Je mizozo kati ya ndugu ina mwisho wake?

Iliyochapishwa

Wakati Roseanne alikuwa mdogo, anasema kulikuwa na mizozo kati yake na ndugu zake mapacha walio wadogo kwake kwa miaka mitatu.

"Waliokuwa pamoja sana , wakiwa kundi lao, kwa hivyo kawaida ilikuwa ni wawili dhidi ya mmoja, anasema Rosean, mama mwenye umri wa miaka 46 anayeishi New Jersey nchini Marekani.

Baadhi ya mizozo hiyo hudumu, anasema, hata sasa, na unaweza kuhisi kuwa hakuna kitu kimebadilika tangu utotoni. "Tulikuwa tofauti sana sana. Tulihisi kana kwamba tulikuwa kwenye dunia tofauti na nafikiri hiyo ndiyo sehemu ya tatizo kwa watoto wangu wawili sasa."

Roseanne ana mtoto wa kiume wa umri wa miaka 16 na msichana mwenye umri wa miaka 14 ambao hawajapatana tangu walipokuwa shule ya chekechea. "Mabishano yanachosha," anasema.

Kwa muda mrefu, tumezuia kufanya vitu vingi pamoja kama familia kwa sababu hatutaki kuyasikia.

Hatuwezi kukaa meza moja kwa chakula cha jioni kwa dakika 10 bila suala fulani kuibuka. Kila wakati wana hofu kati yao, wakichokozana."

Ndugu hupigana. Karibu kila mmtu aliye na ndugu anafahamu hilo. Ushindani wa aina fulani upo.

"Watoto wana uwezo mdogo kuliko watu wazima kufahamu kile kinachoweza kuwakasirisha au kuweka misukumo yao pembeni. Kwa hivyo watazozana sana vile sote tunafahamu," aansema Dr Raymond Raad, muasisi mwenza kwa RIVIA Mind, kituo cha cha afya ya akili mjini New York.

Kwenye famialia nyingi ugomvi baina ya ndugu na kama malezi. Inasaida watoto kushughulikia mizozo na kuwafanya bora katika kuingiliana na wengine.

Kwa wengine, ushindani hupungua wanapofika utu uzima na kuwa kitu cha kucheka kwenye sherehe za familia.

Mizizo kati ya ndugu haionekani kuleta wasiwasi utotoni. Lakini wengine kama Roseanne, bado wanahosi mizozo hiyo siku nyingi baada ya kucha kuishi nyumba moja. Ni kwa ni ni ushindani huu hudumu - na je tunaweza kuumaliza?

Ulinganisho na migogoro

"Kama wanadamu, tuna tabia za kulingansiha," anasema Shawn D Whitehead, profesa wa masuala ya ukuaji wa mwandamu na yale ya famialia katika chuo cha Utah nchini Marekani.

"Ndugu huwa na tabia ya ulinganisho. Wako nyumbani kwako, wakikua na wewe. Wako katika mzingira sawa, nyumba moja kwa hivyo wanatupa ulinganisho ulio bora."

Kwa mfano, ni rahisi kwa ndugu kulinganisha mafanikio yao kielimu au kushindana kuhusu ni nani anayependwa kwa kuwa mara nyingi wana uzoefu sawa kama wa kuhudhuria shule moja.

Na wakati umri wa watoto unakaribina sana ndivyo mizozo inakuwa mingi.

Whitehead anasema baadhi ya ndugu hujaribu kujitofautisha katika jitihada za kuzuia ushindani - hususan wakati umri wao unakaribiana sana. "Hiyyo inaweza kupunguza mizozo, kwa mujibu wa Whitehead lakini utafiti umechanganyika."

Hilo linakubaliana na tuko la Rosean: na kaka zake na pia watoto wake, anasema kuwa tofauti inaweza kuwa chanzo cha mzozo.

Binti yake Roseanne ana kipaji cha riadha, huku mwanawe akiwa na kipaji cha masomo. Roseanne anasema kuwa bintiye ni lazima afanye bidii zaidi kupata alama nzuri shuleni, tofati zao zimekuwa za mara kwa mara. "Walimu wengi na hata jamaa zangu wametoa maoni jinsi mwanangu alivyo na akili," anasema Roseanne. "Ninajua ni kitu kinachomsumbua binti yangu."

Suala la haki

Kitu kinginine kinachozua mizozo kati ya ndugu ni haki, suala ambalo Whitehead anasema ni muhimu sana kwa watoto.

"Wazazi wana tabia ya kuwapenda watoto wadojo kuliko vile walivyowafanya wale wakubwa," anasema.

"Kama mzazi, wakati unamuambia mtoto wa umri wa miak a12 kuwa "unaweza kukaa macho hado saa nne, labda yule wa miaka 10 naye anafanya hivyo kwa sababu wazazi hawataki mizozo.

"Wakati watoto wa umri mdogo wanapata ruhusa mapema kuliko vile wale wakubwa walikuwa wanapata, yaweza kusababisha wale wakubwa kuhisi kuwa mambo hayako sawa. Hilo linasabaisha mzozo," anaongeza Whitehead.

Katika utu uzima maswali kuhusu usawa kati ya ndugu huchangia masuala kama mafanikio ya kitaaluma, jinsi watu waanavyofurahia ndoa zao na mengine mengi, anaongeza Raad.

"Tofauti na marafiki, ambapo unaweza kusema, oh, tuko tofauti tunatoka maeneo tofauti, kuna hili suala kuwa ndugu wanatoka katika malezi sawa, kwa hivyo kitu kinapaswa kuwa sawa kuhusu mahala wanapoishia."

Kusukuma kwa upole

Mizozo kati ya ndugu watu wazima sio lazima iwe mibaya.

Zaidi ya robo ya waliohojiwa kwenye utafiti wa OnePoll wanasema wanashindana na ndugu na dada zao kuhusu malengo yao ya kitaaluma na asilimia 15 ya waliohojiwa walisema ushindani umewachochea katika taaluma zao.

Kwa karibu waialia kati ya 10 ya watu wazima, kuna iamnia kuwa mizio kati ya nddi mecannia wao kutimzia maengo yao maishani.

Haijalishi kuwa kila kundi la ndudu litashindana kwa maisha yao yote. Kwa wengine mzozo hutoweka wanapofika utu uzima. Wataalamu wanasema kuwa hakuna sababu ni kwa nini mizozo hutokewa kwa baadhi ya familia na kwa familia zingine.

Wataalamu wanasema wazazi wanaweza kusaidia watoto wadogo kupunguza mzozo na kuwapusha kuzozana siku za baadaye.

"Wazazi wanastahili kuwa mfano bora wa kutatua mizozo," anasema Raad. "Unaweza kuwa na mzozo nyumbani mwako, lakini namna unaweza kuutataua mzozo huo yaweza kuwasaidia watoto wako siku za baadaye."