Mazungumzo ya Biden na Xi Jinping: China yaionya Marekani dhidi ya kupigania uhuru wa Taiwan

Virtual meeting between Xi and Biden

Chanzo cha picha, Reuters

Iliyochapishwa

Rais wa China Xi Jinping amefanya mkutano na mwenzake wa Marekani rais Joe Biden kuonya kuwa kuhimiza uhuru wa Taiwan kutakuwa ni sawa na "kuchezea moto".

Mazungumzo hayo yanachukuliwa kuwa muhimu zaidi tangu Bw Biden aingie madarakani mwezi Januari.

Pande zote mbili zimesisitiza uhusiano wa kibinafsi wa viongozi hao wawili na mkutano huo ulikuwa ni jaribio la kupunguza mvutano.

Lakini hawakuweza kuepuka kuzungumzia mada moja tata zaidi ya kujitawala kwa kisiwa cha Taiwan.

China inaiona Taiwan kama jimbo lililojitenga na siku moja linaweza kuunganishwa tena na bara.

Marekani inatambua kuwa ina uhusiano rasmi na China. Lakini pia imeahidi kuisaidia Taiwan kujilinda endapo litatokea shambulizi.

Gazeti la serikali ya China Global Times lilisema Bw Xi alilaumu mvutano wa hivi karibuni kutokana na "majaribio ya mara kwa mara ya mamlaka ya Taiwan kutafuta uungwaji mkono wa Marekani kwa ajenda yao ya uhuru pamoja na nia ya baadhi ya Wamarekani kutumia Taiwan kuidhibiti China".

"Hatua kama hizo ni hatari sana, kama vile kucheza na moto. Yeyote anayecheza na moto atateketea," ilisema.

Ikulu ya Marekani ilisema Bw Biden "anapinga vikali juhudi za upande mmoja za kubadilisha hali iliyopo au kudhoofisha amani na utulivu katika kisiwa cha Taiwan".

U.S. President Biden speaks virtually with Chinese leader Xi from the White House in Washington

Chanzo cha picha, Reuters

Maelezo ya picha, Viongozi wakizungumza kwa njia ya simu ya video

Licha ya maneno makali kuhusu Taiwan, mkutano huo ulianza kwa viongozi wote wawili kusalimiana kwa furaha, huku Bw Xi akisema kuwa amefurahi kumuona "rafiki yake wa zamani" Bw Biden.

Bw Biden alisema wawili hao "kila mara walikuwa wanawasiliana vizuri kwa uaminifu ," na kuongeza kuwa hawakuwahi kuondoka wakiabaki kuwaza mwingine anafikiria nini."

"Bw Xi alisema nchi hizo mbili zinahitaji kuboresha "mawasiliano" na kukabiliana na changamoto kwa pamoja".

"Ubinadamu unaishi katika kijiji cha kimataifa, na tunakabiliwa na changamoto nyingi pamoja.

China na Marekani zinahitaji kuongeza mawasiliano na ushirikiano." alisema bwana Xi.

Mambo gani mengine yalizungumziwa?

Mataifa haya mawili yenye nguvu zaidi duniani hayakubaliani katika masuala kadhaa, na Bw Biden alielezea wasiwasi wa Marekani kuhusu ukiukwaji wa haki za binadamu huko Hong Kong na dhidi ya Uyghurs katika eneo la kaskazini-magharibi la Xinjiang.

China inaishutumu Marekani kwa kuingilia masuala yake ya ndani.

Kuhusu biashara, Bw Biden aliangazia "haja ya kuwalinda wafanyakazi na viwanda vya Marekani dhidi ya PRC ya [Jamhuri ya Watu wa China] biashara isiyozingatia haki na wazo sahihi la kiuchumi".

Bw Xi pia alionekana kutoa maoni makali kuhusu suala hilo, huku shirika la habari la Reuters likiripoti kwamba alimwambia Bw Biden kwamba Marekani inapaswa kuacha "kutumia vibaya dhana ya usalama wa taifa kukandamiza kampuni za China".

Mabadiliko ya tabia nchi pia yalijadiliwa. Wiki iliyopita wawili hao walishiriki katika tamko la pamoja la kushughulikia mabadiliko ya hali ya tabia nchi, katika mazungumzo huko Glasgow, Scotland.

Hii ilikuwa mara ya tatu kwa viongozi hao wawili kuzungumza tangu Biden aingie madarakani mwezi Januari. Mazungumzo hayo yalichukua muda wa saa tatu na nusu, muda mrefu kuliko ilivyotarajiwa.

Bw Xi hajawahi kutoka nje ya China kwa karibu miaka miwili, tangu mlipuko wa janga la Covid-19 uanze.

Uhusiano wa China na Marekani ni muhimu kwa pande zote mbili na dunia nzima, huku Beijing imetoa wito mara kwa mara kwa utawala mpya wa Washington kuboresha uhusiano ambao ulidorora chini ya mtangulizi wa Bw Biden, Donald Trump.

Wote wawili wanakabiliwa na masuala ya ndani ya nchi zao huku idadi ya kura ya Bw Biden ikishuka kutokana na mfumuko wa bei, tishio la virusi vya corona na kujiondoa kwa ghasia kutoka Afghanistan. Bw Xi anakabiliana na uhaba wa nishati na mzozo wa mali.

Presentational grey line

Uchambuzi

Mkutano huu umefanyika wakati ambao viongozi hawa wawili wenye nguvu zaidi duniani wanaamini kwamba uhasama wa wazi wa awali kati ya China na Marekani haukuwa na manufaa kwa yeyote kati yao na ulikuwa hatari.

Mazungumzo yao yalihusisha juu ya uhusiano wao kuwa mbaya na kutoleta manufaa yeyote kwa pande zote mbili.

kwa sehemu, jaribio la kuhakikisha kuwa ushindani kati ya China na Marekani hauelekei kwenye mzozo wa kivita kwa sababu ya kutoelewana katika eneo kubwa la kimataifa.

Kwa upande mmoja, labda tunapaswa kuwa na furaha sana kwamba wanaondoka kwenye vita kabla ya kutokea, lakini, kwa upande mwingine, ni jambo ambalo wamehisi hitaji la kufanya hivyo.

Kwa kweli, ukiangalia mkutano huu ni mambo mazuri zaidi yameonekana kwa muda mrefu katika mazungumzo ya viongozi wa China na Marekani.

Juhudi hizi za kufanya mijadala kuwa ya kupendeza kwa kupunga mkono, mazungumzo ya "kijiji cha kimataifa" na "changamoto za kibinadamu" zilikuwa mbali na msukosuko wa Alaska mwezi huu wa Machi wakati wawakilishi wakuu kutoka tawala zote mbili waliishia kubishana hadharani.

Hili halionekani kuwa jaribio la kweli la kuweka upya na tunapaswa kutarajia kubadilisha mahusiano ya kijiografia ya kimataifa kwa njia thabiti.

Presentational grey line