Je ni kwanini Jeshi la Urusi linazidi kuongeza hifadhi yake ya nguvu kazi?

Wanajeshi

Chanzo cha picha, KIRILL KUKHMAR / TASS

Iliyochapishwa

Wizara ya ulinzi ya Urusi imetangaza kuwa akiba yake ya nguvukazi ya jeshi itaongezwa.

Hatahivyo wavuti ambao kwa kawaida hudai taarifa za aina hii na miito inayowataka raia wa nchi hiyo kujiunga na mchakato huo, haupo katika hifadhi ya taarifa ya Wizara yenyewe ya ulinzi.

Wanajeshi hao wa akiba watakaotoka miongoni mwa raia watatakiwa kusaini mkataba na wizara ya ulinzi, ili wapokee kiasi fulani cha fedha na kushiriki katika mazoezi ya kijeshi. Utaratibu huo umekuwa ukifanyiwa majaribio tangu mwaka 2016.

Taarifa kutoka wizara ya ulinzi inasema kwamba raia hao wa akiba pia watashiriki katika mazoezi ya kijeshi yatakayofanyika katika eneo la Kaliningrad.

Wizara hiyo haikusema jeshi linawahitaji raia hao wa akiba wangapi

Mradi usiojulikana

Haijulikani ni nani aliyebuni mfumo huu mpya katika wizara ya ulinzi ya Urusi na kwa uamuazi gani.

Katika wiki za hivi karibuni, taarifa za miito inayowataka watu kujitokeza kushiriki mafunzo chinini ya mradi unaoitwa BARS-2021 (Akiba ya nchi ya Boyevoy Armeyskiy - akiba ya jeshi la nchi ) zilionekana kwenye mitandao ya mamlaka nchini humo.

Lakini taarifa hizi mara hii zimekuja kwa utofauti mkubwa, kwa mtindo pamoja na maudhui yake.

Kwa mfano, Wilaya ya kaskazini mwa Moscow ilichapisha makala ya kina kwenye wavuti wake yenye "viwango vya juu zaidi vya mafunzo yanayoweza kutolewa popote mtu alipo " (ikimaanisha kuwa kikosi cha akiba ), na katika Veliky Novgorod maafisa wametengeneza video fupi kuhusu vijana wadogo waliokuja kwenye makao makuu ya jeshi kujiunga na kikosi cha akiba.

Baadhi wanasema wavuti huo ni wa Wizara ya ulinzi "ulitengwa kwa ajili ya mradi mpya wa BARS-2021 ", lakini huu sio wavuti rasmi wa wizara ; ukiwa katika eneo huru; wavuti huu umetengenezwa kwa usaidizi wa kifaa ambacho kiko wazi kwa mtu yeyote, kinachotumiwa katika utengenezaji wa tovuti za "Tilda".

Kipengele cha sheria za tovuti kina taarifa zaidi kuhusu nyaraka zinazohusiana na mwaka 2015 na miaka ya nyuma zaidi, kama vile sheria nambari 370 "Kuhusu kuongeza kikosi cha akiba cha jeshi la Urusi " iliyosainiwa na Vladimir Putin mwaka 2015. Wataalamu wa jeshi wanaiita sheria hiyo kiwango kidogo cha majaribio ambayo umuhimu wake hauwezi kutathminiwa katika nchi nzima.

Hakuna waraka mwingine ambao umechapishwa katika vyombo vya habari juu ya kuanzishwa kwa mradi wa BARS - taasisi ambayo itachukua nafasi au itakayoongezwa kwenye kikosi cha akiba kinachoweza kuitwa wakati wowote kushiriki katika harakati za ulinzi wa taifa.

Hakuna taarifa zozote kuhusu mradi huu mpya kwenye tovuti ya wizara ya ulinzi ya Urusi.

Hatahivyo, tovuti ya bars2021.tilda.ws unaeleza kuwa uhamasishaji wa raia kujiunga na kikoasi cha akiba unafanywa na "jopo la watu wakarimu " na wizara.

Wavuti huo umetengwa kwa ajili ya kubuni akiba mpya ya wanajeshi. Unatoa taarifa za kina juu ya masharti ya mkataba, malipo ya fedha na vigezo vya wanaotaka kujiunga na kikosi kipya cha akiba.

Kwenye kitengo cha "Mawasilianot" zimeorodheshwa nambari za simu za makamishna wa jeshi la Urusi . Tovuti hiyo haina taarifa zozote kuhusu miundo isiyohusiana na mamlaka za nchi.

BBC Idha ya Urusi ilituma ombi kwa wizara ya Ulinzi kutaka kujua ni nani anayehusika katika mradi huo na uhusiano wake na wizara ya ulinzi, bado inasubiri kupata jibu.

Je binadamu wa akiba wanaoweza kuzunguka ni akina nani?

Kulingana na tovuti ya bars2021.tilda.ws, "akiba ya binadamu wanaoweza kuzunguka'' ni akiba ya raia wenye uwezo wa kiwango cha juu cha kupatikana mara wanapohitajika na wenye utayari wa hali ya juu wa kupatikana ."

Raia wa akiba watahusika katika mazoezi ya kijeshi na uhamasishaji

Chanzo cha picha, LEV FEDOSEYEV / TASS

Maelezo ya picha, Raia wa akiba watahusika katika mazoezi ya kijeshi na uhamasishaji

Kwa maneno mengine, hao wanaojumuishwa katika akiba hiyo wataendelea kuishi maisha yao ya kiraia na watakuwa wakihamasishwa mara kwa mara.

Sheria mpya inatofautiana na ile ya enzi ya Usovieti, ambapo yeyote aliyehudumu katika jeshi alitakiwa kuwa amesomea katika idara za jeshi za vyuo vikuu na aliyehudumu kama mwanajeshi alikuwa anachukuliwa kama askari wa akiba.

Katika mfumo huu, kuondolewa katika usajili hufanyika baina ya umri wa miaka kati ya 35 na 70, kulingana na cheo ulichonacho.

Katika tukio la vita, raia wa akiba wanajumuishwa katika vikosi vilivyoundwa kulingana na hali ya amani iliyopo wakati huo.

Wazo la kubuni kikosi cha akiba cha nguvu kazi linasaidia kuhakikisha kwamba ujuzi wa awali hausahauliki na kwamba ujuzi wa sasa unapatikana kupitia mafunzo ya mara kwa mara.

Kwahiyo, faida mbali mbali na usaidizi wa kifedha unatolewa kwa wanaojiunga na kikosi cha akiba.

Mara tu baada ya kusaini mkataba, watapewa fedha, mishahara yao itaongezwa kutoka 10% hadi 50% katika kipindi cha miaka 20 cha hudumu yao.

Wavuti huo unaahidi kuwa ngongeza ya mshahara ya kati ya roble elfu 4 hadi elfu 9 kwa maafisa na roble 4 elfu 2 hadi elfu 6, kulingana na mahala huduma hiyo inapotolewa

Kwanini Urusi inahitaji raia wengi wa kujiunga na kikosi cha akiba?

Haijafahamika ni raia wangapi wa akiba ambao wizara ya ulinzi inapanga kuwavutia kujiunga na kikosi hicho.

Mapema mwezi Agosti , Konstantin Zapatotsky, mkuu wa shirika na idara ya uhamasishaji katika wilaya ya kijeshi ya kusini (CHB), alisema kuwa CHD ilipanga kuunda kikosi cha wapiganaji wa akiba 38,000 kufikia mwishoni wa mwezi wa Septemba .

Awali, kikosi cha nguvu kazi kilikuwa na jumla ya watu 400. Hii ndio idadi pekee iliyotajwa na afisa wa wizara ya ulinzi . Hatahivyo, wavuti wa bars2021.tilda.ws umeandika kuwa raia waliojisajili wamekwisha ajiriwa.

Mtaalamu wa masuala ya kijeshi nchini Urusi Alexander Golts, aliandika katika makala yake kuhusu tovuti ya Jamuhuri kwamba kunaweza kuwa na sababu mbili za ongezeko kubwa na la haraka la wanajeshi wa akiba -maandalizi kwa ajili ya vita vikuu au kipindi cha mpito cha kufanya mikataba ya jeshi:

"Katika mazingira mabaya zaidi ni kwamba wanabuni kikosi cha akiba kwa Warusi, kwa madhara yote, kuanzisha operesheni kubwa za kijeshi katika kipindi cha mwaka mmoja na nusu hadi miwili .", anasema Golts.

Mtaalamu mwingine wa masuala ya kijeshi nchini Urusi, Viktor Murakhovsky, alisema kuwa mpango wa kuongeza idadi ya wanajeshi wa akiba unaonyesha kwamba wizara ilikuwa inatafuta udhamini wa fedha. Kwa mujibu wake, jaribio la kubuni nguvu kazi ya akibam lililoanza mwaka 2015, limekwishapata uzoefu fulani.

Murakhovsky anasema jeshi la Urusi limetumia kanuni ya mfumo wa Marekani katika kubuni kikosi cha akiba kilichopewa mkataba.

"Nchini Marekani, pia, jeshi la akiba huundwa kwa misingi wa mkataba, pamoja na jeshi la kawaida, linahusika katika mizozo mikubwa na sheria za kikosi kipya kilichoundwa hubuniwa ."

Kulingana na mtaalamu huyu, mpango wa kikosi chanye mkataba haumaanishi kuvunjwa kwa uhamasishaji wa ujumla wa Urusi, kikosi cha akiba kitakuwa sehemu muhimu ya jeshi, aina moja ya kikosi cha jeshi la Urusi.

Murakhovsky anaamini kuwa kipindi cha mpito cha Urusi cha mfumo wa jeshi lenye mkataba kinaweza kusababusha matatizo kuvipeleka vikosi nyakati za mizozo ya kijeshi.

Anakadiria kuwa idadi ya kikosi cha akiba nchini Urusi ina watu 150,000.