Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Tetesi za Soka Ulaya Ijumaa 17.12.2021: Rudiger, Haaland, Aubameyang, De Jong, Martial, Loftus-Cheek, Meslier
Mshambuliaji wa Borussia Dortmund na Norway Erling Braut Haaland, 21, ameonya Barcelona kwamba hatafikiria kuhamia Nou Camp isipokuwa tu klabu hiyo itakapocheza Ligi ya Mabingwa mwaka ujao.(Sport, via Star)
Kocha wa Roma Jose Mourinho anakaribia kuishawishi klabu yake ya zamani Chelsea na ofa ya kiungo wa kati wa Uingereza Ruben Loftus-Cheek, 25.(11 Romanista,via Sun)
Manchester United wana nia ya kutaka kumnunua mlinzi wa Chelsea na Ujerumani Antonio Rudiger, 28, na wana matumaini kwamba Ralf Rangnick anaweza kuwasaidia kuishinda Real Madrid, Paris St-Germain na Bayern Munich kwenye usajili wake.(Bild,via Mail)
Rudiger, ambaye mkataba wake unamalizika msimu wa joto, anapanga kuondoka Chelsea baada ya kupewa ofa ya chini ya pauni 140,000 kwa wiki ambayo kiungo wa kati wa Uingereza Mason Mount, 22, amepewa ofa ya kusaini mkataba mpya.(FootballInsider)
Mchezaji anayefuatiliwa na Manchester United Frenkie de Jong, 24, angekataa fursa ya kuhamia Old Trafford kutoka Barcelona Januari kwa sababu ya hali ya hewa ya Uingereza, kulingana na baba wa kiungo huyo wa kati wa Uholanzi.(AD,via Express)
Manchester United ina mbadala ikiwa tayari mshambuliaji Mfaransa Anthony Martial, 26, ataondoka huku winga wa Uswidi Anthony Elanga, 19, akikaribia kusaini mkataba mpya baada ya kumvutia kocha mpya Ralf Rangnick.(Telegraph)
Arsenal wanavutiwa na kiungo wa kati wa Juventus na Brazil Arthur Melo, 25, pamoja na winga wa Uswidi mwenye umri wa miaka 21 Dejan Kulusevski.(Calciomercato-in Italian)
Everton wana nia ya kumsajili beki wa kushoto wa Dynamo Kiev wa Ukraine Vitaliy Mykolenko, 25, kwa £20m. (Liverpool Echo)
Manchester United wamemtambua Illan Meslier wa Leeds United kama mlinda mlango bora chipukizi nchini Uingereza - lakini walipomtuma mlinda mlango Tony Coton kumtazama Mfaransa huyo mwenye umri wa miaka 21, aliruhusu mabao saba huko Manchester City Jumanne.(Mail)
Everton ni miongoni mwa vilabu kadhaa vya Ligi ya Primia vinavyomuwinda mlinzi wa kulia wa Metz Mfaransa Fabien Centonze, 25.(Football Insider)
Kiungo wa zamani wa Arsenal Emmanuel Frimpong ameitaka klabu hiyo kumuuza Pierre-Emerick Aubameyang baada ya mshambuliaji huyo wa Gabon, 32, kuvuliwa unahodha.(Sun)
Mkurugenzi wa michezo wa Monaco Paul Mitchell amezionya Manchester United na Chelsea kwamba kiungo wa kati wa Ufaransa Aurelien Tchouameni mwenye umri wa miaka 21 hatakuwa bei nafuu.(Tuttosport,via Metro)
Newcastle United imekuwa ikifuatilia kwa makini talanta katika michuano ya mabingwa, huku mshambuliaji wa Luton mwenye umri wa miaka 23 Muingereza Elijah Adebayo akilengwa.(Newcastle Chronicle)