Tetesi za soka Ulaya Alhamisi tarehe 2.09.2021: Niguez,Haaland, Woodward, Ronaldo, Olmo

Chanzo cha picha, Getty Images
Kiungo wa kati wa Uhispania Saul Niguez, 26, anatarajiwa kuvaa jezi namba 17 huko Chelsea baada ya kujiunga kwa mkopo kutoka Atletico Madrid siku ya mwisho ya uhamisho. (Star)

Chanzo cha picha, Reuters
Mshambuliaji wa Borussia Dortmund na Norway Erling Braut Haaland, 21, atakuwa mlengwa mkubwa wa Manchester United msimu ujao licha ya kuwasili kwa mshambuliaji wa Ureno Cristiano Ronaldo mwenye umri wa miaka 36 kutoka Juventus. . (ESPN)

Chanzo cha picha, Getty Images
Makamu mwenyekiti anayemaliza muda wake wa Manchester United Ed Woodward alikuwa na jukumu muhimu katika kuwezesha kupatikana kwa Ronaldo. (Manchester Evening News)

Chanzo cha picha, Getty Images
Barcelona itajaribu kumsajili tena kiungo wa kati wa Uhispania Dani Olmo, 23, mnamo mwezi Januari baada ya kushindwa kufanikiwa siku ya mwisho ya uhamisho kwa kitita cha pauni milioni 50 ambayo ilikataliwa na RB Leipzig. (Mail)

Chanzo cha picha, Rex Features
Leicester, Southampton na Nottingham Forest zote zilitoa ofa ya kuchelewa kwa beki wa kulia wa Middlesbrough, Muingereza, 21, Djed Spence. (Northern Echo)
Kocha wa Tottenham, Nuno Espirito Santo alimhakikishia Emerson Royal, mwenye umri wa miaka 22, kwamba atakuwa na jukumu muhimu katika timu hiyo, kabla ya mlinzi wa Brazil kukubali kuondoka Barcelona. (Marca)

Chanzo cha picha, Getty Images
Manchester United, Liverpool na Arsenal ziko tayari kupigania kumsaka kiungo wa kati wa Brighton na Mali, 25, Yves Bissouma mnamo mwezi Januari. (Mirror)
Mlinzi wa Chelsea raia wa Ufaransa Malang Sarr, 22, ameachwa kwenye njia panda baada ya mpango wake wa kuhamia upande wa Bundesliga timu ya Greuther Furth kwa mkopo kushindwa kufanikiwa siku ya mwisho ya uhamisho. (Mail)














