Afghanistan: Dada yangu mdogo hatalazimishwa kuolewa na mpiganaji wa Taliban '

Iliyochapishwa

Mwanaume aliyetoroka Afghanistan kwenda kusoma katika Chuo kikuu cha Uingereza anasema Taliban wamekuwa wakiitishia familia yake.

Mwanaume huyo ameiambia BBC, ambayo hailitaji jina lake kwamba amepokea ujumbe unaosema kuwa dada yake - ambaye ana umri wa chini ya miaka 13 atapelekwa kuolewa na mpiganaji wa Taliban.

Anahofia kuwa sasa yake atakuwa mfungwa wa maisha iwapo atalazimishwa kuolewa.

Mwanaume huyo , ambaye anasoma chini ya mfumo wa udhamini wa masomo wa Chevening , aliokolewa kwa ndege hadi nchini Uingereza baada ya Tliban kuchukua mamlaka lakini hakuweza kuileta familia.

Alikuwa mmoja wa Waafghanistan 35 waliookolewa kutoka nchini Afghanistan na kuletwa Uingereza kulipiwa masomo chini ya mfumo wa Chevening - unaodhaminiwa na Wizara ya Mambo ya nje ya Uingereza na kuwawezesha wanafunzi kutoka maeneo mbali mbali duniani kusoma shahada ya uzamili nchini Uingereza.

Akizungumza na kipindi cha BBC Radio 4 , mwanafunzi huyo wa Chevening alisema kuwa Taliban walimwambia yeye na mama yake kwamba dada yake atapelekwa kuolewa katika kipindi cha mwezi mmoja.

"Wanasema mama yangu ataolewa na mmoja wa wafuasi wa kikundi hicho mwenye matatizo ya akili. Sio hukumu ya kifo, lakini kile wanachokifanya ni kumfunga maisha.

"Atakuwa kama mfungwa wa vita, hawezi hata kutamka baadhi ya maneno, anasoma shule. Lakini wanasema hapaswi kuwa shuleni, anapaswa kuolewa ."

Tarehe 21 Agosti , mwnaume huyo alipokea ujumbe wa barua pepe kutoka udhamini wa masomo wa Chevening uliomwambia kuwa yeye pamoja na watu wengine wanaomtegemea wanaweza kwenda nchini Uingereza.

Lakini anasema hali ya "vurugu" iliyokuwa kwenye uwanja wa ndege wa mji mkuu Kabul, ilimaanisha kuwa "angehatarisha" maisha yake kwa kuileta familia.

Kulikuwa na hali ya wasiwasi katika uwanja wa ndege wakati Marekani na washirika wake - ikiwa ni pamoja na Uingereza-walipokuwa wakigombania kuwaokoa raia wao na Waafghanistan wanaostahili kuokolewa kabla ya Marekani kuondoa vikosi vyake tarehe 31 Agosti.

Baadhi ya watu walianguka na kufa baada ya kujaribu kupanda ndege ya kijeshi ya Marekani ilipokuwa ikiondoka uwanjani, huku hali ya usalama ikiendelea kuimarishwa baada ya mlipuaji wa kujitoa muhanga kuwaua raia 170 na wanajeshi 13 wa Marekani nje ya umwanja wa ndege tarehe 26 Agosti. Tawi la IS-K lilisema ndilo lililofanya shambulio hilo.

Wengi wa wale waliouawa walikuwa na matumaini ya kupanda ndege za uokoaji na kuondoka mjini Kabul.

Serikali ya Uingereza inasema imekuwa ikiwasaidia wanafunzi wanaosoma chini ya mfumo wa Chevening kuondoka Afghanistan kwenda Uingereza, huku msemaji wake akiongeza kuwa: Tutaendelea kufanya kila tunaloweza kupata mapito salama na kutekeleza wajibu wetu kuwawezesha raia wa Uingereza na Waafghanistan kuondoka nje ya nchi hiyo ."

Mwanafunzi huyo wa Chevening anaamini kuwa Taliban wanamuadhibu kwa shuguli zake za ujasiliamali nchini humo.

"Nilipokea simu za Whatsapp zinazoniambia kuwa niliokolewa na jeshi la Uingereza kwasababu nilikuwa wakala wao. Wananiambia hawawezi kunidhuru mimi, lakini familia yangu italipa.

"Taliban wanadhani kuwa kama una uhusiano na jamii ya kimataifa basi unakula njama dhidi ya maadili ya utamaduni wa kiislamu ya nchi.

"Watafanya vyovyote vile kulipiza kisasi. Hawana utu. Wanazitisha familia za watu ambao wamekuwa wakijaribu tu kufanya mema kwa jamii yetu ."

Mwanaume huyo anasema "ana uhakika kwa 100%'' kuwa dada yake atapelekwa mwezi ujao na akaonya juu ya athari zitakazotokea iwapo hataweza kumleta mama, dada na kaka zake nchini Uingereza.

"Mama yangu atakuwa mfungwa kwa watu hawa wenye matatizo ya akili kwa maisha yake yote kama hili litatokea ."

Aliongeza kuwa ana "matumaini" kwamba anaweza kuileta familia yake nchini Uingereza, kama wanafunzi wengine wa Chevening walivyoweza kufanya, lakini bado hajapokea"jibu chanya" kutoka kwa serikali ya Uingereza.

Mbunge wa chama cha kijani cha Uingereza- (Green Party) Caroline Lucas, ambaye amekuwa akiwasiliana na baadhi ya wanafunzi wa Chevening sambao wana wasiwasi na familia zao zilizopo Afghanistan, alitoa wito kwa serikali kuchukua hatua ya dharura.

Alitoa wito kwa mawaziri kulegeza sheria za wizar ya mambo ya ndani ambazo anasema zinazosema ni mke au mume na mtu wenye chini ya miaka 18 pekee anayeweza kuja Uingereza chini ya mfumo wa hivi sasa mapazi mapya wa Afghanistan.

Bi Lucas ameiambia BBC Radio 4 : "Tunahitaji serikali iingilie kati, wanaendelea kutuambia tusubiri kufunguliwa kwa mfumo wa makazi mapya kwa raia wa Afghanistan.

Serikali bado inajenga mpango wake wa makazi mapya ya raia wake wa Waafghanistan . Serikali ya Uingereza imelenga kuwachukua wakimbizi 5,000 Waafghanistan katika mwaka wa kwanza na imelenga kuwachukua raia hadi 20,000 kwa muda mrefu.