Afghanistan: Ripoti mbali mbali zanaelezea kuhusu kutokea kwa mlipuko mkubwa karibu na uwanja wa ndege wa Kabul

Chanzo cha picha, EPA
Kumekuwa na taarifa nyingi kuhusu mlipuko uliotokea karibu na uwanja wa ndege wa kimataifa wa Kabul nchini Afghanistan. Hii ni baada ya rais wa Marekani Joe Biden kuonya kuwa shambulio lingine huenda likatokea uwanja wa ndege wa Kabul, Rais Joe Biden ameonya akisema makamanda wamemwambia kuwa linaweza kutokea Jumapili.
Baadhi ya picha zilizotumwa kwenye mitandao ya kijamii zinaonesha moshi mweusi ukipaa juu ya majengo.
Mkala hii imebeba madhui yaliyotoka kwenye mitandao ya kijamii. Tunaomba ruhusa yako kabla kitu chochote hakija pakiwa, sababu wanaweza wakawa wanatumia Cookies na tekinolojia nyingine. Unaweza ukasoma sera sera ya kutumia cookies katika mitandao ya kijamii kabla ya kukubali. Kutazama maudhui haya chagua accept and continue
Mwisho wa X ujumbe
Maafisa wa wizara ya afya amethibitisha kuwa mlipuko ulitokea katika eneo hilo, wakisema kuwa umesababishwa na roketi lililopita karibu na uwanja wa ndege.
Uwanja wa ndege haukupigwa moja kwa moja, chanjo cha taarifa hii kimesema.
haijafahamika iwapo kulikuwa na majeruhi yeyote kufuatia shambulio hilo.
BBC inaendelea kutafuta taarifa zaidi kuhusu tukio hili.
Awali wizara ya mambo ya nje ya Marekani ilitoa wito kwa raia wote wa Marekani kuondoka kwenye eneo hilo kwasababu "tisho la kipekee la kuaminika ".
Marekani inaendelea na shuguli ya uokoaji, lakini vikosi vya mwisho vya Uingereza , wanadiplomasia na maafisa kwa sasa wameondoka Kabul.
Siku ya Alhamisi mlipuko wa bomu la kujitolea muhanga karibu na uwanja wa ndege uslisababisha vifo vya watu 170.
Tawi la kieneo la Islamic State - katika jimbo la Khorasan (IS-K) -lilidai kuhusika na shambulio hilo.
Katika kujibu shambulio hilo , Marekani ilifanya shambulio la droni mashariki mwa Afghanistan siku ya Ijumaa jioni, ikisema kuwa imewauwa wajumbe wa "cheo cha juu " wa IS-K.
Wawili hao wanaelezewa kama wapangaji na wawezeshaji. Haijafahamika wazi iwapo walikuwa wanahusika katika mpango wa kushambulia uwanja wa ndege wa Kabul.
"Shambulio hili halikuwa la mwisho. Tutaendelea kumuwinda yeyote aliyehusika katika shambulio lile baya na kuwafanya walipie ," Bw Biden alisema katika taarifa iliyotolewa siku ya Jumamosi.

Chanzo cha picha, Reuters
IS-K ni kikundi chenye itikadi kali na cha ghasia zaidi kuliko makundi yote ya Jihadi ya Wanamgambo wa Kiislam yaliyoko nchini Afghanistan na kinatofauti nyingi na Taliban , ambao kwa sasa wanadhibiti maeneo mengi ya nchi. Linawashutumu Taliban kwa kuacha uwanja wa mapigano na badala yake kufanya mazungumzo ya amani na Wamarekani.
Taliban ililaumu shambulio la ndege la Marekani , ikisema kuwa Wamarekani wangepaswa kwanza kushauriana nao kwanza, msemaji wao aliliambia Shirika la habari la Reuters.
Siku mbili za operesheni ya uokoaji wa Marekani huenda zikawa za hatari zaidi kuwahi kushuhudiwa tangu ilipoanza, Maafisa wa Ikulu ya White House wanasema.
Wanajeshi wa Marekani walianza kuondoka kwao kwenye uwanja wa ndege -idadi yao kwa sasa ni chini ya 4,000, kati ya 5,800 waliokuwa huko wiki moja iliyopita.
Afisa mmoja wa usalama kutoka nchi ya magharibi aliliambia Shirika la habari la Reuters kwamba vikosi vya Marekani viko katika awamu ya mwisho , ingawa muda wa kumaliza shughuli hiyo bado haujaamriwa.
Unaweza pia kusoma:
Ni raia 1,000 tu waliobakia kuokolewa kwa dege, alisema afisa huyo.
Afisa wa Taliban aliliambia shirika la Reuters kwamba wataalamu wao wa kiufundi na wahandisi wako tayari kuchukua uwanja wa ndege wa Kabul wakati watakapopewa "idhini ya mwisho kutoka kwa Wamarekani ''.
Taliban wameweka vizuizi zaidi vya barabarani kata maeneo yanayozingira uwanja wa ndege na hawawaruhusu wengi wa Waafghanistan kupita, liliongeza shirika la habari la Associated Press.
Kwa ujumla, zaidi ya watu 110,000 - raia wa Afghanstan na raia wa kigeni kwa pamoja wameokolewa kutoka kwenye uwanja wa ndege wa Kabul tangu uokoaji wa kutumia ndege ulipoanza yapata wiki mbili zilizopita.

Chanzo cha picha, US DEPARTMENT OF DEFENSE
Jumamiosi, ndege ya mwisho ya Italia kutoka Afghanistan aliwasili Rome. Italia ilisema kuwa iliwaokoa raia takriban 5,000 kutoka Kabul - ikiwani idadi kubwa zaidi kuliko nchi nyingine yoyote ya muungano wa Ulaya.
Ufaransa ilisema kuwa imewasafirisha kwa ndege nje ya Afghanistan zaidi ya watu 2,800 tangu tarehe 17 Agosti, huku Ujerumani ikisema iliwaokoa Waafghanistan takriban 4,000.
Mkuu wa majeshi ya Uingereza , Jenerali Sir Nick Carter, alisema kuwa "inasikitisha " kwamba hawakuweza kumuokoa kila mtu.
Ufaransa na Uingereza zitautaka Umoja wa Mataifa kubuni "eneo salama'' mjini Kabul kusaidia juhudi za uokoaji . alisema rais wa Ufaransa Emmanuel Macron.
Amesema itaruhusu jamii ya kimataifa kufanya kazi za kibinadamu na "kuimarisha shinikizo dhidi ya Taliban".

Chanzo cha picha, EPA
Tangu Taliban ilipochukua udhibiti wa Kabul tarehe 15 Agosti, uchumi wa Afghanistan uliporomoka huku wahisani wahisani wakiondoa usaidizi wao wa fedha na watu walioweka fedha zao walikitaka kuziondoa kwenye benki kutokana na wasi wasi.
Jumamosi umati wa waandamanaji ulikusanyika nje ya mabenki katika mji mkuu wa Afghanstan.
"Kama hali itaendelea na wafanyakazi wa serikali hawapati mishahara yao na wafanyabiashara hawawezi kupata pesa zao kutoka kwenye benki kwa ajili ya biashara, matokeo yatakuwa ya kutisha sana, na kutakuw ana umasikini katika jamii pia, na hakuna yeyote anayeweza kutatua suala hili ,"mwanaume mmoja aliiambia Reuters.














