump katika maadhimisho yake kwanza ya shambulio dhidi ya Bunge la Marekani -US Capitol.
Katika hotuba aliyoitoa kupitia televisheni Bw Biden alimshutumu mtangulizi wake kwa kusambaza "wavuti wa uongo" uliosababisha mashambulio ya kundi la watu.
Wafuasi wa Bw Trump walivamia jengo la Capitol tarehe 6 Januari 2021 wakati kikao cha wabunge wa congress kilipokuwa kimekaa kuidhinisha ushindi wa urais wa Bw Biden.

Picha za moja kwa moja za wanasiasa wa Marekani waliokuwa wakitoroka kundi la wafuasi ziliishangaza dunia.
Bw Trump alikuwa amewataka waandamanaji waliokuwa wamekongamana nje ya Ikulu ya White House muda mfupi kabla ya tukio hilo, kuandamana kwa "amani'' katika congress, lakini aliwashawishi ku ''pigana'' na kuuchochea umati huo kwa madai yasiyokuwa na ushahidi ya wizi mkubwa wa kura katika uchaguzi ambao alikuwa ameshindwa.
Muda mfupi baada ya hotuba ya Bw Biden siku ya Alhamisi Bw Trump alitoa taarifa ya jazba dhidi ya mrithi wake. Katika taarifa hiyo, alimshutumu Bw Biden kwa "kushindwa" na akarudia madai ya uongo kuhusu uchaguzi.
Wanasiasa wa Democrat , ambao walikuwa na wingi wa kura kayika baraza la Congress la Marekani, walipanga matukio kadhaa ya kuadhimisha mwaka mmoja wa shambulio- ukiwemo usiku wa kuwasha mishumaa nje ya jengo la Capitol.
Wengi walizungumzia kuhusu uzoefu wao wa siku hiyo, ikiwa ni pamoja na hofu waliyokuwa nayo na kujificha waandamanaji wenye ghasia pamoja na wafanyakazi vijana.
Kamati ya bunge inafanya uchunguzi, na hadi sasa uchunguzi umekwisha wakamata washukiwa 725 kuhusiana na ghasia hizo.
'Sime kwenye koola demokrasia ya Marekani '
Bw Biden aliwalaani washambuliaji na Bw Trump katika hotuba yake ya Alhamisi, akitumia baadhi ya lugha kali kuhsuu maandamano ya ghasia na mtangulizi wake
"Wale walioshambulia Capitol na wale waliochochea tukio hili, walishikilia sime kwenye koo la Marekani na demokrasia ya Marekani ", Alisema Bw Biden katika Ukumbi wa Statuary, eneo la Capitol ambalo lilivukwa na waandamanaji wenye ghasia.
"Walikuja hapa kwa ghasia, sio kwa ajili ya kuihudumia Marekani, bali kumhudumia mwanaume mmoja.
"Rais wa zamani wa Marekani alisambaza kwa mtandao wa uongo kuhusu uchaguzi wa mwaka 20202…Majivuno yake yalikuwa muhimu zaidi kwake... kuliko demokrasia yetu au katiba yetu".
Kiongozi huyo wa Marekani pia alionya kwamba vitisho kwa demokrasia ya Marekani "havijapungua."
'Taifa lililodidimia- jinsi dunia ilivyoshuhudia fujo za Capitol
Baadaye Alhamisi Spika wa bunge la Congress Nancy Pelosi aliongoza kipindi cha kukaa kimya katika ukumbi wa bunge. Aliwasifia maafisa wa polisi waliowalinda wabunge na watu wengine walikuwa wamejificha ndani ya jengo la bunge wakati fujo zilipotawala bungeni.
"Waasi walilenga zaidi ya jengo. Waliilenga demokrasia yenyewe," alisema.
Baadhi ya wabunge wa chama cha Rublican hawakuhudhuria kongamano la maadhimisho ya sambulio hilo. Kiongozi wa seneti wa chama hicho, Mitch McConnell, aliongoza ujumbe kwenye mazishi ya seneta wa zamani Atlanta, Georgia.
Wakati huo huo mbunge wa congress wa Florida Matt Gaetz na mbunge wa Georgia Marjorie Taylor Greene - ambao ni wabunge wawili wanaoonyesha wazi uungaji mkono wao kwa Trump walifanya mkutano na waandishi wa habari katika Capitol kama njia ya "jibu la Republican" kuhusiana na matukio ya siku.
Walirejelea tena nadharia zisizokuwa na Ushahidi kwamba shambulio lilichochewa na maafisa wa usalama.
Mama yake Ashli Babblit, mwanajeshi wa zamani wa kikosi cha US Air Force ambaye alikufa baada ya kupigwa risasi na polisi wakati alipokuwa akijaribu kuvamia bunge la wawakili, pia alizungumza nje ya Congress.
"Alikuwa mzalendo. Alihudumia nchi hii katika maisha yake yote ya utu uzima ," Micki Witthoeft aliliambia shirika la utangazaji lenye makao yake Alabama- Right Side Broadcasting Network.
Seneta wa Republican Lindsey Graham,katika ujumbe wake wa Twitter, alimhutumu Bw Biden kwa "kuwasha moto wa kisiasa " kwa kutumia fujo za tarehe 6 Januari.













