Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
"Askari hewa" wa Afghanistan walivyoikabidhi nchi hiyo kwa Taliban
"Hakuna angeweza kufikiri kuwa taifa hilo lingeanguka kirahisi namna hiyo."
Khalid Payenda, ambaye alikuwa waziri wa fedha wa mwisho wa Afghanistan kabla nchi hiyo haijaanguka mikononi mwa Taliban, akizungumzia hali ilivyokuwa kabla ya hali hiyo kutokea.
Katika mahojiano na BBC, afisa huyo asimulia kile kilichotokea mwishoni mwa mwezi Agosti na kueleza mtazamo wake juu ya kile anachokiona kuwa sababu kuu za kushindwa kwa serikali,iliyokuwa ikishirikiana na Marekani.
Makosa mawili alisema ,walikuwa wanajaribu kujenga jeshi kwa taswira ya Marekani - kwa misingi thabiti ya jeshi la anga - na uwezo wa kukabiliana na mikakati iliyofanywa na Taliban kutoa uhakika wa kupambana nao.
Lakini pia, ukweli ni kwamba wanaodai kuwa wanachama 300,000 ya wanajeshi wa Afghan hawakuepo .
Katika maoni yake, anaona walikuwa, "wanajeshi hewa."
"Hatukuwahi kuwa na jeshi kubwa kiasi hicho. Namna ambavyo walivyokuwa wanafanya ni kuuliza wakuu wa mikoa kuwa wana askari wangapi kwa kuzingatia gharama za matumizi na mishahara, na takwimu hizo na takwimu hizo zilikuwa zinaongezeka." , alihesabu.
Kwa mujibu wa Payend waliongeza majina ya watu ambao hawakuepo , na kutaka mishahara yao.
Alikadiria kuwa jeshi la Afghan litakuwa na kati ya watu 40,000 na 50,000 na wengine wote walikuwa feki.
"Na pia kuna wale ambao walikuwa wanaacha na pia askari wengine walikuwa wanauawa katika mapigano ambao hawakuhesabiwa kama majeruhi kwasababu baadhi ya makamanda walificha kadi zao za benki.
Takwimu zisizo sahihi
Wanamgambo wa Taliban walichukua udhibiti wa Afghanistan mnamo Agosti, wakati wanajeshi wa Marekani waliondoka baada ya miaka 20 katika taifa hilo.
Although initially the number of the Taliban (about 60,000 to 70,000) was believed to be lower than that of the military, it is now believed that the actual number of the armed forces was actually much lower
Ingawa idadi ya mwanzoni ya wanajeshi wa Taliban ilikuwa 60,000 mpaka 70,000 iliaminika kuwa iko chini zaidi ya jeshi la Afghan, sasa inaamininika kuwa idadi halisi ilikuwa chini zaidi.
Ripoti ya mwaka 2016 ya mkuu wa jeshi la Marekani la ujenzi (Sigar) ilisema namna ambavyo Marekani na washirika wake wa Afghan wanaojua idadi halisi ya wanajeshi wa Afghan na polisi ambao wapo, wangapi wapo kutoa huduma hiyo na uhalisia wa uwezo wao wa kufanya kazi.
Katika ripoti ya hivi karibuni, Sigar ilieleza wasiwasi wake kuhusu athari za ufisadi na uhakika wa takwimu ya wanajeshi waliopo.
Ufisadi ulivyoenea
Payenda, ambaye alijiuzulu na kuondoka Afghanistan wakati kundi la kiislamu lilipokaribia kuvamia, alisema wanajeshi wa Afghan pamoja na kuwa wachache kwa idadi , pia walikatishwa tamaa.
Askari wengi walikuwa hawalipwi vizuri na serikali na wakati mwingine wanakosa mishahara kabisa kwa muda.
Pia alibainisha kuwa kuna viongozi ambao walikuwa wanawaunga mkono wanamgambo wa Taliban ambao walikuwa wanapokea mshahara na malipo kutoka kwa Taliban walijisalimisha bila kupigana.
"Hisia za wote ilikuwa ni : 'Hatuwezi kubadili hali hii ya rushwa. Hivi ndivyo bunge linafanya kazi , pia magavana wanafanya kazi hivyo. Kila mtu atasema ni kuwa imeanzia ngazi ya juu mpaka chini, alisema.
Alisema rushwa imeenea sana katika masuala mbalimbali , kwa maofisa wa serikali na maofisa wa umma ambao hudai rushwa kwa ajili yao na wafuasi wao.
"Kuna mwanasiasa mmoja ambaye alikuja kuniambia : 'tumetoka kwenye uchaguzi tu na nmegharamika dola milioni kwa ajili ya wanachama wenzangu waweze kupata ushindi wa kuingia bungeni,'" anakumbuka.
Hata hivyo , alieleza kuwa haamini kama rais wa zamani Ashraf Ghani alikuwa anahusika na rushwa .
Katika majibu ya madai ya rushwa dhidi ya wizara ya fedha ambayo alikuwa akiisimamia mwenyewe, Payenda alisema mambo yalikuwa hayaendi sawa, lakini katika suala hili hapana."
Waziri wa zamani anaona wageni kutoka mataifa ya magharibi wanahusika kwa namna fulani kushindwa kwa Afghanistan , ingawa alieleza ushiriki wa Uomja wa Mataifa na NATO katika taifa hilo ni kukosekana kwa jambo muhimu.