Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Fahamu mbinu za kisaikolojia zinazotumiwa na wapelelezi kugundua udanganyifu
Katika makala hii tunaangazia kuhusu mbinu za upelelezi zinazotumiwa kubaini udanganyifu(uongo) hususan inapokuja katika uhalifu. Na ili kufahamu hayo makala inaangazia jinsi kikosi cha afisa usalama wa kimataifa Thomas Ormerod anavyokabiliana na kazi hii ambayo inaonekana kuwa haiwezekani.
Katika viwanja vya ndege vya Ulaya , huwa wanawauliza wasafiri historia ya maisha yao na mipango yao ya safari. Omorod iliwatuma watu kadhaa kwenye kituo cha ukaguzi wa usalama , watu hawa walikuwa na historia za maisha yao ya nyuma ambazo hazikuwa halisi na mipango yao ya baadaye, na maafisa hao walitaka kubaini ni nani alikuwa muongo.
Ukweli ni kwamba ni mmoja tu kati ya maelfu ya watu waliyemuhoji aliyewadanganya. Kumgundua muongo unapaswa kuwa kama kutafuta sindano iliyodondoka ndani ya nyasi. Vipi kuwahusu?
Chaguo moja ni kufuatilia lugha yao ya mwili na mzunguko wa macho yao , sio? Hili kusema ukweli ni wazo baya inapokuja katika kumtambua mdanganyifu.
Utafiti unaoendelea unaonyesha kuwa hata maafisa wa polisi waliopewa mafunzo huwa wanajaribu kumuelewa muongo kupitia lugha yake ya mwili na muonekano wa uso wake, na wanasema mara nyingi kuelewa mafanikio ya njia hii huwa ni bahati.
Kulingana na utafiti uliofanywa kati ya watu 20,000 , ni 50 tu walioweza kuwatambua wakweli huku 80% wakiwa sahihi. Mara nyingi, ni vyema kutumia mbinu tofauti kupata majibu sahihi.
Siri yao ni ipi? Achana na viashiria vya awali vya uongo na utumie mbinu nyingine rahisi kuanzia mwanzo.
Katika miaka ya hivi karibuni, matokeo ya utafiti juu ya udanganyifu yamekuwa ya kukatisha tamaa. Kazi nyingi za awali za utafiti wa jambo hili uliangazia zaidi katika kubaini nia za muongo kupitia lugha ya mwili wake au uso wake, kicheko cha hofu, na upepesaji wa macho.
Mfano maarufu zaidi ni ule wa rais wa zamani wa Marekani Bill Clinton, ambaye aligusa pua lake wakati alipokanusha kuwa na mahusiano ya kimapenzi na Monica Lewinsky, jambo ambalo lilichukuliwa kama ishara ya wazi ya udanganyifu wakati huo.
Kwa mujibu wa Timothy Levine wa Chuo kikuu cha Alabama katika Birmingham, hii inaweza kuelezewa kwa ukweli kwamba udanganyifu unaweza kusababisha hisia thabiti- wasiwasi, majuto, na hata kuchangamkia changamoto —hii ni ngumu kuidhibiti.
Hata kama tunajihisi kama "tuna nyuso ngumu za kuficha yaliyomo moyoni ", ukweli ni kwamba bado nyuso zetu zinaweza kuwa na mizunguko fulani inayoitwa "viashiria vidogo vya kujieleza", ambavyo vinaweza kutusaliti.
Licha ya matokeo haya ambayo hayazuiliki, usalama wetu mara nyingi hutegemea dalili hizi .
Chukua kwa mfano ukaguzi wa wasafiri fulani wanaoupitia kabla ya kusafiri safari ndefu ya ndege kama mfano- Omorod iliombwa kutafuta suluhu ya usalama wao siku moja kabla ya michezo ya Olyimpiki 2012.
Alisema kwamba kwa hali ya kawaida, maafisa wa usalama hutumia "ndio/hapana" kama majibu ya maswali yanayolenga nia za wasafiri, na pia wamepata mafunzo maalumu ya kutizama "dalili zinazoshukiwa " ambazo zinaweza kufichua mienendo ya udanganyifu (kama vile mtu kuonyesha hali ya uonga).
"Hiyo haiondoi fursa ya kusikiliza, kutafakari, kuchunguza mabadiliko katika tabia ya mtu -haya ni mambo ya kimsingi ya kugundua uongo," alisema.
Alisema hatahivyo kuwa sheria zilizopo na kanuni zinaweza kusababisha ubaguzi kwa urahisi-kwa mfano, maafisa wa usalama wana uwezekano mkubwa wa kupata dalili wanazoshuku katika aina fulani ya makundi ya asili ya watu. " Mbinu ya sasa inazuwia kukamatwa kwa watu wenye mienendo ya udanganyifu," aliongeza.
Bila shaka, mbinu mpya inahitajika. Hatahivyo ukizingatia ufichuzi wa udanganyifu mbaya umekuwa ukipatikana kwa njia ya maabara , mbinu mpya inapaswa kuwa ipi?
Jibu la Omorod ni rahisi sana: Usiangalie tu vigezo vichache vya maelezo na tabia ya mtu, bali angalia zaidi ni nini watu wanasema, baina kwa akili ni wapi kuna "vitu muhimu unavyotaka ", kugundua udanganyifu uliojificha.
Misingi ya uhalisi
Omorod na mwenzake Coral Dando kutoka Chuo kikuu cha Wolverhampton wameelezea kwa kifupi msururu wa mazungumzo juu ya kanuni ambazo zinaweza kuboresha uwezekano wa kumtambua muongo :
- Uliza maswali ya wazi. Hii humfanya muongo kupanua maelezo yake hadi anapoanguka katika mtego wa udanganyifu
- Buni jambo la kushitukiza "kubaini utambuzi " wa muongo kwa mfano kwa muuliza baadhi ya maswali ambayo yanaweza kumkanganya ,au kwa kumtaka akueleze jinsi tukio lilivyotendeka- jambo litakaloleta ugumu kwa mtu kuzingatia udanganyifu hadi mwisho
- Fuatilia kwa karibu mambo madogo madogo yanayoweza kukusaidia kuthibitisha taarifa unayopewa.
- Tazama na ufuatilie mabadiliko katika viwango vya kujiamini wakati wa mahojiano. Tazama kwa uangalifu mienendo ya muongo inapobadilika: Muongo anaweza kuongea maneno mengi zaidi anapohisi mambo yanamuendea sawa, lakini kujiamini kwake hupungua anapohisi ameshinikizwa, anaweza kunyamaza
Wakala waliofundishwa kuhusu mbinu za kuhoji za wapelelezi Omorod na Dandal wana uwezekano mara ishiri wa kung'amua wasafiri bandia kuliko wale wanaotumia dalili za kushuku, na uwezekano wao wa kuwabaini wadanganyifu ni wa 70%.
Mbinu ya ushawishi
Uzoefu binafsi wa Levine pia ni wa kuaminika. Sawa na Omorod, pia anaamini kuwa kuhoji maswali kwa kutumia ujanja kwa lengo la kufichua mashimo katika hadithi ya muongo ni bora zaidi kuliko kujaribu kupata dishara za kawaida katika lugha ya mwili ya mtu anayechunguzwa.
"Watu huwa wanataka kufikiri kuwa ni wakweli, jmbo linalowafanya kuonyesha ushirikiano ," Levine anasema. "Hata watu ambao ni waongo ni vigumu sna kujifanya kuwa hawana ushirikiano, kwahiyo mara nyingi, unaweza kuona ni nani anajifanya . "
Bila shaka baadhi ya wataalamu wa upelelezi wanaweza kuwa wametumia mbinu hizi-lakini kuokana na uzoefu wa muda mrefu wa matumizi ya lugha ya mwili katika kubaini udanganyifu. Ni muhimu kusisitiza kuwa njia ya ushawishi ni bora zaidi , kulikio kuangalia lugha mwili ya mshukiwa wa udanganyifu.