Vita vya afghanistan:Saba wafariki kwenye msongamano katika uwanja wa ndege wa Kabul

tl

Chanzo cha picha, Reuters

Iliyochapishwa

Watu saba raia wa Aghanistan wamefariki kenye msongamano mkubwa wa watu nje ya uwanja wa ndege wa Kabul, wanaojaribu kuikimbia nchi hiyo, kufuatia kundi la Taliban kudhibiti nchi hiyo, kwa mujibu wa wizara ya ulinzi ya Uingereza.

"hali ni mbaya na inaleta changamoto kubwa lakini tunafanya kila tunachokiweza kukabiliana nayo kwa usalama kwa kadri itakavyowezekana," ilisema sehemu ya taarifa ya msemaji wa wizara hiyo.

Kumekuwa na vurugu nje ya uwanja wa ndege wa Kabul, ambapo maelfu ya raia wa Afghanistan wakijaribu kukimbia huku serikali za mataifa mengine zikihaka kuondoa raia wake na wengine wa Afghaistan.

Zaidi ya wanajeshi 4,500 wa Marekani wako katika uwanja huo wa ndege wa Hamid Karzai kwa muda kudhibiti na kusaidia kuweka mambo sawa, huku askari wengine wapatao 900 wa Uingereza wakiendelea na doria katika eneo hilo katika jitihada za kulinda ndege zinazowabeba watu kuwaondoa Afghanistan.

Wanamgambo wa Taliban wamekuwa wakiweka vituo maalumu vya ukaguzi karibu na uwanja huo na kuwazuia raia wa Afghanistan ambao hawana nyaraka na hati za kuingia uwanjani humo kwa ajili ya kusafiri.

Biden azidi kulaumiwa

Rais wa Marekani Joe Biden ameendelea kushinikizwa ili kuongeza muda wa kuondoa vikosi vya jeshi la nchi hiyo nchini Afghanistan. Ratiba ya sasa inaonyesha vikosi vya jeshi la nchi hiyo vitakuwa vimeondoka kabisa kwenye ardhi ya Afghanistan mpaka kufikia Agosti 31, 2021.

MO

Chanzo cha picha, MOD

Mataifa kadhaa yamekuwa yakisema haitawezekana muda huo wa hadi Agosti 31 kuweza kuwaondoa raia wote wa kigeni na hata wa nchi hiyo wanaokimbia kwa hofu ya usalama wao.

Waziri wa ulinzi wa Marekani Ben Wallace alisema kwamba "hakuna taifa litakaloweza kuondoa raia wake wote nchini humo".

Aliliambia gazeti la Mail kwamba muda hausubiri, ngumu kuzuia" wakati huu majeshi ya Uingereza yakielekea kuhitimisha shughuli zake za kijeshi Afghanistan, na kuo geza kwamba Uingereza itapasa kuinga mkono Marekani kama itaamua kusogeza uda mbele.

Wakati huo huo Mkuu wa masuala ya sera za nje wa Umoja wa Ulaya Josep Borrell amesema "kimahesabu haiwezekani" kuondoa watu 60,000 mpaka kufikia mwishoni mwa mwezi huu.

Borrell alisema mpaka sasa ni raia 150 wa Afghnasitan kati ya 400 walioajiriwa na Umoja wa ulaya ndiyo wameweza kuondolewa nchini humo, hii "hairidhishi kabisa".

"Ndege zinaondoka lakini watu wakiendelea kusalia bado," aliongeza.

Borrell aliiambia AFP kwamba alilalamika kwa wamerakani kwamba ulinzi wao kwenye uwanja wa ndege wa Kabul unakwamisha jitihada za waafghanistan waliokuwa wanafanya kazi na nchi ulaya kuingia uwanjani hapo ili kuondoka.

Waziri mkuu wa zamani wa Uingereza Tony Blair alikielezea kitendo cha Marekani kuondoa majeshi yake Afghanistan ni kama "janga, cha hatari na kisichokuwa cha ulazima".

Akizungumza kwa mara ya kwanza tangu Taliban washike hatamy jumapili iliyopita, Blair anasema kwa sasa kule kujitolea kwa vikosi vya jeshi vya kimataifa kumebadilika, vikosi vikipungua sanavimepungua sana na hakuna wanajeshi washirika aliyepiteza maisha katika kipindi cha miezi 18 iliyopita.

"Hatulazimika kufanya hilo. Tulichagua kulifanya," aliandika Blair kuhusu kuondolewa kwa wanajeshi wa kimataifa nchini Afghanistanl.

Blair, aliyekuwa madarakani wakati ikiivamia Afghanistan pamoja na mshirika wake Marekani baada ya mashambulizi ya septemba 11, 2001, alisema kuondolewa kwa vikosi hivyo ni kuwapa nguvu vikundi vya kijihadi.

Rais Biden ametaka kuondolewa kwa raia wote wa Marekani nchini Afghanistan lakini ameelzea operesheni ya kuwaondoa ni moja kati ya opereshi ngumu kuwahi kutokea katika historia ya nchi hiyo ".

Mtoto azaliwa kwenye ndege ya Marekani iliyokuwa inaondoa watu Afghanistan

Huku hayo yakiarifiwa mwanamke mmoja raia wa Afghanistan amejifungua ndani ya ndege huko nchini Ujerumani.

US Air Mobility Command/ Twitter

Chanzo cha picha, US Air Mobility Command/ Twitter

Katika machapisho yaliyochapishwa Twitter leo, mmoja wa wahudumu wa ndege hiyo alisema mwanamke huyo alikuwa anasafiri pamoja na familia yake kutoka mashariki ya kati kwenda Ramstein Air Base nchini Ujerumani kaba ya kushikwa na uchungu.

Baada ya kuanza kupata uchungu, kiongozi wa ndege hiyo aliamua kushusha ndege chini kidogo ya anga la kawaida, ili kupata hewa ya kawaida na kusaidia kuokoa maisha ya mama huyo.