Wahamiaji wa Belarus: Poland yahofia ongezeko la haraka la mapambano ya silaha mpakani

Iliyochapishwa
Muda wa kusoma: Dakika 3

Poland imeonya juu ya uwezekano wa kuongezeka haraka kwa idadi ya ''watu wenye silaha" kwenye mpaka wake na Belarus, ikihofia kuwa jirani yake anaweza kujaribu kufanya tukio la uchokozi dhidi ya wahamiaji wanaotaka kuvuka mpaka kuingia katika nchi za Muungano wa Ulaya.

Wanajeshi wa ziada wamepelekwa kweny mpaka huo baada ya umati wa watu wenye shauku kujaribu kukata waya wa uzio wa mpaka ili wavuke.

Poland, Muungano wa Ulaya na Nato wanasema Belarus imepanga tatizo, dai ambalo limepingwa a kiongozi wake.

Poland inasema inafunga mpaka wake mkuu unaovuka kuingia katika Kuznica.

Wajumbe wa Muungano wa EU na Nato Poland, Lithuania na Latvia zimeshuhudia ongezeko kubwa la idadi ya watu wanaojaribu kuingia katika nchi zao kinyume cha sheria kutoka Beralus katika miezi ya hivi karibuni kutoka Mashariki ya Kati na Asia.

Usiku wa kuamkia leo vipimo vya joto kwenye mpaka huo vilishuka hadi chini ya sifuri na wahamiaji kadhaa tayari wamekufa katika wiki za hivi karibuni. Wanaharakati wanasema wahamiaji-wengi wao wakiwa ni vijana lakini pia ni wanawake na watoto-wanatumiwa katika mchezo wa kisiasa baina ya Belarus ambayo sio mwanachama wa EU, inayoongozwa na kiongozi wa kiimla Alexander Lukashenko, na majirani zake.

Msemaji wa serikali ya Poland Piotr Muller alisema kuwa zaaidi ya wahamiaji 4,000 walikusanyika karibu na mpaka wa mashariki wa Poland na aliwaambia waandishi wa habari kwamba wakati fulani walitarajiwa " ongezeko la hali ... ambayo itakuwa ya silaha ".

TV ya Poland ilisemawengi wa wahamiaji waliokusanyika karibu na Kuznica walisindikizwa na watu wenye silaha na mbwa.

Mkuu wa wizara ya usalama ya Poland, Stanislaw Zaryn, alisema kuwa wahamiaji wanadhibitiwa na jeshi la Belarus. "Belarus inataka kusababisha tukio kuu, zaidi kwa risasi na majeruhi ," alisema naibu waziri wa mambo ya nje Piotr Wawrzyk said awali.

Waziri wa ulinzi wa ulinzi wa Belarus alipinga taarifa za Poland kama yasiyo na msingi na yasiyo na maana, na kuishutumu, Warsawkwa kukiuka makubaliano kwa kupeleka vikosi kwenye mpaka.

Muungano wa Ulaya unadai kwamba kiongozi wa Belarus anachochea kuingia kwa wakimbizi kama njia ya kulipiza kisasi dhidi ya vikwazo vya EU vilivyowekwa dhidi ya nchi yake.

Bw Lukashenko ameonya mara kwa mara kwamba serikali yake haitauzuwia tena umati wa watu kuingiakatika mataifa ya EU.

Lithuania imehamishia wanajeshi kwenye mpaka wake na Belarus kujiandaa na uwezekano wa kuingia kwa wimbi la wahamiaji.

Wakati huo huo, Marekani imemtaka Bw Lukashenko "kusitisha mara moja kampeni yake ya kupanga njama za kuwaingiza wahamiaji haramu.

Poland, ambayo imekuwa ikikosolewa kwa kuwarudisha nyuma wahamiaji na wakimbizi katika mpaka wake, amejibu kwa kujenga waya wa umeme.

Huku wakiwa na chakula kidogo na vinywaji, watu waliokwama kwenye mpaka walikuwa wanaumia, alisema Bw Ahmed.

Hali ya wasi wasi imeimarika Jumatatu wakati video ilivyotumwa kwenye mtandao wa kijamii zilizoonyeshwa wahamiaji wakiwemo wanawake na watoto, wakitembea kuelekea kwenye mpaka wa Poland na Belarus.

Video nyingine zilionyesha idadi kubwa ya wahamiaji wakisindikizwa na watu wenye silaha waliokua wamevaa nguo za kaki.

Katika picha nyingine zilizotumwa kwenye mitandao ya kijamii, umati wa watu unaonekana ukivunja uzio wa waya kwenye mpaka, lakini wakizuwiwa kupita na walinzi wa mpakani wa Poland.

Shirika la walinzi wa mpaka wa Beralus awali liliviambia vyombo vya habari kuwa zaidi ya ''wakimbizi'' 2,000 walikuwa wamejipanga mbele ya vikwazo vya Poland. Walikuwa wakielekea katika mataifa ya Muungano wa Ulaya'' ambako walitaka kuomba kulindwa'', lilisema shirika.