Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Utafiti mpya: Dunia iliibuka kutoka baharini ikianzia nchini India
Je Singhbhun lilikuwa bara la kwanza dunia? Je Singhbhiun huko Jharkhand na baadhi ya maeneo jirani ya Odisha yalikuwa ya kwanza kutoka baharini?
Je Singhbhun lilikuwa eneo la kwanza baada ya kuzaliwa kwa dunia ambapo kipande cha kwanza cha dunia kilichozama baharini kiliibuka kama bara?
Kulingana na utafiti mpya, jibu ni 'ndio'.
Kwa mujibu wa utafiri uliochapiswa wiki iliyopita kwenye jarida maarufu nchini Marekani la 'Proceedings of the National Academy of Science (PNAS)', bara la Singhbhum lilizaliwa miaka milioni 310 iliyopita, eneo hili liliubuka kutoka majini kwa mara ya kwanza.
Wakati huo ardhi ilikuwa chini ya bahari. Lakini eneo hii la dunai (Singhbhum Craton) liliibuka kutoka baharini kutuatia mlipuko mkubwa wa volkeno uliotokea kilomita 50 ndani ya dunia.
Ni nani anashiriki kwenye utafiti?
Makala ya utafiti imeandikwa na watafiti nane kutoka Australia, Ujerumani na Marekani baada ya utafiti wa siku nyingi. Kata ya hawa, wanne ni wa asili ya India wanaoishi ng'ambo. Muandishi mkuu ni Dr. Priyadarshi Choudhury, mtafiti katika chuo cha Monash nchini Australia.
Dr. Chaudhuri ni wa asilia ya India mwneye umri wa miaka 33. Jamaa zake wanaishi mji wa Asansol, West Bengal. Alipata masomo yake kutoka chuo cha Jadavpur cha Asansol huko Kolkata. Alishi Ujerumani kuanzia mwaka 2013 hadi mwaka 2018. Kutoka huko alipata shada yake ya uzamili. Kwa kipindi cha miaka miatatu amekuwa Australia na amekuwa akifanya utafiti kuhusu asili ya mabara ya dunia.
Dr. Priyadarshi Chaudhuri aliiambia BBC, "Baada ya miaka miwili unusu ya utafiti eneo la Singhbhum, tunaweza kusema kuwa Singhbhum lilikuwa bara la kwanza. Singhbhum tunamaanisha eneo kubwa na sio tu Singhbhum la Jharkhand. Pia inajumuisha maeneo kama Dhaljori, Keonjhar, Mahagiri na Simlipal huko Odisha.
Suryajendu Bhattacharya, Shubhojit Roy, Shubham Mukherjee (wote wa asili ya Indian) Jacob Mulder, Peter Kewood, Ashley Wainwright (wote raia wa Australia) na Oliver Nebel (kutoka Ujerumani ) walishiriki katika utafiti huu pamoja na Dr. Priyadarshi Choudhury.
Hivi ndivyo umri wa mawe ulikuja kujulikana
Kulingana na Dr. Priyadarshi "Ni vigumu kugundua umri wa mawe na mchanga. Tuliyaleta mawe yaliyopatikana huko Singhbhum chuoni mwenu na kuyasaga hadi laini. Kisha mawe hayo yakaangaliwa kwa kutumia hadubini.
Baada ya hilo yalifanyiwa majaribio ya kemikali na kisha umri wake ukabainishwa, anasema. Kemikali kwa jina Zircon inayopatikana kwenye mawe haya ilitusaidia kupata umri kamili wa mawe haya.
Alisema, "kutokana na utafiti wetu , tulifanikiwa kugundua kuwa bara la Singhbhum liliundwa takriban miaka milioni 310 iliyopita. Wakati huo milipuko ya volkano ilikuwa miepesi la ilielea kama vile theluji na kuibuka kutoka baharini. Kwa kipindi kilichofuatia, mabara mengi yaliundwa sehemu zingine duniani.
Kraton ni nini?
Mawe na mchangha mara kwa mara hujikusanya kwenye midomo ya mito na chini ya bahari.
Alama za mawimbi ya bahari zinaweza kuonekana kwenye mawe yanayopatikana Singhbhum. Alama hizo huenda zilitokana nakugongana na bahati kwa miaka mingi, hali iliyochangia kutokea alama hizo.
Mawe kama hayo yamepatikana kwenye mistu ya Chaibasa na Saranda huko Singhbhum, lakini utafiti kama huo umefanywa kwa mara ya kwanza.
Wakati huo huo kraton ni neno la kigiriki. Linamaanisha bara. Kulingnaa na wanajiolojia, kuna mabara au kraton 30 duniani na kumi yao ni makubwa. Kati ya mabara haya 10 manne yako nchini India.
Dr. Priyadarshi anasema kando na Singhbhum, kuna mabara ya Bastar, Bundelkhand na Dharwad nchini India. Ikimaanisha kuwa haya ndiyo mabara ya kwanza kabisa duniani. Mabara mengine ni Amerika, Australia na Afrika.
Umri wa dunia ni karibu miaka milioni 450. Kulingana na wanasayansi, Dunia ilikuwa moto sana wakati wa kuundwa kwake. Baada ya mamilioni ya miaka ilipoa na maji yakatengenezwa.
Singhbhum likawa moja ya mabara. Kutokana na kuwepo kwa mabara haya, kiwango cha hewa ya Oksijeni pia kikaongezeka ambapo chumvi na madini mengine yakatengezwa pamoja na maji ya bahari.
Manufaa ya utafiti ni yapi?
Dr. Priyadarshi anasema kuwa wakati dunia nzima inajadili kuhuus mabadliko ya hali ya hewa, ni muhimu kujua vile anga yetu, bahari, mabara na hali ya hewa ilikuja kuwa. Ni lazima tujue ni njia zipi za kijiografia kuwa dunia ilikuja kuwa ya kuishi wanadamu na wanyama.
Alisema kuwa utafiri huu ni sehemu tu ya mradi wetu mkubwa. Utafiti wa kina bado huajafanywa. Kuna uwezekano kuwa mafumbo mengi kuhusu dunia yatafichuliwa