Moyo wako husimama unapopiga chafya?

Kupiga chafya kwa ghafla kunahusishwa na kuanza ghafla kwa kifafa, baadhi huja na matokeo mabaya.
Madaktari wanasema kupiga chafya kunasaidia kulinda mapafu dhidi ya kitu kingine chochote kinachoingia kwenye mapafu isipokuwa hewa.
Ni hewa tu inayoruhusiwa kuingia kwenye mapafu - ikiwa kuna kitu karibu na pua ambacho sio hewa itajaribu kuiondoa kwa nguvu, na kusababisha kupiga chafya.
Katika makala ya kina iliyochapishwa na jarida la Healthline Health kuhusu kupiga chafya linasema kupiga chafya ni muhimu kwa mwili wa binadamu, na kwa kawaida hakusababishi matatizo yoyote makubwa ya kiafya.
Jarida hilo linaeleza kuwa kupiga chafya ni njia ya muhimu ya kuondoa vitu visivyohitajika kutoka puani au kooni, na huja kwa nguvu wakati upepo ama hewa inapokuja bila maandalizi.
Moja ya kazi kubwa ya pua ni kusafisha hewa tunayovuta, yaani kuhakikisha hakuna uchafu wala ugonjwa wowote. Wakati mwingine uchafu unaweza kuingia kwenye pua na kuwa tatizo ambalo pia husababisha kupiga chafya.
'Chafya na kifo ni mtu na nduguye?
Baadhi ya watu wanasema kitendo cha kupiga chafya kiko karibu na kifo kwa sababu wakati mtu anapiga chafya anakuwa kama amerukwa na akili.
Lakini daktari alisema kwamba ilikuwa taarifa ya matibabu tu na haiko hivyo.
Alisema kupiga chafya ni kama kinga dhidi ya afya ya binadamu lakini mwili ukijaribu kutoa nguvu. "Sio suala la kifo, ni suala la afya."
"Inakuwa kama wazimu kwa sababu koo hufunga kwa sekunde moja lakini inapopiga chafya hufunguka."
"Haitaki kitu chochote zaidi ya hewa kuingia na kufanya eneo hilo lifungwe kiasi cha kuhisi kukimbilia kuzimu," alisema Dk Manya.
Nini kinamfanya mtu kupiga chafya?

Chanzo cha picha, Getty Images
Kuna sababu nyingi zinazosababisha mtu kupiga chafya, hiyo ni kwa mujibu wa Dk. Celeb Manya, mtaalamu katika Hospitali Kuu ya Gusau katika Jimbo la Zamfara.
Sabau hizo ni pamoja na kinga ya mwili, magonjwa kama mafua na kuvuta hewa yenye kemikali kama vile manukato na kadhalika.
Watafiti katika Chuo Kikuu cha Saarland wanasema katika utafiti wao walioufanya kwamba baadhi ya watu wanasema wanapiga chafya mara tu wanapokula na kushiba.
Wengine husema kwamba tamaa ya ngono pia huwafanya kupiga chafya.
Kulingana na hali ya mwili - ni nini kisicho na afya kinaweza kusababisha mtu kuwa na wasiwasi na kupiga chafya sana.
Mtaalamu huyo alisema baadhi ya watu hawapendi miili yao kuathiriwa na vitu vingine mfano vumbi la takataka au moshi ambapo chakula kinakuwa na harufu flani au kunusa kitu na wengine harufu kutoka kwa viumbe kama kuku wanapokuwa karibu husababisha kupiga chafya. - wengine hata Mende huwafanya kupiga chafya.
Kubana chafya kunaweza kuhatarisha maisha?
Watu hujaribu kubana kupiga chafya kwa sababu za kuhofia kunyanyapaliwa na wanaomzunguka katika jamii au kwa sababu zingine.
Baadhi hujaribu kufungua njia ya hewa polepole na wengine hubana hadi kupiga chafya polepole. Lakini madaktari wanasema kupiga chafya hakuwezi kuzuilika pale inapotokea.
Ni ngumu kuzuia kupiga chafya kwani husababisha kifo, Daktari anaeleza. Ingawa jarida la masuala ya afya la Healthline health linasema halijawahi kukutana na taarifa kuwa kupiga chafya kumesababisha kifo cha mtu, lakini haiwezi kusemwa kuwa haiwezekani mtu kufa kwa kubana kupiga chafya.
Anasema kuwa madhara yanayoweza kusababishwa na kupiga chafya yanaweza kuwa makubwa kama vile uvimbe kwenye ubongo na kupasuka koo na mapafu ambayo yote yanaweza kusababisha kifo.Kwa mujibu wa Dokta Manya, kama mtu ataendelea kupiga chafya, itamzuia kumlinda na ugonjwa wowote ule unaopaswa kulindwa kwa wakati huo.
Anasema sababu zinazosabisha mtu kupiga chafya ni ndogo na hazina madhara kwa mfano vumbi. Kwa mujibu wa Healthline, angalau mtu mmoja amepasuka koo kutokana na kupiga chafya, ambapo hawezi kuzungumza au kumeza chakula.
Matatizo mengine yanayosababishwa na kupiga chafya ni pamoja na kuvunjika mbavu na sikio na matatizo ya macho na pua.
Ko zuciya na daina aiki yayin atishawa?

Chanzo cha picha, Getty Images
Daktari anasema wakati mtu anapopiga chafya anapunguza kiwango cha mapigo ya moyo na shinikizo la damu. Anasema kwa mfano, ikiwa mapigo ya moyo ya mtu yanafikia mapigo 100 kwa dakika moja , muda wa kupiga chafya unashuka hadi mapigo 90 au 80, ndivyo pia shinikizo la damu la mtu inapoingia.
Jarida la afya linasema kuwa kupiga chafya hakusababishi mshtuko wa moyo, bali kunapunguza mapigo ya moyo.
Kupiga chafya kama madaktari wanavyoeleza ni njia salama ya kuwa na afya njema na kwa kawaida kuacha kupiga chafya hakusababishi chochote zaidi ya maumivu ya kichwa na viungo lakini wakati mwingine kuidhibiti inakuwa mbaya zaidi.
Jambo muhimu ni kutobana kupiga chafya , ruhusu mwili kupiga chafya pale inapohitajika.













