Fahamu Ehlers-Danlos syndrome, hali inayomzuwia mpishi kuonja chakula anachopika

Chanzo cha picha, AMY MAIDMENT
Loretta Harmes alikuwa hajawahi kula kwa miaka sita, lakini hajapoteza ari yake ya kupika. Hawezi hata kuonja chakula chake alichopika mwenyewe, lakini bado anapata wafuasi kwenye mtandao wa Instagram, ambako huwasilisha utaalam wake wa mapishi ya mtu anayepika asiye na uwezo wa kula kwa mdomo wake.
Loretta anatafuna kiazi na kuoonyesha sehemu yake ya ndani . Yeye na mama yake Julie wamekuwa wakiandaa chakula kwasababu wanafahamu kitakuwa ndio chakula chao cha mwisho.
Katika kipindi cha dakika, uchungu unaofahamu kuwa utalikamua tumbo lako kama taulo lililokamuliwa, ndivyo uchungu unavyokuuma kila wakati unapokunywa au kula kitu fulani.
Halafu utahisi maumivu na kuumwa, kana kwamba linataka kupasuka.
Licha ya hayo Loretta aliamua kupuuza maumivu na kufurahia muda aliokuwa nao katika jiko la familia, eneo ambalo ufundi wake wa mapishi ulishamiri tangu alipokuwa mtoto.
"Kuketi chini na kula na mama yangu na dada yangu kilikuwa ni kitu cha kufurahisha na cha ajabu. Walau tulijaribu na kuwa kama familia ya kawaida," anasema Loretta.
Ilikuwa ni mwaka 2015 na akiwa na umri wa miaka 23- Loretta alikuwa ameishi kwa chakula cha kimiminika kwa miaka kadhaa.

Chanzo cha picha, Loretta Herms
Lakini wakati huu, mtaalamu wa tumbo alimtaka Loretta kula chakula kigumu.
Nilitaka kuelewa kwanini Loretta anapokula hupata maumivu ya aina hiyo na wakati mwingine humaliza wiki kadhaa bila kuweza kupata haja kubwa.
Loretta alikuwa amesafiri siku ile kwenda hospitali ya St Mark mjini London ili awekewe mrija wa pua uingie kwenye utumbo mdogo kuchunguza utendaji kazi wa mfumo wake wa umeng'enyaji wa chakula.
Hatimaye, baada ya miaka mingi ya mateso alipata daktari ambaye alilichunguza matatizo yake.
Shauku tangu utotoni
Akiwa mtoto, Loretta na mlezi wake Mavis waliigiza aina mbali mbali za mapishi waliyoyatazama kwenye vipidi vya televisheni vya mashindano ya upishi .
"Alikuwa Malkia wa uokaji na kekii zake za maadhimisho ya siku ya kuzaliwa zilikuwa za kiufundi , " anasema Loretta.
"Dada yangu Abbie pampoja nami tulikuwa tukilamba sinia la kuoka keki mpaka linakua safi kutokana na utamu wa keki ."

Chanzo cha picha, Loretta Herms
Nyingi kati ya hadithi za vyakula alivyovipika zimechanganyikana na kumbukumbu za upendo na furaha za maisha yake.
Kila Alhamisi, familia yake ilikuwa inakuja katika nyumba ya Mavis kwa chakula cha mchana.
Loretta anakumbuka vyema akiwa ameketi kwenye meza na meza iliyojaa vyakula vilivookwa na vinginevyo vitamu.
Akiwa na umri wa miaka 11, Loretta aliipikia familia yake chakula cha jioni kila siku ya Jumanne, kwasababu mama yake alifanya kazi hadi masaa ya usiku.

Chanzo cha picha, Tangu alipokuwa mdogo, Loretta alikuwa na u
Alianza kuigiza jinsi mama yake anavyooka tambi za viazi, lakini baada ya muda mfupi alihitimu kutengeneza keki na supu. Alianza kutengeneza nyama za kusagwa na kuku vyakula vilivyopendwa na familia yake.
Akiwa na umri wa miaka 15, Loretta aliugua maradhi ya anorexia, ingawa anasema maradhi hayo yalidumu kwa chini ya mwaka mmoja. Akiwa katika umri wa miaka ya kubalehe pia alipata matatizo ya umeng'enyaji wa chakula. Lakini mara nyingi aliendelea kupika na kula kwa furaha.

Chanzo cha picha, Loretta Herms
Ulaji mbadala
Kwa wastani, huchukua miaka 10 hadi 14 kugundua tatizo alilonalo, anasema Dkt Alan Hakim wa taasisi ya Ehlers-Danlos Society, kwasababu dalili za ugonjwa hutofautiana baina ya wat una baadhi yake huwa zinaonekana kutohusiana na ugonjwa.
" Mtu anaweza kwenda kumuona daktari akiwa na hofu yake ya kibinafsi, bila kuwa na mtizamo wa jumla wa ugonjwa,"
"Ila pale tu mtu anapokuwa pindo la fundo ndipo inapogundulika kwamba ana dalili ."
Daktari anasema maradhi huwa na dalili mbali mbali.
Miaka sita baada ya mlo wake wa mwisho, Loretta anafahamu kwamba hatawahi kula kitu chochote wala kunywa hata glasi ya maji tena.
Analishwa kwa kutumia mfumo wa upitishaji wa chakula kwenye utumbo mdogo (TPN), hii ikimaanisha kwua ameunganishwa na mfuko mzito wa vimiminika kwa saa 18 kila siku ambao hukwepa mfumo wa umeng'enyaji wa chakula na kuingia moja kwa moja kwenye mfumo wa damu.
Mrija unaofahamika kama Hickman line hupita kwenye kifua na ndai ya mhipa mkubwa ambao huingia ndani ya moyo.

Chanzo cha picha, Loretta Herms
Matatizo ya afya
Alipomaliza shule, Loretta alichaguliwa kuingia shule ya kifahari mjini London. Alikuwa na matumaini ya kufuata nyayo za wapishi wengine maarufu. Hata hivyo aliweza tu kumaliza miaka mitatu tu kutokana na matatizo ya afya yake.
Akiwa na miaka 19, maumivu yalimfanya alale kitandani wakati wote.
"Mambo yalianza kuwa mabaya zaidi. Sikuweza kula au kupata haja kubwa kabisa na kwa miaka mitano iliyofuatia hali ilikuwa ya kutisha sikuweza hata kuamka'' , anasema.
Tatizo lilianza na daktarin ambaye aliamini kuwa kupoteza uzito wa mwili haraka kwa Loretta huenda kulisababishwa na kukataa kula kwasababu alitaka kupoteza uzito wa mwili.
Huduma za afya ya akili zilishirikishwa kumpatia ushauri wa kisaikolojia na Loretta alilazwa katika kitengo cha maradhi ya kushindwa kula. Alikuwa na uzito wa kilo 25.
Maradhi ya Ehlers-Danlos syndrome ni nini?
- Ehlers-Danlos ni kikundi cha hali 13 za kushindwa kwa mpangilio wa mfumo wam wili kunakoathiri uhusiano wa nyama za mwili. Nyama hizi husaidia, kulinda na kutengeneza nyama ningine na viungo mwilini
- Hupatikana katika Ngozi, mifupa, na mishipa kwa mfano.
- Kwa ugonjwa wa Loretta, nyama zilizoungana kwenye ukuta wa utumbo zimeharibika. Matokeo yake chakula hakiwezi kusafiri ipasavyo tumboni.
- Hali hiyo kwa ujumla husababisha kunyooka kwa viungo kusiko kwa kawaida, na kudhoofika kwa mwili.












