Yafahamu maeneo manne yenye mizozo ya muda mrefu kuhusu mipaka

th

Chanzo cha picha, Getty Images

Iliyochapishwa

Mizozo inayohusu sehemu hizi nne imekuwa ikiendelea kwa muda mrefu na kutishia amani duniani .

Ripoti za hivi punde zaeleeza kwamba China imetengez meli za kivita zinazofanana na za Marekani hatua inayohusishwa na mzozo kuhusu bahari ya Kusini mwa China .Kando na mizozo ya mipaka inayotokota katika sehemu nyingi za ulimwengu ,mizozo kuhusu sehemu hizi nne ina uwezo mkubwa wa kuwa tishio kwa amani na usalama duniani .

Baadhi ya mizozo hii imekuwa ikiendelea kwa muda mrefu na licha ya kutulizwa kwa muda ,wakati mwingine milipuko ya mapigano huhatarisha kabisa Maisha ya maelfu ya watu na kuzivutia nchi nyingi kujiingiza katika migogoro hiyo

Bahari ya China Kusini

Mapema mwaka huu, China ilishukiwa kufanya jaribio la kombora la hypersonic lenye uwezo wa kinyuklia - makombora ambayo yanaweza kuruka katika anga ya juu kwa zaidi ya mara tano ya kasi ya sauti - ambayo ilizua wasiwasi huko Washington.

Beijing baadaye ilikanusha taarifa hizo na kusema ilikuwa ni ukaguzi wa kawaida wa vyombo vya anga.

Jeshi la Wanamaji la Marekani mara kwa mara hufanya kile kinachoelezea kama misheni ya kawaida na meli za kijeshi katika Bahari ya Uchina Kusini, ambayo ni moja ya maeneo yenye mzozo zaidi ulimwenguni.

China inadai sehemu kubwa ya eneo hilo, lakini nchi jirani na Marekani hazikubaliani na msimamo huo.matayarisho ya uboreshaji wa jeshi la China yamehusishwa na uwezekano kwamba China inalenga kujilinda na kutetea umiliki wake wa eneo hilo linalozozaniwa.

th

Chanzo cha picha, Getty Images

Eneo hilo ni sehemu ya njia kuu ya usafirishaji inayotumiwa kusafirisha biashara ya zaidi ya $3 trilioni (£2.2 trilioni) kila mwaka.

Ufilipino, Brunei, Malaysia, Taiwan na Vietnam zote zimekuwa zikipinga madai ya Uchina kwa karibu Bahari yote kwa miongo kadhaa, lakini mvutano umeongezeka kwa kasi katika miaka ya hivi karibuni.

Marekani imeunga mkono nchi nyingi kati ya hizi katika mzozo huu wa eneo.

Beijing imekuwa ikitengeneza na kufanya majaribio ya makombora ya kuzuia meli za kivita kwa miaka.

Marekani imeonya kwamba katika miezi ya hivi karibuni China imekuwa ikipanua kwa kasi jeshi lake, ikiwa ni pamoja na uwezo wake wa nyuklia, huku hali ya wasiwasi ikiongezeka katika Bahari ya China Kusini.

Peninsula ya Korea

Vita vya Korea, vita kati ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Watu wa Korea (Korea Kaskazini) na Jamhuri ya Korea (Korea Kusini) vilisababisha angalau watu milioni 2.5 kupoteza maisha.

Vita vilifikia kiwango cha kimataifa mnamo Juni 1950 wakati Korea Kaskazini, iliposhauriwa na muungano wa Kisovieti, ilipovamia Korea Kusini na kulazimisja Marekani kuingilia kati ikihofia kusambaa wa ukomunisti .

th

Mgogoro wa Korea ni mzozo unaoendelea kutokana na mgawanyiko wa Korea kati ya Korea Kaskazini (Jamhuri ya Kidemokrasia ya Watu wa Korea) na Korea Kusini (Jamhuri ya Korea), ambazo zote zinadai kuwa serikali pekee halali ya Korea nzima . Mvutano ulizuka katika Vita vya Korea, vilivyodumu kutoka 1950 hadi 1953.

Licha ya mapigano kukoma. Mkataba rasmi wa amani haukuafikiwa na tangia hapo Korea zote zimesalia katika hali ya mzozo.Hatua hiyo imesababisha kutengwa kwa Korea kaskazini ambayo badala yake imeendeleza mipango ya kujenga silaha hatari zikiwemo zenye uwezo wa kinyuklia ikidai inalenga kujilinda .Vikwazo vya kimataifa kwa Korea Kaskazini pia vimetumiwa kujaribu kuileta nchi hiyo katika meza ya mazungumzo lakini bila mafanikio makubwa .

Jammu na Kashmir

Mzozo wa Kashmir ni mzozo wa eneo la juu la e Kashmir, haswa kati ya India na Pakistan, huku Uchina ikiwa nchi ya tatu katika mzozo huo .

Mzozo ulianza baada ya kugawanywa kwa India mnamo 1947 kwani India na Pakistani zilidai kuchukua jimbo la kifalme la Jammu na Kashmir.

th

Chanzo cha picha, AFP

Ni mzozo kuhusu eneo hilo ambao uliongezeka na kuwa vita vitatu kati ya India na Pakistan na mapigano mengine kadhaa ya silaha.

India inadhibiti takriban 55% ya eneo la ardhi la eneo linalojumuisha Jammu, Bonde la Kashmir, sehemu kubwa ya Ladakh, Glacier ya Siachen, na 70% ya wakazi wake; Pakistan inadhibiti takriban 35% ya eneo la ardhi linalojumuisha Azad Kashmir na Gilgit-Baltistan; na Uchina inadhibiti asilimia 20 iliyobaki ya eneo la ardhi ambalo linajumuisha eneo la Aksai Chin, Trakti ya Trans-Karakoram isiyokaliwa na watu wengi, na sehemu ya sekta ya Demchok.

Golan Heights, Ukanda wa Gaza na West Bank.

Katika vita vingine vya mwaka 1967, Israel iliikalia kwa mabavu Jerusalem Mashariki na Ukingo wa Magharibi, pamoja na sehemu kubwa ya Miinuko ya Golan ya Syria, Gaza na rasi ya Sinai ya Misri.

Wakimbizi wengi wa Kipalestina na vizazi vyao wanaishi Gaza na Ukingo wa Magharibi, na pia katika nchi jirani za Jordan, Syria na Lebanon.

th

Chanzo cha picha, Getty Images

Si wao wala vizazi vyao wameruhusiwa na Israel kurejea makwao - Israel inasema hili lingeishinda nchi hiyo na kutishia kuwepo kwake kama taifa la Kiyahudi.

Israel bado inakalia Ukingo wa Magharibi, na ingawa ilijiondoa kutoka Gaza Umoja wa Mataifa bado unakichukulia kipande hicho cha ardhi kama eneo linalokaliwa kwa mabavu.

Israel inadai Jerusalem nzima kama mji wake mkuu, huku Wapalestina wakidai Jerusalem Mashariki kama mji mkuu wa taifa la baadaye la Palestina. Marekani ni mojawapo ya nchi chache zinazotambua mji huo kama mji mkuu wa Israel.

Katika miaka 50 iliyopita Israeli imejenga makazi katika maeneo haya, ambapo zaidi ya Wayahudi wengi sasa wanaishi.

Wapalestina wanasema hizi ni kinyume cha sheria chini ya sheria za kimataifa na ni vikwazo kwa amani, lakini Israel inakanusha hilo.