Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Afghanistan: Adhabu kali kurejeshwa, afisa mwandamizi wa Taliban asema
Kiongozi mwandamizi wa kundi la Taliban amesema adhabu kali kama vile kunyongwa na kukatwa viungo zitaanza tena nchini Afghanistan. Mullah Nooruddin Turabi, ambaye kwa sasa ni mkuu wa Magereza, ameiambia AP News kukatwa viungo ilikuwa "muhimu kwa usalama".
Alisema adhabu hizi haziwezi kutolewa hadharani, kwani zilikuwa chini ya utawala uliopita wa Taliban miaka ya 1990. Lakini alitupilia mbali hasira za watu kuhusu utekelezaji wa adhabu hizo kwa umma huko awali: "Hakuna wa kutuambia sheria zetu ziweje."Tangu waingie madarakani Afghanistan Agosti 15 kundi Taliban wamekuwa wakiahidi aina kali ya utawala kuliko utawala uliopita.
Lakini kumekuwa na ripoti mbalimbali kuhusu uvunjifu wa haki za binadamu unaoendelea katika maeneo mbalimbali nchini humo. Alhamis hii, Shirika la kutetea haki za binadamu la Human Rights Watch limeionya kundi la Taliban huko Herat walikuwa "wakiwasaka wanawake wenye hadhi kubwa, wakiwanyima wanawake uhuru wa kutembea nje ya nyumba zao na kuweka kanuni za mavazi ya lazima"."
Mwezi Agosti Shirika lingine la kimataifa la Amnesty International lilisema wapiganaji wa Taliban walihusika na mauaji ya watu tisa kutoka jamii ya wachaceh ya Hazara. Katibu mkuu wa Amnesty, Agnès Callamard wakati huo alisema kwamba mauaji hayo ya "ukatili wa kinyama" yanakumbusha rekodi ya zamani ya Taliban, na kiashirio cha kutisha cha namna utawala wa Taliban unaweza kuleta".
Siku kadhaa kabla Taliban kushika hatamu mji wa Kabul, jaji wa kundi hilo huko Balkh, Haji Badruddin, aliiambuia BBC kwamba aliunga mkono vitendo vya kundi hilo na tafsiri yake ya sheria za kiislamu. "Kwenye sharia zetu, iko wazi, kwa wote wanaozini , awe mwanammme ama mwanamke, adhabu ni viboko 100 hadharani," alisema Badruddin. "Lkini kwa wote ambao yuko kwenye ndoa, watapaswa kupigwa mawe mpaka kufa... kwa wote ambao wameiba: iikithibitishwa, anapaswa kukatrwa mikono."
Turabi - ambaye amewekwa vikwazo na Umoja wa mataifa kwa vitendo vyake huko nyuma - alisema baraza la mawaziri la Taliban kwa sasa linajadili kama adhabu hizo ziwe hadharani ama la kwamba wataandaa sera rasmi".
Katika miaka ya 1990s, adhabu hasa za vifo zilikuwa zikifanyika hadharani kwenye uwanja wa michezo wa Kabul au kwenye viwanja vya wazi vya msikiti wa Eid Gah. Wakakti huo Turabi alikuwa waziri wa sheria. "Kila mmoja alitukosoa kwa adhabu za uwanjani, lakini hatukuwahi kusema chochote kuhusu sheria zao na adhabu," alisema katika mahojiano yake ya hivi karibuni.
Mapema wiki hii, Taliban waliomba kuzungumza katika mkutano mkuu wa Umoja wa Matifa ambao unafanyika jijini New York City. Waziri wa ,masuala ya kigeni wa Ujerumani Heiko Maas alisema kwamba ingawa ni muhimu kuwasiliana na Taliban, "lakini mkutano mkuu wa Umoja wa Mataifa sio sehemu sahihi kwa ajili ya hilo".