Mlipuko wakumbuka msikiti wa Afghanistan wakati wa ibada ya Ijumaa

Iliyochapishwa
Muda wa kusoma: Dakika 1

Takriban watu 30 wamethibitishwa kufariki huku wengine 32 wakijeruhiwa baada ya mlipuko kukumba msikiti wa waumini wa dhehebu la Shia wakati wa ibada ya Ijumaa katika mji wa pili kwa ukubwa wa Kandahar nchini Afghnistan.

Vyombo vya habari vinaripoti kwamba mlipuko huo ulitokea katika msikiti wa Imamu Bargash na kwamba idadi kubwa ya watu wameuawa.

Hatahivyo chanzo cha mlipuko huo hakijatajwa licha ya kwamba kuna tuhuma za mlipuaji wa kujitolea muhanga. Kundi la wapiganaji wa Taliban liliteka mji wa Kandahar, mji wa pili kwa ukubwa nchini Afghanistan tarehe 13 Agosti baada ya vita vikali.

Mwandishi wa BBC nchini Afghanistan Secunder Kermani , alituma ujumbe wa Twitter kwamba kundi la IS-K , tawi la Islamic State nchini humo , linatarajiwa kutangaza kwamba ndilo lililohusika na shambulio hilo.

Ijumaa iliopita , mlipuaji wa kujitolea muhanga alishambulia msikiti wa waumini wa dhehebu la Shia wakati wa ibada ya Ijumaa katika mji wa kaskazini wa Kunduz na kuwaua watu 50 . Kundi la IS-K tawi la Afghanistan lilisema kwamba lilitekeleza shambulio hilo , ambalo ndilo baya zaidi tangu vikosi vya Marekani kuondoka nchini humo mwezi Agosti.

Shahidi mmoja aliambia AFP kwamba alisikia milipuko mitatu katika lango kuu ambapo waumini hujiosha , na la tatu .

Msikiti huo ulikuwa umejaa wakati wa mlipuko na takriban ambyulensi 15 zilionekana katika eneo la tukio.

Vikosi vya Taliban vimeimarisha usalama katika eneo hilo na kuwataka raia kusaidia kutoa damu ili kuwasaidia waathiriwa, Reuters imeripoti..

Tutaendelea kukujuza......