Je, Instagram ni baraka au laana?

شعار إنستغرام

Chanzo cha picha, Reuters

Iliyochapishwa

Unapoamka asubuhi, unachukua simu yako ya mkononi, na kuanza kuvinjari mtandaoni.

Ni utaratibu ambao wengi wetu tunaufahamu. Lakini programu hiyo inaathiri vipi afya yetu ya akili.

Hivi karibuni, mkurugenzi mkuu wa zamani wa Facebook Frances Haugen ameonya kwamba Instagram ni "hatari zaidi kuliko mitandao mingine ya kijamii," baada ya utafiti wa kampuni hiyo kuonesha madhara yanayoweza kutokea kwa kuitumia.

Kuna wakati Instagram ilitangaza kuwa utafiti walioufanya unaonesha "kujikita kuelewa masuala magumu na magumu" huku wanasiasa wanaendelea kuchunguza madhara ya matumizi ya mitandao ya kijamii, BBC ilizungumza na wasichana watano kuhusu uzoefu wao kuhusu Instagram.

Inawajumuisha Jamii

Uhusiano wa Danny na Instagram ni uhusiano wa chuki ya mapenzi. Danny, mwenye umri wa miaka 29 kutoka South Wales anapata kipato chake kupitia Instagram na ameunda kundi la watu waliobadilisha jinsia mtandaoni.

Lakini ananyanyaswa na kupata matusi mengi kwa sababu ya muonekano wake.

Instagram ni baraka kubwa na laana kubwa maishani mwangu," Danny aliambia BBC.

"Unapokuwa na mtu uliyebadilisha jinsia na kuwa na akaunti isiyo ya kibinafsi kwenye tovuti, inakufanya uwe katika mazingira magumu, hata hivyo baadhi ya matamshi ya chuki ninayopokea mtandaoni yanakatisha tamaa."

"Maoni mabaya na ya kuudhi , kuna mtu alinitumia link ya page ambayo watu waliweka picha zangu na kunifanyia mzaha."

m

Frances Haugen aliiambia kamati ya House of Commons and Lords kwamba Instagram inazingatia "ulinganisho wa hali ya kijamii, maumbile ... na mtindo wa maisha ya watu, ambayo husababisha hasara athari kubwa kwa watoto."

Danny, ambaye ameshinda uraibu wa pombe, anasema anaelewa jinsi mitandao ya kijamii inavyoweza kuwa uraibu.

"Niliacha kunywa pombe miaka michache iliyopita, lakini ninahisi Instagram ni mbaya kwa wale walio na uraibu. Ni hisia sawa na wewe, ambapo unakuwa unahitaji kupata muda zaidi na zaidi wa kuendelea kutumia mtandao huo."

Bwana Nick Clegg, makamu wa rais wa masuala ya kimataifa katika kampuni ya Meta, inayomiliki mtandao wa Instagram, ametetea mtandao wa kijamii huo, akisema kuwa kuna wasichana wengi wanaoutumia.

Aliendelea kusema kuwa kampuni hiyo inafanyia kazi ya kukabiliana na matumizi mabaya ya Instagram na kuweka kipengele kiitwacho "Take a break"(pumzika) kinachowataka vijana wanaotumia programu hiyo kufunga programu hiyo.

Taswira ya Mwili

Hana hutumia saa sita hadi 10 kwa siku kwenye mitandao ya kijamii, ambayo amekuwa akiitumia tangu akiwa kijana mdogo.

Hana ana umri wa miaka 24 na anasoma katika Chuo Kikuu cha Magharibi mwa Scotland, na ana akaunti kwenye majukwaa yote makubwa ya mitandao ya kijamii: Facebook, Instagram, Twitter, Snapchat na Tik Tok.

"Kiukweli nina tabia mbaya ," anasema , "kitu cha kwanza ninachofanya ninapoamka asubuhi ni kupitia taarifa zote ninazopata katika mitandao."

"Pia hilo ndilo jambo la mwisho ninalofanya kabla ya kulala. Siku yangu yote inazunguka kwenye mitandao ya kijamii."

"Kwa hakika nina uraibu wa TikTok, na ninaweza kutumia kwa urahisi saa kadhaa kuivinjari. Najua ninapoteza muda wangu..na wakati mwingine, huwa najaribu kupunguza kufuatilia mitandao."

Hapa alikuwa akifuata "watu wenye ushawishi" kwenye Instagram ambao walikuwa wakimkosesha raha kwa muonekano wa mwili wake.

هنا دايلي

Ilinifanya niamini kuwa mwili wangu unapaswa kufanana na wao, na nilianza kuwa na matarajio yasiyo ya kweli ya kuwa mwanamitindo mwembamba. Niligundua kuwa hilo jambo ni baya kwa afya yangu ya akili, hivyo niliamua kuacha kuwafuatilia."

Kwa sasa nafuatilia akaunti zenye mtazamo chanya, na kuangalia picha zenye uhalisia badala ya hawa"washawishi".

"Niligundua kuwa sio sisi sote ni wanamitindo wenye ngozi nzuri wenye urefu wa karibu mita 2. Nilianza kufuata watu waliofanana zaidi na mimi, jambo ambalo liliongeza kujiamini kwangu."

Hapa alipokea maoni ya chuki kwenye Instagram.

"Nimekuwa na maoni kutoka kwa watu wakiniambia nipunguze uzito kwa sababu ninanenepa sana - Ilinifanya nichukie mwili wangu."

Mazingira magumu

Katika shule ya wasichana ya Hornsey kaskazini mwa London, Scarlett na Anissa alilizungumza na BBC na kusema kuwa wanafahamu hatari ya mitandao ya kijamii.

Scarlett ana umri wa miaka 15 na anatumia mitandao ya kijamii isipokuwa Facebook, ambayo hafikirii inafaa kwa watu wa umri wake.

"Ninafuata watu wanaochapisha kwenye YouTube kuhusu mitindo, kama vile Emma Chamberlain, ambaye ninapenda," Scarlett anasema.

سكارلِت وأنيسة
Maelezo ya picha, Sicarlett na Anisa wanatumia Instagram

Anisa, ambaye pia ana umri wa miaka 15, anasema huwa anabadilisha akaunti zake ili kuepuka maudhui hasi.

Lakini bado anaona mambo ambayo hataki kuyaona mtandaoni.

"Nimegundua kuwa baadhi ya akaunti za watu hutengeneza mazingira mabaya," anasema Anisa. "Kwa sababu mimi ni kijana, najua ni lazima niwe mwangalifu ili nisichanganye akili."

"Kama Muislamu, ninahisi kama kuna uwakilishi mbaya sana juu yetu...kwa hivyo nikikutana na aina hii ya maudhui, naacha kuyafuatilia."

Wasichana hao wawili wanasema pia walikuwa wanafurahia mitandao ya kijamii, haswa linapokuja suala la kupiga picha za video na marafiki.

"Nilijaribu mapishi mengi ya kupikia kupitia video za mtandaoni, na nilijifunza ujuzi mwingi kutokana na kutazama video mtandaoni," anasema Scarletta.

"Na kuna akaunti (kwenye mitandao ya kijamii) zilizo na ukweli wa kushangaza, maoni na vidokezo muhimu - bila shaka (tovuti hizi) sio zote mbaya, ingawa nyingine zinaweza kuwa na maudhui hai.

"Lakini ninapomwona msichana au mwanamke mrembo sana, nikiwa nimemaliza kubalehe, huwa najisikia vibaya kwa sababu kumwangalia kunanifanya nifikirie kuwa ni lazima nionekane sawa. Ilinifanya nijisikie kutojiamini."

"Nimeacha kufuatilia akaunti nyingi."

Lakini si wasichana wote wanaosoma wana akaunti za Instagram. Kwa mfano, Leah mwenye umri wa miaka 15, hakuruhusiwa na familia yake kufungua akaunti kwenye tovuti.

"Ni kwa sababu ya mambo yote mabaya kwenye tovuti, hivyo ninaamini uamuzi wa mama yangu uko sahihi," anasema Leah.

ليا

"Ningependa kuwa na uwezo wa kutumia mitandao ya kijamii kwa sababu marafiki zangu wote wanaitumia, na mimi najihisi siko mahali sahihi, lakini najua mitandao ya kijamii ina upande mbaya pia. Nimesikia simulizi nyingi kutoka kwa marafiki zangu wakitumiwa picha na video zisizofaa - vitu ambavyo kwa umri wao hawapaswi kuiona."

Mwezi Septemba, kampuni ya Meta ambayo bado ilikuwa Facebook wakati huo, iliamua kusitisha mpango wa kuanzisha tovuti ya Instagram kwa wale walio chini ya umri wa miaka 13.

Kampuni hiyo ilisema inatafuta wakati wa kusikiliza wazazi na wataalam, watunga sheria na wadhibiti," Adam Moseri, mkurugenzi wa Instagram anaeleza.