Eneo hatari la Afrika Kusini: Kuishi katika jengo 'lililotekwa nyara'

Chanzo cha picha, BBC/SHIRAAZ MOHAMED
Jiji la ndani la Johannesburg nchini Afrika Kusini ambalo ni hatari kwa watu wa nje, lina viwango vya juu vya uhalifu, utumiaji wa dawa za kulevya na ukahaba.
Mpiga picha Shiraaz Mohamed alipata kuaminiwa na watu wengine ambao wanaishi eneo hilo na kujua zaidi juu ya nyumba ambayo ni moja ya maeneo maarufu na yenyewe ni kuu kuu iliyotelekezwa.

Chanzo cha picha, BBC/SHIRAAZ MOHAMED
Ni zaidi ya miaka 17 tangu mamlaka ilipotangaza jengo la San Jose huko Hillbrow kuwa halifai kwa makazi ya binadamu.
Leo hii, jengo hilo la muundo wa ghorofa nyingi - linaonekana vifaa vyake vyote vya ndani vilivyotumika wakati wa ujenzi kama vile fremu za milango na madirisha.
Vote hivyo vilibadilishwa pesa taslimu katika yadi ya vifaa chakavu muda mrefu uliopita.

Chanzo cha picha, BBC/SHIRAAZ MOHAMED
Wakazi ambao wamehamia kwenye jengo hilo wameweka mablanketi na shuka za kitambaa kufunika mashimo makubwa ambayo awali yalikuwa ni madirisha ili kufanya eneo kuwa na joto.
Joto hupungua wakati wa msimu wa baridi, na kufanya maisha kuwa magumu sana huko San Jose.

Chanzo cha picha, BBC/SHIRAAZ MOHAMED
Wakati wa baridi kali, mchana, harufu ya kinyesi ni kali sana katika shoroba zenye giza za San Jose, ambazo wakaazi wake ni mchanganyiko wa Waafrika Kusini kutoka vitongoji jirani na maeneo ya vijijini, pamoja na wahamiaji kutoka kote Afrika.
Idadi ya watu kwenye jengo hilo imeongezeka mara mbili hadi karibu 200 - pamoja na wanawake na watoto - kwasababu ya amri ya kutotoka nje inayotekelezwa ili kuzuia kuenea kwa ugonjwa wa virusi vya corona na matatizo yanayotokana na janga hilo.

Chanzo cha picha, BBC/SHIRAAZ MOHAMED
Wale ambao walikuwa wakiishi hapa kabla, walishinda kesi mahakamani na kuamuliwa wahamishwe kwengineko katika makazi yaliyotolewa na mamlaka ya mji mnamo mwaka 2008. Kufukuzwa kutoka San Jose na majengo mengine yaliyopigwa marufuku kuishi binadamu kulikusudiwa kuinua eneo la Hillbrow na maeneo ya karibu kama Berea.
Lakini hii imekuwa kama ndoto ambayo bado haijatokea na pia jengo lenyewe bado halijabomolewa.

Chanzo cha picha, BBC/SHIRAAZ MOHAMED
Wakati maskwota wanaingia, majengo yaliyotelekezwa husemekana kuwa "yametekwa nyara".
Katika visa vingine "watekaji nyara" yaani magenge yanayowatoza wakaazi - lakini hiyo ni hali mbaya inayoshuhudiwa huko San Jose kwamba watu wanaokuja hapa hawalipi kodi kwa mtu yeyote.
Sehemu ya chini, eneo la lifti ambalo halitumika na maeneo ya karibu yamejazwa taka taka na maji taka.
Hakuna umeme, maji ya bomba wala vyoo.
Wakazi hujisaidia katika nafasi zenye giza ndani ya jengo na wakati mwingine kwenye njia za watembea kwa miguu.

Chanzo cha picha, BBC/SHIRAAZ MOHAMED
"Msimu wa baridi hufanya mambo kuwa magumu zaidi kwa wakaazi," anasema Sabelo Mapempeni mwenye umri wa miaka 38 (pichani juu).
Amekuwa akiishi katika jengo hilo kwa miaka minne iliyopita na yeye huwa anawafuatilia wakazi wenzake.
"Tunaishi mbawula," Bwana Mapempeni anasema, akitumia neno la Kizulu la ngoma za chuma zilizotumiwa kwa moto.
"Asubuhi hadi usiku moto unawaka."
Ingawa ilikusudiwa kutoa faraja, mbawula huleta hatari za kiafya kutokana na moshi wa kuni, ngozi, plastiki na chochote kingine kinachoweza kutakaswa hutumiwa kama mafuta.

Chanzo cha picha, BBC/SHIRAAZ MOHAMED
"Ni jambo la kutisha sana kuishi hapa. Watu wanaumwa na lazima wapelekwe hospitalini," anasema Bw. Mapempeni, ambaye ametumia maisha yake mengi gerezani au mitaani.
Watu wawili walifariki kutokana na baridi mnamo mwezi Julai, wakati msimu wa baridi ulipokuwa kilele chake, anasema.
"Unahisi kama moyo wako umechukuliwa na simba," Bwana Mapempeni anasema juu ya kupatikana kwa miili yao.
"Pia walikuwa na ndoto za maisha bora lakini hayako tena." Walipatikana kama mawe, wanadamu ambao waligeuka kuwa jiwe.
Hawakuwa na zulia licha ya godoro la kulala."

Chanzo cha picha, BBC/SHIRAAZ MOHAMED
Ndani ya moja ya vyumba, Derrick Brown (hapo juu), anajaribu kuwasha moto kujipikia kahawa na rafiki yake.
Moto hutumika kama jiko lake na pia njia ya kuhakikisha kuna joto.
Bwana Brown ameachiliwa hivi karibuni kutoka gerezani kwa udanganyifu wa kitambulisho na hana pa kwenda.

Chanzo cha picha, BBC/SHIRAAZ MOHAMED
Ni vita vigumu kupigania maisha ya wakaazi ambao wengine wao huamka asubuhi kutafuta chakula kwenye mapipa.
Wengine huenda kugonga milango ya watu majirani wakiuliza chakula.

Chanzo cha picha, BBC/SHIRAAZ MOHAMED
Makanisa, mashirika ya kidini na ya kutoa misaada huchukua jukumu muhimu katika kuziendeleza familia hizo.
Hapa kuna foleni ya mkate, chakula cha kwenye kopo na blanketi kutoka Jumuiya ya Waislamu ya Afrika Kusini.

Chanzo cha picha, BBC/SHIRAAZ MOHAMED
Bwana Brown, ambaye amekuwa mara kwa mara anagungwa gerezani na kuachiwa huru katika maisha yake yote, anasema anapambana na uraibu wa dawa za kulevya - kama wengi wale wanaoishi San Jose.
Mkazi anayeonyeshwa hapo juu anavuta sigara aina ya Mandrax, dawa ya kupuliza iliyochanganywa na bangi.
Inavutwa kupitia shingo ya chupa iliyovunjika.

Chanzo cha picha, BBC/SHIRAAZ MOHAMED
Lakini sio kila kitu kabisa ni giza na huzuni.
Moosa Sikhele (mwenye miaka 23) hapo juu anasema amepata eneo patakatifu huko San Jose baada ya kuishi mitaani.
Hangeweza tena kuvumilia baridi na rafiki akamchukua. Mtu mpya au mtu asiyejulikana kwa wakaazi kuna uwezekano mkubwa akaibiwa isipokuwa tu awe na mawasiliano katika jengo hilo.

Chanzo cha picha, BBC/SHIRAAZ MOHAMED
Wakazi wanafanya kila wawezalo kuweka vyumba vyao nadhifu - na kuzuia jengo kuzorota zaidi.
Hasa hawataki wahalifu wahamie kwenye jengo hilo kwani hiyo inaweza kufanya maisha kuwa magumu zaidi.
Bwana Sikhele amekuwa akiishi katika jengo hilo lililotelekezwa kwa miezi michache iliyopita - na anasema anafurahi kuwa San Jose.
Anajaribu kupata pesa za kujikimu kimaisha kwa kuuza saa na mikanda ya bei rahisi ya Wachina lakini pia hutegemea sana watu kupata nguo na chakula.
Picha zote zina haki miliki












