Siku ya Afya ya Akili Duniani 2021: Jinsi kupata msaada kunategemea ni nani na uko wapi

Iliyochapishwa

Jumapili Oktoba 10, ni Siku ya Afya ya Akili Duniani, hafla ya ulimwengu ambayo inakusudia kuhamasisha jamii kuelewa juu ya hali ya afya ya akili.

Kauli mbiu ya mwaka huu, iliyowekwa na Shirikisho la Afya ya Akili Dunia(WFMH), ni 'Afya ya Akili katika Ulimwengu Usio na Usawa'.

Kati ya asilimia 75 na 95 ya watu wanaokabiliwa na matatizo ya afya ya kiakili katika nchi zenye mapato ya chini na zile za mapato ya wastani hawawezi kupata huduma kabisa, kulingana na WFMH. Hata hivyo, baadhi ya waathiriwa ambao wanaishi katika nchi tajiri pia wanatatizika kupata huduma ya afya wanayohitaji.

BBC imezungumza na mama wa mwathiriwa, mtoa huduma na mtaalamu wa magonjwa ya akili kutoka nchi tofauti kufahamu kwa nini waathiriwa wanatatizika kupata msaada.

Mgonjwa: 'Asipokua na kitambulisho, hapati matibabu'

Mara tu baada ya kuolewa, mume wa P Thiruchelvi alianza kumnyanyasa - hata "kumtesa" - anasema.

Thiruchelvi anasononeka akikumbuka madhila aliyopitia chini ya mume wake.

Alijifungua mtoto wa kiume lakini miaka kadhaa baada ya 2009, mume wake alimtelekeza katika hali ambayo ilimfanya kupata msongo wa mawazo.

Thiruchelvi na mwanawe waliachwa bila makazi, na mahitaji mengine ya kimsingi wilayani Gudalu, jimbo la Tamil Nadu kusini mwa India. Cha kusikitisha hakuwa na nyaraka za kuthibitisha yeye ni nani.

Alipoteza matumaini maishani baada ya kukosa wa kumsaidia.

Nchini India, ni vigumu sana kupata huduma yoyote ya afya bila ya kuwa na kitambulisho.

Sawa na wengine wengi, Thiruchelvi hakua na nyaraka ya kuthibitisha utambulisho na hakua na mahali maalum anapoishi , kumaaninisha hakuwa na uwezekano wa kupata kadi.

Bila ya kuwa na uwezo wa kupata matibabu katika hospitali za umma, hali ya afya ya akili ya Thirucheli ilizorota.

"Si kujua mahali paa kwenda aula kufanya. Niliingwa na mawazo ya kujitoa uhai," anasem.

Thiruchelvi alifanikiwa kufika makao makuu ya jimbo lake, Chennai, ambako alipata msaada kutoka kwa shirika la Banyan.

Wakati huo, Banyan ilikuwa inaendesha mradi unaowaangazia watu wasiokuwa na makazi.

Mambo yalibadilika kwa Thiruchelvi na mwanawe baada ya kupatana na shirika hilo - alipewa makazi ya muda katika hoteli moja na kuanza kupokea matibabu.

Leo, anajitegemea na kuwasiliana na familia zinazokabiliwa na changamoto za kiakili na kuziunganisha na mashirika yanayotoa huduma za afya.

Pia anafanya kazi na watoto ambao wazazi wao wanakabiliwa na matatizo ya kiakili kupata usaidizi.

Mhudumu wa afya: 'Lakini ni msaada gani unaopatikana?'

Mnamo mwaka wa 2014, Sunday Times ya Afrika Kusini iliripoti kuwa watu milioni 17 nchini walikuwa wakikabiliwa na msongo wa mawazo, matumizi mabaya ya dawa za kulevya, wasiwasi, na ugonjwa wa bipolar au schizophrenia.

Hii ni kutokana na utafiti wa awali uliofanywa na kitengo cha afya ya akili nchini Afrika Kusini, ambao ulibaini kuwa asilimia 30.3% ya watu wazima wanakabiliwa na aina fulani ya shida ya akili katika maisha.

Hii inamaanisha kuwa "thuluthi moja ya Waafrika Kusini wataugua ugonjwa wa akili ", kulingana na Philippa Reekie,mwanaharakati wa afya ya akili.

Anasema watu walio na umri kati ya miaka 15-hadi-25 wanakabiliwa na hatarizaidi ya kuathiriwa, na visa vya kujitoa uhai vinaendelea kuongezeka kila mwaka.

Lakini kuna uhaba wa wafanyikazi wa huduma ya afya ya akili, na ukosefu wa muda mrefu wa wataalam wa magonjwa ya akili.

"Hudma za afya ya jamii haina ufadhili ya kutosha," Reekie anasema. "Kuna huduma chache sana kwa watoto au vijana ambao wako katika hatari zaidi."

Reekie anasema kuna ukosefu mkubwa wa wodi za magonjwa ya akili katika hospitali za umma na uhaba mbaya zaidi wa taasisi za magonjwa ya akili nchini Afrika Kusini.

Tume ya Haki za Binadamu ya Afrika Kusini imeripoti juu ya usimamizi mbaya wa kifedha na upungufu wa muda mrefu wa wafanyikazi katika taasisi za afya ya akili.