Mbinu za hali ya juu za waajemi wa kale za kuweka nyumba zao baridi zinawoweza kutumiwa sasa

Iliyochapishwa

Mji wa Yazd kwenye jangwa na Iran ulikuwa kitovu na ubunifu na ugunduzi wa hali ya juu.

Mji huu una majengo ya kale ya uvundi wa juu ukiwemo mjengo wa kupoza wa chini ya ardhi, mfumo wa unyunyizaji wa chini ya ardhi na hata mfumo wa kutuma ujumbe ulio wa umri wa miaka 2,000 zaidi ya huduma za posta nchini Marekani.

Kati ya teknolojia hizo za kale kuna zinazofahamika kama badgi au vikamata upepo.

Ni kawaida kuona miundo hii kwenye paa za majengo ya miji. Inaweza kuwa ya minara ya mstatili, ingawa inaweza kuwa ya duara, mraba, mstatili au kuwa maumbo mengine maridadi.

Yazdi unatajiwa kuwa na vikamata upepo vingi zaidi duniani, licha kuwa vimetokea nchini Misri

Lakini mjini Yazd sasa vikawa vya lazima , kuifanya sehemu yenye joto ya jangwa la Iran kuwa bora kuishi.

Licha kuwa mingi ya miundo hii haitumiki kwa sasa, imewavutia wasomi na wahandisi kuona iwapo wanaweza kutusadia wakati huu kupata baridi kwenye dunia inayopata joto.

Kwa kuwa haiitaji umeme kufanya kazi, gharama yake ni ya chini na salama kwa mazingira

Inafanya kazi kwa njia gani

Kuna mifumo miwili inayoingiza hewa kupitia kwa kikamata upepo hadi kwa jengo kwa njia fulani ambapo hewa yenye joto inakaa sehemu ya juu ya hewa baridi ya jangawa.

Hewa inaingia kupitia mashimo ya kikamata upepo na kupitishwa kwenda kwa nyumba ikiacha mchanga chini ya mnara.

Kisha inagia kwenye nyumba, wakati mwingine kupitia hifadhi za maji yanayoipoza hata zaidi.

Hili husababisha hewa yenye joto iliyo ndani kupaa na kutoka nje ya nyumba kupitia mnara ikisaidiwa na msukumo ulio ndani ya nyumba.

Matumizi ya hewa katika kupoza majengo ni ya kitambo kuanzia wakati mazingira ya jangwa yaliana kufurika watu. Baadhi ya tekenolojia za kwanza za kushika upepo ni za kutoka misri za miaka 3,300 iliyopita kwa mujibu wa watafiti Chris Soelberg na Julie Rich.

Mfumo wakati huo ilihusu majengo yenye kuta nene, madirisha machache yanayoangalia jua, mianya upande mmoja ya hewa kuingilia na shimo la kutokea hewa upande mwingine.

Baadhi wanasema kuwa mwanzo wa kikamata upepo ni Iran yenyewe. Haijalishi viligunduliwa wapi lakini vilitumiwa sana mashariki ya kati na Kaskazini mwa Afrika.

Hata hivyo inakisiwa kuwa ustaarabu wa kiajemi ulibadilisha muundo huo na kuufanya bora zaidi.

Kufutia kuwepo mazingira ya joto miundo hi ilipata umarufu sana huko Yazd.

Ulitambuliwa kuwa eneo la kitamaduni na shirikala UNESCO mwaka 2017.

Kikamata upepo kwa jina Dowlatabad, chenye urefu wa mita 33, kinatajwa kuwa kirefu zaidi duniani na ni kati ya vile vinavyofanya kazi hadi sasa.

Uwezo wa siku zijazo

Kwa sababu ya uwezo wake wa kupoza bila kutoa gesi, kuna watafiti wanaopendekeza kuwa tunastahili tena kufikia kuvitumia.

Parham Kheirkhah Sangdeh kutoka chuo cha Ilam nchini Iran amevifanyia utafiti mkubwa

Leo hii teknolojia ya sasa ya kupoza hutumia mafuta ya kisukuku na kemikali ambazo huzalisha gesi chafu ikiwa zitaachiliwa kwenda hewani.

Kuibuka kwa teklojia za friji inalaumiwa kwa kudorora kwa mbinu za kitamaduni nchini Iran, kwa mujibu wa mwanahistoria wa Iran Elizabeth Beazley mwaka 1977.

Kheirkhah Sangdeh ana matumaini kuwa vikamata upepo hivi vinaweza kuboreshwa na kuwa njia bora isiyohitaji nishati nyingi ya kupoza majengo.

Huko Palemo nchini Italia, watafiti wamegundua kuwa kutokana na hali yake ya upepo inafaa kuwekeza katika ujenzi ya vikamata upepo hivi vya Iran.

Oktoba iliyopita kikamata upepo kilipata umaarufu kwenye maonyesho ya kimataifa ya Dubai.

Huku watafiti kama Kheirkhah Sangdeh wakidai kuwa kikamata upopo kina manufaa mengi zaidi ya kupoza nyumba bila kutumia mafuta, teknolojia hii tayari inatumiwa kuliko vile unadhani.

Kwa hivyo wakati mwingine ukiona mnara juu ya duka la jumla, jengo refu au shule, angalia vizuri, yawezekana unatazama kikamata upepo cha Iran.