Je kuongeza ukubwa wa midomo ni ishara ya urembo?

Iliyochapishwa

Wanawake wa Kisomali wamekuwa wakitumia utaratibu wa kuongezea ukubwa wamidomo ili kuimarisha urembo wao.

Baadhi ya watu wanafikiria utaratibu wa kuongeza ukubwa wa midomo ni sehemu ya urembo huku wengine wakihoji matokeo ya utaratibu huo ''sura mbaya''.

Upasuaji bandia wa mifupa katika juhudi za kutafuta urembo ni utaratibu mpya ambao umewavutia wanawake wa KIsomali.

Utaratibu wa kuongeza ukubwa wa midomo umepata umaarufu duniani katika siku za hivi karibuni, ripti zikiashiria kuwa vijana wadogo wanapendelea sana mtindo huo wa urembo.

Watu mashuhuri wanaotumia mitandao ya kijamii ndio wanaathiriwa zaidi na vijana hawa, ambao ni mfano wao wa kuigwa.

Mmoja wa wasichana waliofanyiwa utaratibu huo, Filsan aliambia vyombo vya habari kwamba, "Kwa muda mrefu nimekuwa nikitamani kuongeza ukubwa wa midomo yangu. Leo nina furaha hatimaye nimefanikiwa kufanya hivyo. Najihisi mrembo zaidi kuliko nilivyokuwa .Ni utaratibu ambao unaimarisha muonekano wako kama inavyooneshwa kwenye picha zinazotumiwa kunadi utaratibu wenyewe. "Mimi ni mrembo," alisema.

Kuna hatari gani?

Utaratibu huu unatumika katika mataifa mengi sawa na Uingereza, lakini kumekuwa na miito ya kubuniwa kwa sheria ya kudhibiti utaratibu wa kuongeza midomo na jinsi utaratibu huo unavyofanywa.

Baadhi ya watu wanalalamikia hatari inayotokana na utaratibu huo wa kuongeza urembo.

"Ilifikia mahali midomo yangu ulikuwa kubwa katika hali ambayo haikuwa ya kawaida. Ilikuwa mbaya sana nilihisi imeanza kupitana ," mwanamitindo Lora Mua,32 aliiambi BBC.

Knappier, pia anafurahi hatimaye ameweza kutoka nje baada ya kusalia ndani kwa muda kutokana na madhara yaliyotokana na utaratibu huo.

"Badala ya kupata urembo aliokuwa akitafuta, amekuwa na sura mbaya,"alisema. skiku zijazo ni vyema kutafuta ushauri kwa wale wanaofanya utaratibu huo.

Je kuna sheria inayodhibiti utaratibu huu?

Vidonge vya ngozi ni sindano zinazotumiwa kujaza mikunjo na nyufa kwenye ngozi, ingawa hutumiwa pia kuongeza ukubwa wa midomo na mashavu

Sheria ya sasa ya nchini Somaliana mataifa mengine duniani zinasema unahitaji uwe na mafunzo ya matibabu ili kutekeleza utaratibu, ijapokuwa mtu yeyote anaweza kuagiza kifaa hiki mtandaoni na kujidunga mwenyewe sindano.

Lennes, kutoka Leicester, anasema alihisi 'uchungu sana'. Anawashauri wasichana kutoingilia urembo wa aina hiyo na ikiwa wanataka kufanya hivyo basi waende kwa wataalamu walio na ujuzi.

Inagharimu pesa ngapi kuongeza ukubwa wa midomo?

Inategemeao unafanyia katika mji gani, kiwango na sindano- kuongeza midomo kunaweza kukugharimu kati ya ya dola 500hadi dola 1,000.

Ikiwa unaishi katika miji mikubwa kama New York au Los Angeles, unaweza kulipa hadi dola 2,000. Ijapokuwa bei hiyo huenda ikaonekana kuwa ghali mno.

Inachukuwa muda gani kusalia na urembo huu?

Muda unategemea miaka yako na kiwango unachotaka kuongezea midomo yako lakini kwa kawaida urembo wa aina hii hudumu kw kati ya miezi sita hadi miaka mitatu kabla ya kurejelea tena mfumo wa tiba.