WhatsApp: Jinsi ya kukwepa makundi ya Whatsapp

WhatsApp
Iliyochapishwa

Mtandao wa Whatsapp umekuwa ukisaidia kuimarisha umoja na urafiki baina ya watumiaji na hasa wanafamilia na marafiki ambao wanaishi mbali kwa kipindi kirefu.

Huwaruhusu mashangazi na wajomba kwa mfano, kuhakikisha kila mmoja ndani ya familia anachangia mchango wa harusi, kilio, sherehe za kufungua nyumba mpya au tukio lolote jingine ambalo linawafurahisha wao.

Kwa upande mwingine Mtandao wa WhatsApp umekuwa kiunganishi cha kuwaunganisha watu kwa ajili ya kuchangisha pesa, hususan za kuandaa harusi miongoni mwa watu wa familia mojo, marafiki na hata kuandaa sherehe mbali mbali, kuwaunganisha watu wanaofanya kazi moja au biashara kwa lengo kufanikisha malengo yao ya kikazi.

Kero ya matumizi ya WhatsApp

Hatahivyo kwa baadhi mtandao huu umekuwa kero hususani pale watumiaji wake wanapounda makundi yanayolenga maslahi yao ya binafsi na kuwaingiza watu kwenye makundi hayo bila kuwafahamisha lengo la kikundi.

Kwa baadhi, jumbe, picha , vibonzo vinavyoonesha hisia za msomaji(meme) vinavyoendelea kumwagika katika makundi ya kumbi hizi vimekuwa kero kubwa.

Wakati mwingine mtumiaji wa Whatsapp huingizwa kwenye kikundi ambacho hata hamfahamu mtu mwingine au , hata kama wajumbe wengine huwafahamu

Lakini je unawezaje kuondoka katika kundi la Whatsapp bila kugunduliwa na watu wengine?

Hili haliwezekani. Kusema kweli hadi kufikia leo hii hakuna vyovyote unavyowerza kukweka ukumbi huu pasipo watu wengine kujua kuwa umetoka.

Ukitumia njia ya kuondoka kwenye kikundi (leave group) programu hii itatuma ujumbe kwa wajumbe wote wa kikundi cha Whatsapp ukionesha jina lako kwamba umeondoka ukumbini. Na kama ni kikundi cha familia basi baadhi watataka uelezee kwanini umeondoka na baadhi wakijaribu kubashiri ni kwanini umeondoka ukumbini.

Wengi wangependelea kuondoka kwenye makundi ya Whatsapp bila kutambuliwa na mtu yeyote, lakini kwa bahati mbaya WhatsApp haikutoa chaguo hilo kwa wateja wake.

Je unaweza kujiondoa kwenye kikundi cha familia?

Kusema ukweli kuna watu wengi ambao wangependa kwa sababu moja au nyingine kujiondoa kwenye makundi haya ya Whatsapp

Lakini inapokuja katika suala la familia, suala hili linakuwa gumu mno.

Kwa mfano Murielle Alapini, ambaye ni mkufunzi wa usafi kwa njia ya digitali, anaamini kuwa kikundi cha Whatsapp hakipaswi kuwa tatizo kwa mtumiaji. Una uhuru wa kuondoka ukumbini. Kama huhisi vyema kuwa katika kikundi, unaondoka, ''anadai.

Je kama ni rahisi ni kwanini watu wengi sana wanasita kujiondoa kwenye kundi?

Jibu ni rahisi, anasema mkazi huyu wa Kinshasa DRC : ''Wakati nilipoingizwa kwenye kikundi cha familia, sikuwa nimeambiwa mapema. Nilijipata nipo ndani tu siku moja. Lakini sikuondoka. Nimo. Lakini bila shaka siandiki chochote. Sijibu ujumbe wowote, lakini siwezi kuondoka kwasababu familia ni kitu kitakatifu. ''

Na kama unataka kujiondoa ukumbini, unaweza kufanya nini?

WhatsApp

Mbinu unazoweza kutumia kukwepa Whatsapp

Tusikate tamaa. Kwasababu suluhu mbadala zipo

Funga(Mute) au zima( turn off) taarifa za kikundi.

Mbinu rahisi ya kuondoka katika kikundi cha WhatsApp ni kuacha kuamua kufunga au kuzima taarifa za kikundi zinazokuarifu kuwa ujumbe umetumwa.

Kwa namna hii hautakuwa ukifahamishwa kuhusu mazungumzo yanayoendelea ndani ya kikundi cha WhatsApp.

Unaweza kuwa unafuatilia mazungumzo pale unapohisi kufanya hivyo.

Hivi ndivyo unavyozima taarifa za kikundi: nenda wenye - Mipangilio (Settings) kwenye kikundi chako cha WhatsApp. Bofya 'Notifications'. Hapo utaona chaguo la Taarifa za Kikundi 'Group Notifications' chini utaona kipengele kinachoonesha 'Alerts'. Bofya uzime kikundi cha WhatsApp.

Weka kikundi cha Whatsapp katika (kumbukumbu) au Archive

Chaguo la kukiweka kikundi kwenye kitengo cha kumbukumbu na kuzuia taarifa za kikundi linawezekana. Hivi ndivyo unavyotakiwa kufanya : unafungua WhatsApp, nenda kwa jina la kikundi, bofya kwa muda mrefu na usogeze upande wa kushoto, ambapo utaweza kuona chaguo la kumbukumbu '' Archive ''. Unabonyeza tu na hilo linafanyika.

Subiri katikati ya usiku wa tarehe 31 Disemba.

Kulingana na Mounass, ambaye hakupenda jina lake litajwe, kitu bora zaidi ni kusubiri hadi tarehe Disemba 31 wakati kikundi cha Whatsapp kinapokuwa na ujumbe mwingi, video na vibonzo vya kila aina.

Hapo unaweza kutoweka kwa urahisi na kufanikiwa kujiondoa ukumbini huku ukiomba sana ujumbe maarufu unaoonesha (kwa jina lako) umeondoka( left) kwenye kikundi " hautaonekana miongoni mwa mamia ya ujumbe wa kutakiana heri ya mwaka mpya .

Pia una chaguo la kuanzisha mjadala katika kikundi , utakaomkera kila mtu hadi uondolewe nje ya ukumbi wa Whatsapp.

Mbinu hii ilipendekezwa na mtumiaji wa Whatsapp kwa jina Raissa. Na inaonekana ilifaa sana familia hii ya Benin.

"Kuna mmoja wa madada zetu ambaye alitoa maoni yasiyofaa kumhusu dada yetu mwingine. Malumbano yalianza, wakaanza kuitana majina. Hatimaye kikundi kilivunjwa mara moja. Familia nyingine mmoja wao alianzisha kikundi. Lakini hakuna hata mmoja aliyeandika chochote ndani yake " alisema Bi Claudine mmoja wa wajumbe wa kikundi hicho.

Whatsapp ina uwepo kiasi gani barani Afrika ?

Mtandao huo wa ujumbe ulianzishwa na Facebook mwaka 2014 na kwa sasa una watumiaji bilioni mbili kote duniani.

Ripoti ya taasisi ya The Quartz Africa ya mwaka 2018 tayari ilionesha kuwa usajili wa watu katika mtandao huo ulikuwa ukiongezeka kwa kazi barani Afrika.

Kenya inaongoza katika orodha ya watumiaji wa mtandao wa WhatsApp kwa usajili wa (97%), huku Afrika Kusini wakisajili kwa (96%) na Nigeria (95%) zikichukua nafasi ya pili na ya tatu kulingana na ripoti ya GlobalWebIndex, ya mwaka 2020.