Fahamu kwa nini watu huanza kupigana mabusu

Pareja besándose

Chanzo cha picha, Getty Images

Iliyochapishwa

Wengi wetu tunathamini sana busu la kwanza, lakini ni nini hufanya tukio la kubusu kuwa spesheli?

Ukweli ni kwamba, kupigana busu midomo ikiwa imeshikana sio njia pekee ya kuoneshana mahaba kama vile wengi wetu tunavyofikiria.

Kuna njia zingine za kupigana mabusu ...

Je njia tofauti zinazotumiwa na wanadamu kubusu zinaweza kufichua kile ambacho ni muhimu kwetu katika tendo hilo la kuoneshana mahaba?

Chini ya nusu ya jamii zote zinabusu kwa midomo, kulingana na utafiti ambao tamaduni 168 kutoka sehemu tofauti duniani zilichambuliwa.

William Jankowiak, mhadhiri wa somo la kimaumbile yaani anthropology katika Chuo Kikuu cha Nevada Las Vegas, aligundua kuwa ni asilimia 46 tu ya watu hubusu midomo ya wapendwa wao kimapenzi. Ishara zingine kama busu kati ya wazazi na watoto au salamu hazikujumuishwa.

"Nadhani kinachowafanya watu kubusiana, au kutobusiana, ni kwamba watu wanaweza kuonyesha mahaba yao kwa njia zingine nyingi ambazo ni zaidi ya kubusu la kawaida."

'Lakini ni jambo la kufurahisha anasema ni kutambua kwamba kulikuwa na muundo uliotiwa alama: Kadri kijamii unavyozidi kuwa kubwa, ndivyo tendo la kubusu linafanyika mara kwa mara."

Ladha asilia

Moja ya nadharia ambazo zinajaribu kuelezea kwanini wanadamu wana hitaji la kubusu zinaibua wazo kwamba wakati tukiwa watoto wachanga tuna ladha ya asili ya kugusa mdomo.

Kwa mtazamo huo, tunaunganisha kugusa na midomo na kitendo cha kunyonyesha na hiyo ni tafakari ya asili. Ni kichocheo ambacho ni chanya kwetu.

Madre besando a su bebé

Chanzo cha picha, BBC/Workerbee TV

Kuna nadharia nyingine ambayo inatokana na mabadiliko yetu ya zamani inadokeza kuwa akina mama na watoto wao walikuwa wakikaribiana mdomo kwa mdomo ili kupeanana chakula.

Mama zetu zamani walikuwa wakitafuna chakula na kutupatia moja kwa moja kupitia midomo yao.

Hali hiyo ya kulishana chakula imeonekana pia kwa sokwe katika mchakato wa malezi ya watoto wachanga wanapoanza kufundishwa kula.

Usikivu

Midomo yetu ni nyeti sana. Kwa kweli, ni moja wapo ya sehemu chache za mwili ambazo ni nyeti sana, ijapokuwa hatufuniki.

Midomo ni moja wapo ya sehemu chache za mwili ambazo ni nyeti sana, ijapokuwa hatufuniki.

Chanzo cha picha, Universal Images Group/Getty Images

Maelezo ya picha, Midomo ni moja wapo ya sehemu chache za mwili ambazo ni nyeti sana, ijapokuwa hatufuniki.

Kulingana na wataalam, utafiti umebaini kuwa hakuna busu kati ya wawindaji na wakusanyaji mawindo.

"Kwa nini iwe hivyo? Katika maeneo mengine , wawindaji na wakusanya mawindo hawavai nguo. Kumaanisha wanaweza kugusana sehehu yoyote ya mwili na wasihisi chochote. Lakini unapovalia nguo sehemu kubwa ya mwili imefunikawa na iliyobakia ni uso ", anasema mtaalamu mtaalam wa maumbile.

Zaidi ya miaka 3,000

Ushahidi wa zamani zaidi ulioandikwa juu ya tabia kama ya kubusu imeanzia kwenye maandishi ya Kihindu ya Vedic Sanskrit ya miaka 3,500. "Kadiri nguo zinavyoonekana, ndivyo mzunguko wa kubusu unavyoongezeka. Kadri unavyovaa nguo chache, ndivyo mzunguko unavyopungua," anasema Jankowiak.

Charles Darwin alielezea busu ya Malay.

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Charles Darwin alielezea busu ya Malaysia.

Katika tamaduni ambazo hazibusu mdomo, jamaa wanapata njia zingine za kuwa wa karibu, anasema Sheril R. Kirshenbaum, mwandishi wa "Sayansi ya busu."

"Kwa kweli kumekuwa na tamaduni nyingi ambazo watu hupeana mabusu ya mdomo kwa mdomo, kwa njia ambayo ni kama tunavyofanya leo. Lakini kuna busu la Kimalesia ambalo Darwin alielezea, ambapo wanawake walichuchumaa chini na wanaume waliwategemea na kunusa harufu yao kwa haraka kama wanavyofanya wanandoa, "anasema.

"Moja ya mazoea ya kushangaza ambayo nilipata katika utafiti wangu ni ile inayotokea katika Visiwa vya Trobriand (huko Oceania)."

Ni nini hufanyika mwilini watu wanapobusu?

Kwa nini huwa tunaelekeza vichwa vyetu kulia wakati tunabusu kinywa?

"Hapo wapenzi wanakaa ana kwa ana na wakati wanajisikia kuwa wa karibu wanaporamba kope zao, kitu ambacho kwa wengi wetu haionekani kama ishara ya mapenzi, lakini wao wanathamini sana."

Jambo muhimu juu ya busu za mdomo na aina zingine za mabusu ni kwamba ni wakati wa kuwasiliana kimahaba.

"Ni sehemu ya uaminifu na ukaribu nunaotumika kwa lengo la kuwa karibu na watu tunaowajali."

Sokwe

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Hisia ya kibinadamu ya harufu sio ya kali kama ile ya spishi zingine.

Binadamu walianza kupigana mabusu kutokana na hali ambayo haikutarajiwa: walikaribiana ili kupata ishara kwa wenza wao, na kwa kufanya hivyo, walianza kubusu.

Lakini ikiwa kupigana mabusu huwa na lengo maalum kwa nini hauoni wanyama zaidi wakibusu?

Mwandishi wa BBC Melissa Hogenboom alijibu swali hilo lililoulizwa na kitengo ya BBC Earth mwaka 2015, akisema moja ya sababu ni kwamba huenda umelazimishwa na mazingira kumkaribia mwenzako kwa lengo.

Hali hiyo huweza kusaidia kutoa taarifa tofauti muhimu: chakula, magonjwa, mhemko na mshikaman miongoni mwa vitu vingine.

Kwanini wanadamu hubusu ikiwa wanayama wengi hwabusiani?

Wanyama wengi wana hisia zaidi ya harufu kuliko yetu, kwa hivyo sio lazima waae karibu sana ili kuoneshana mahabaIjapokuwa ndege wengi huvunha midomo yao wakijaribu kuonesahan mahaba , wanyama wengi hutumia pua zao kutofautisha rafiki na adui, ni spishi chache sana za wanyama huleta pamoja midomo yao.

Pareja besándose

Labda ni kwa sababu uwezo wa wanadamu sio mzuri ikilinganishwa na spishi ya wanyama kama vile sokwe.

Wanayama wengine wana uwezo kunusa harufu ya wenzao bila kuleta pamoja nyuso zao.

Kwanini wanadamu hubusu ikiwa wanayama wengi hawabusiani?

Wanyama wengi wana hisia zaidi ya harufu kuliko yetu, kwa hivyo sio lazima waae karibu sana ili kuoneshana mahabaIjapokuwa ndege wengi huvunha midomo yao wakijaribu kuonesahan mahaba , wanyama wengi hutumia pua zao kutofautisha rafiki na adui, ni spishi chache sana za wanyama huleta pamoja midomo yao.

Labda ni kwa sababu uwezo wa wanadamu sio mzuri ikilinganishwa na spishi ya wanyama kama vile sokwe..

Wanayama wengine wana uwezo kunusa harufu ya wenzao bila kuleta pamoja nyuso zao.