Amelia Tiganus: 'Niliitwa kahaba baada ya kubakwa na wanaume watano'

Chanzo cha picha, Cèlia Atset
Alibakwa na wanaume watano nchini Romania akiwa na umri wa miaka 13. Lakini badala ya kuchukuliwa na mwathirika wa unyanyasaji wa kingono alitengwa na jamii iliyomzunguka. "Nilibadikwa jina la 'kahaba'," alisimulia BBC Mundo.
Majambazi ambao wanajinufaisha kiuchumi kwa kuwanyanyasa wanawake kingono walimkamata akiwa na umri wa miaka 17 na kumuuza kwa wanaowatafutia wateja wafnyabishara ya ukahaba kwa euro 300 (karibu dola 340 za Kimarekani).
Na kwa miaka mitano alifanya ukahaba katika zaidi ya madanguro 40 kote nchini Uhispania, akivumilia kile alichoelezea kuwa "ukatili", katika maeneo ambayo hasiti kufafanua kama "kambi za kuzuilia watu".
Lakini Amelia Tiganus, mzaliwa wa Galati, mji wa Romania, aliponea madhila yote hayo aliyopitia na sio hayo tu bali,
alifanikiwa kuacha nyuma ulimwengu wa ukahaba na leo hii anapambana na walea ambao wanaendelea na biashara hiyo na kuwalinda wale wanaokabiliw ana hatari ya kujiunga na mtindo huo hatari wa maisha.
Amekuwa msemaji, mwandishi na mwanaharakati wa kupinga ukahaba,kigezo cha kutetea haki za wanawake nchini Uhispania ambako anaendelea kuishi. Anaandaa warsha ya kuzungumza katika shule tofauti na hivi karibuni amechapisha kitabu kwa jina "The revolt of the whores" (Ediciones B), kinachoangazia kwa undani jinamizi la ukahaba nchini.
Je ushawahi kuwa kahaba. Umenyanyaswa kingono kwa muda gani?
Kwa miaka mitano, kutoka 2002 hadi 2007, nikiwa na miaka 18 hadi 23.
Hali hii ilianzaje? Mtu anaanza vipi kuwa kahaba?
Baada ya miaka hiyo yote , kwa sababu ni miaka mingi kwani naelekea kufikisha miaka 38, kwa kiwango kidogo nimewaza kuelewa kazi hii inavyoendeshwa.
Nikiwa kwenye mfumo wa ukahaba, niliweza kufanya kazi hiyo bila hofu kwani haikuwa makosa yangu, lakini baada ye niliikubali kwa kuwa nilesema "ndio" bila ya kuwa na vifaa vya kuniwezesha kuchanganua mazingira yaliyonifanya nikubali kuwa kahaba".
Sasa naona wazi hali hii ikijirudia, sio tu katika historia yangu lakini pia miongoni mwa wanawake wengi ambao wanaishia kufanywa makahaba.
Ni hali gani?
Kwa upande mmoja ni umasikini. Lakini pia unyanayasaji wa kingono ambao yalitukabili tukiwa na umri mdogo na baadaye kutengwa na jamii inayotuzunguka wakati ilikuwa na jukumu la kutulinda.
Wakati jamii inapotutenga, inatuacha katika mazingira magumu san ana tunapaswa kuishi.
Hali ambayo inakuwa rahisi kwa watu wanaowatafutia makahaba wateja kutufikia.
Kwako mwenyewe, nini kilitokea?
Nilizaliwa mwaka 1984 inchini Romania, katika familia iliyokuwa ikijimudu kimaisha kwani ilikuwa ikifanya kazi.
Hata hivyo, hakuna kitu kilichoashiria siku moja atakuwa 'kahaba' ijapokuwa jamii imeamua kulifumbia macho suala hilo
Alikuwa msichana mwerevu sana shuleni na alikuwa na ndoto ya kuwa daktari.
Lakini kila kitu kilibadilika alipokuwa na miaka 13. ''Nilibakwa karibu na mlango wa nyumba yetu nikitoka shuleni.''
Hapo ndhio Maisha yake yalibadilika. Sio tu kwasababu ya kubakwa, bali pia mambo mengine yaliyofuata baada ya kitendo hicho.
Nini kilifanyika baada ya kubakwa na wanaume watano?
Kilichofuata nji jinsi jamii ilivyochukulia kitendo hicho kwa ukali na kumlimbikizia lawama mwathirika.
Ni kitu ambacho tunashuhudia mara kwa, wakati tunapoona mwathiriwa akilaumiwa kwa hali iliyomkabili na kufukuzwa kijijini au kutengwa.
Niliteseka sana baada ya kitendo hicho hadi nikaacha shule , kwasababu ya kuzomewea na wanafunzi wenzangu. Tayari nilikwa nimebandikwa jina la "kahaba ".

Chanzo cha picha, Zsófia Sákán
Ina maana baada ya kubakwa na wanaume watano, jamii yake haikumchukulia kama mwathirika, badala yake ilimlaumu kwa unyanyasaji huo wa kijinsia?
Naam, kwa kweli inasikitisha. Hili ni jambo tunaendelea kushuhudia.
Kwanza baadhi ya watu wanajiuliza mwanamke alikuwa katika mazingira gani, amevalia vipi na wengine wanasema mbona hakutoroka... ISuala linalojitokeza ni kuhoji hatia ya mwathirika.
Hali hiyo iliniathiri sana, kwa kuwa sikupata suluhisho, nilipofikisha miaka 17 nilishauriwa kuhusu uwezekano wa kuja Uhispania.
Waliyonishauri waliahidi kusuluhisha matatizo yangu maishani ndani ya miaka michache, wanaowatafutia wateja wafanyabiashara wa ukahaba hutumia sana maneno hayo kuwashawishi wasichana huku wakitumia pesa kama chambo cha kusuluhisha matatizo yao ya kimaisha.
Hatuambii ukweli kwamba tutakuwa tukijilimbikizia madeni, hawatuambii madhara ya kimwili, kisaikolojia na kiafya yatakanayo na ukahaba, na pia nilikuwa mdogo waliponichukua.
Kutokana na hali iliyokuwa ikinikabili nilisema "ndio." Na pale unapokubali, jamii na wanaoendesha biashara ya ukahaba wanakuchukulia kuwa unastahili kufikwa mambo yote mabaya.
Mazingira yaliyotufanya kukubali kujiingeza katika ukahaba hayazingatiwi ndio maana tunanyanyaswa kingono, wakati wanaoendesha biashara hiyo wanajinufaisha kifedha huku wateja wao wakifurahia kuwatumia kingono wasichana wadogo wasiokuwa na njia ya kujiondoa katika mtandao huo haramu.
Kama sijakosea, uliuzwa Romania kwa gawadi wa Uhispani kwa 300 euros. Sio?
Naam, ni kweli waliniuza kwa gawadi wa Uhispani wa kwa euro 300.
Na haikuwa biashara ya kawaida, ilijumuisha utekaji. Ilikuwa kama mkataba wa maelewano na ni jambo la kwaida.
"Tunakuunganisha na huyu mtu ambaye anakufanyia hisani," waliniambia, kwas ababu kila wakati mazungumzo yao yaliashiria kuwa wananifanyia hisani, na wanatimiza ombi langu..
"Kisha utamlipa hizo euro 300 euros (karibu dola 340) pamoja na gela ya kugharamia pasipoti, tngo na safari...".
Kwa hiyo nilikuwa na deni la zaidi ya euro 3,000 (karibu dola 3,400 za Kimarekani).












