Daktari wa Misri ahukumiwa kifungo cha jela kwa kutumia sumu 'kuyafukuza majini' kwa mkewe

Iliyochapishwa

Waswahili husema, kuishi kwingi kuona mengi…basi wakati ukitafakari hayo, Daktari mmoja nchini Uingereza, raia wa Misri amepatikana na hatia baada ya kumdunga mke wake sumu, alipokuwa katika harakati za 'kuyafukuza majini' yaliyokuwa yakimsumbua.

Mahakama ya Uingereza imeamua kumfunga kifungo cha miaka 14 kwa kumdunga sindano ya sumu aina ya Nicortin kwa lazina kama njia ya kumtoa mashetani nyumbani kwao katika eno la Grimsby .

Mahakama ya Sheffield ilisikiliza ushahidi kuwa Metwally, mwenye umri wa miaka 34, alimshutumu mke wake kwa kudhibitiwa na pepo wabaya.

Mahakama ilimpata na hatia ya makosa manane Bw Metwally ikiwa ni pamoja na kudunga sindano yenye madhara pamoja na ulaghai.

Pia alipatikana na hatia ya kutazama picha za utupu , baada ya kupatikana na kamera za siri alizoziweka katika chumba cha mwanamke mmoja , alizoziweka ndani ya kliniki yake ya kibinafsi.

Kwa kipindi cha wiki nane, jopo la mahakama lilisikia ushahidi wa madai ambapo alisema ilisemekana aliamini kwamba kulikuwa na kiumbe au ''majini'' ndani ya mwili wa mke wake na kwamba alikuwa akisoma aya kutoka ndani ya Qur'an na kumwaga maji ya mafuta kwenye mwili wa mpenzi wake Wilson.

Waraka wa mashitaka pia ulitaja kwamba mwanaume huyo alikuwa akishiriki katika aina 250 za matambiko pamoja na mpenzi wake na alirekodi makumi kadhaa ya video za matibabu hayo aliyoyaanza na mke wake tangu mwaka 2016.

Video 200 za tiba zilizorekodiwa, daktarin Metwally alisikika akimdunga mke wake kimiminika cha sumu ya Narcotin , huku akiwa amelala mbele yake bila fahamu kitandani.

Metwally alikamatwa baada ya Wilson tarehe 4 Julai, 2019 alipokuwa mahututi na kulazimika kulazwa jioni baada ya kupoteza fahamu jioni.

Wakati wa uchunguzi kuhusiana na kesi hiyo, polisi ilibaini kiwango kikubwa cha sumu za narcotics, zikiwemo zile za aina ya ketamine, propofol na fentanyl.

Polisi walibaini pia video pia zilizotengenezwa na kuhaririwa, zinazoonyesha muathiriwa akitazamwa mtupu, hatia ambayo ilimpata Metwally.

Jaji Jeremy Richardson alipinga madai yaliyotolewa na Husam Metwally, ambaye ni daktari bingwa wa upasuaji na kuzuwia maumivu katika kituo cha taifa cha Uingereza cha huduma za afya, kwamba alikuwa akitoa sumu kutoka kwenye mwili wa mke wake, akisema kuwa alikuwa akifanya matambiko akisema ni ''uongo kabisa ".Jaji Muingereza pia alisisitiza kwamba hii ilikuwa ni ibada "haihusiani kabisa na taratibu za Kiislamu katika matukio kama hayo."

Richardson alielezea kile ambacho Hossam Metwally alikitaja kama "itikadi kali", alisisitiza kwamba "ibada hizo alizozifanya na Wilson zilikuwa ni taratibu za kidini ."

Jaji alisema kwamba Metwally huenda alikuwa anafikiria kuwa alikuwa akimsaidia , "kwa njia iliyokatazwa", na kwamba alifanya hivyo akitumia "mchakato wa tiba usio na ufanisi" na "kumdunga na sumu kali za narcotic , na kuhatarisha Maisha yake ."

Aliongeza kwamba Metwally, "ambaye hata hakuonyesha kujutia kitendo alichokifanya alipokuwa akijitetea ," alitumia udhaifu wa aliyekuwa mpenzi wake, "kumuweka hatarini kimwili."

Akizungumza na Richardson jaji alisema: "Wewe ni fedheha kwa kazi yako, na hautakuwa daktari tena ."

Aliongeza kuwa: "Umemzuwia kupata matibabu ya hospitali kwa ajili ya faida zako za kibinafsi. Wewe sio daktari mzuri… nusura umuue mke unayedai unampenda."

"Hii ni kesi ya ajabu ambayo haijawahi kusikilizwa na polisi wa Humberside,"

Alisema Ispekta mkuu wa polisi Police Rodrigue Truk.