"Mwanaume aliyenifanya niwe kahaba ndio mwanaume huyohuyo, mume na baba wa watoto"

Chanzo cha picha, BBC MUNDO
Sonia Sánchez ni mzaliwa wa Villa Ángela, jimbo la Chaco, Argentina, alizaliwa mwaka 1964. Anapozungumzia masuala ya biashara ya ngono anazungumza kitu anachokielewa kwa undani.
Kwa miaka sita, akiwa na umri wa miaka 16 mpaka 22, alikumbana na unyanyasaji mkubwa wa kingono.
Alijiingiza kwenye biashara ya ukahaba, wakati huo akisaka maisha mazuri, alipoamua kuondoka kwenye mji aliokuwa akiishi na kwenda katika mji wa Buenos Aires, kufanya kazi za ndani.
Lakini akapoteza kazi yake, na kujikuta akiwa hana uelekeo mtaani na huko safari yake ya kuuza mwili wake ikaanza rasmi.
Alitumia nguvu na jitihada kubwa kujiondoa katika biashara hiyo.
Tangu wakati huo, aliamua kuijitolea kuelimisha umma kuhusu dhamha za biashara ya ukahaba akielimisha hasa vijana, kama jitihada za kuwalinda wasichana na vijana kwa ujumla wasitumbukie kwenye biashara ya ukahaba.

"Watu kama nyie hampaswi kuwa na watoto": ni kauli ya mwanamke mmoja anayeishi na virusi vya Ukimwi ambaye anazituhumu mamlaka za nchi hiyo kumuhasi bila ridhaa yake.
Sánchez amezungumza na BBC na kueleza kuwa 'Majina kama kahaba, changudoa na mengineyo ni kupunguza tu ukweli halisi.
Biashara ya ngono inatajwa kuwa ni biashara ya muda mrefu zaidi duniani, lakini unaweza kuhoji kwamba hakuna mwanamke aliyezaliwa kufanya biashara hiyo.
Hivyo ndivyo ilivyo. Naamini hilo kwamba hakuna mwanamke aliyezaliwa kufanya hivyo, ila wanasababisha tuwe hivyo.
Waliniingiza kwenye biashara hiyo nikiwa na miaka 16, nikawa kahaba kwa miaka sita na mhanga wa biashara ya kusafirisha binadamu kwa miaka mitano. Hakuna mwanamke anayezaliwa kuwa fuska. Wanatufanya tuwe hivyo "
Unaweza kujinasua vipi kwenye Biashara hii?
Ili kujinasua na yote niliyopita, niliwaza mambo mengi, baadhi ya vitu naweza kukumbuka
Sijui kwa namna gani nilijinasua kwenye biashara hiyo, Argentina ukweli sijui, naweza kusema hapana sijui ".
Nilitoka huko na kwenda Buenos Aires. Huko nikaendelea na biashara kwa mwaka mmoja zaidi.
Mpaka saiku moja nilipokumbana na kipigo cha kutisha . Nilisaidiwa na mhudumu wa hoteli, ambaye alipiga simu Polisi. Lakini huwezi amini walinikamata mie badala ya aliyekuwa akinipiga. Kwa sababu hakuna anayejali'.

Chanzo cha picha, Getty Images
Nini athari za biashara ya ngono?
Kitu cha kwanza ni inaondoa utu na utambulisho wako, na inakufanya kuwa kama chombo tu kinachotumika na kutelekezwa
Kama wafanyabiashara ya ngono ni makahaba, je wateja wao tuwaitaje?
Kahaba hana wateja, kwa sababu sio benki au duka. Wote wanaowafuata nao ni makahaba.

Chanzo cha picha, Getty Images
Makahaba hawa ni kina nani?
Waume zetu, kaka zetu, majaji wetu, wanasiasa wetu, wachungaji wetu, karibu wanaume wa aina zote.
Una watoto?
Namna gani ya kukwepa kuingia kwenye ukahaba?
Watoto wanapaswa kuelimishwa kuhusu biashara hii wakiwa mashuleni, shule za msingi, sekondari na vyuoni...
kwa njia hii tu tunaweza kuwalinda watoto wetu wasiingie kwenye biashara ya ngono na mabinti wasiwe makahaba.













