Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Vita vya Afghanistan: Nchi hiyo itakuwa kimbilio la makundi ya kigaidi Taliban ikiwa madarakani?
Katika maeneo ya mbali, mabonde ya jimbo la Kunar la Afghanistan na kwenye majukwaa ya mazungumzo ya mtandaoni ya wapiganaji wa jihadi kuna shangwe kwa kile wafuasi wa al-Qaeda wanaona kama "ushindi wa kihistoria" wa Taliban.
Kuondoka kwa kufedhehesha kwa vikosi ambavyo kwa muda vilifukuza Taliban na al-Qaeda miaka 20 iliyopita kumekuja kama chachu kubwa ya morali kwa wanajihadi wanaopinga Umagharibi kote ulimwenguni.
Sehemu za kujificha ambazo sasa zinaweza kufunguliwa katika nafasi ambazo hazijatumiwa nchini ni tuzo inayowavutia, haswa kwa wanamgambo wa kikundi cha Islamic State (IS) wanaotafuta kupata kituo kipya baada ya kushindwa kwao huko Iraq na Syria.
Majenerali wa Magharibi na wanasiasa wanaonya kuwa kurudi kwa al-Qaeda nchini Afghanistan, kwa nguvu, ni jambo lisilo la "kuepukika".
Waziri Mkuu wa Uingereza Boris Johnson, akizungumza baada ya mkutano wa dharura, alionya kuwa mataifa ya Magharibi yanahitaji kuungana ili kuzuia Afghanistan isirudi nyuma kuwa kimbilio la vikundi vya kigaidi vya kimataifa.
Na Jumatatu Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres alitoa wito kwa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa "kutumia zana zote zinazoweza kukomesha tishio la kigaidi ulimwenguni nchini Afghanistan".
Lakini je, kurudi kwa Taliban moja kwa moja kunatafsiri kurudi kwa kambi za al-Qaeda na jukwaa la mashambulio ya kigaidi ya kitaifa yanayolenga nchi za Magharibi, kati ya nyingine?
Sio lazima, iwe hapana.
Kutafuta uhalali na kutambuliwa
Mara ya mwisho Taliban ilitawala nchi nzima, kutoka 1996-2001, Afghanistan ilikuwa serikali iliyotengwa.
Ni nchi tatu tu, Saudi Arabia, Pakistan na Falme za Kiarabu, zilitambua uhalali wao.
Pamoja na kuwanyanyasa watu wao wenyewe, Taliban walitoa makazi kwa shirika la Osama Bin Laden la al-Qaeda ambalo lilipanga mashambulio ya 9/11 dhidi ya Marekani mnamo mwaka 2001, na kuua karibu watu 3,000.
Waajiriwa wanaokadiriwa kutoka 20,000 kote ulimwenguni walipitia kambi za mafunzo za al-Qaeda, wakijifunza uuaji mbaya na kuunda kile kilichojulikana kama "chuo kikuu cha ugaidi" wakati walitawanyika kurudi nchi zao.
Leo Taliban bado wanajiona kama halali - ikiwa hawajachaguliwa kama watawala wa "Emirate wa Kiislamu wa Afghanistan" na watataka kutambuliwa kimataifa.
Tayari wanaonekana kuwa na shauku ya kubuni wazo kwamba wamekuja kurejesha utulivu, utulivu na mamlaka, baada ya ufisadi, ugomvi sifa ilizopewa serikali kwa miaka 20 iliyopita.
Wakati wa mazungumzo ya amani yaliyoshindwa yaliyofanyika Doha, iliwekwa wazi kwa washauri wa Taliban kwamba utambuzi huu unaotamaniwa unaweza kuja tu ikiwa watajitenga kabisa na al-Qaeda.
Tumefanya tayari, walisema Taliban. Hapana hawajafanya hilo, inasema ripoti ya hivi karibuni ya UN ambayo ilionesha uhusiano wa karibu wa kikabila na ndoa kati ya vikundi hivyo viwili
Wakati wa udhibiti wa kushangaza wa Taliban wa nchi nzima hivi karibuni, kumekuwa na taarifa kadhaa za kuonekana kwa "wageni" katika safu zao, yaani wapiganaji wasio wa Afghanistan.
Ni wazi pia kwamba kuna kupishana kwa kati ya maneno yanayosemwa na wapiganaji wa mstari wa mbele wa Taliban - wapatanishi na wasemaji kwa upande mwingine - na vitendo vingine vya kisasi vya vinavyofanyika.
Mnamo tarehe 12 Agosti, wakati Taliban walipokuwa wakiuelekea na mji mkuu, mwakilishi wa masuala ya kidiplomasia wa Marekani mjini Kabul aliandia katika ukurasa wa twitter:"Matamko ya Taliban huko Doha hayafanani na matendo yao huko Badakhshan, Ghazni, Helmand na Kandahar. Jaribio la kuhodhi madaraka kwa nguvu , hofu na vita vitasababisha tu kutengwa kimataifa. "
Nchi za Magharibi zinaweza kupata changamoto kudhibiti wapiganaji wa jihadi
Mtazamo wa Taliban ni juu ya kutawala Afghanistan kulingana na tafsiri yao kali ya Sharia, sheria ya Kiislamu, na sio zaidi ya mipaka yake.
Lakini wanajihadi wengine katika al-Qaeda na IS wanaweza kuwa na matarajio tofauti zaidi ya mipaka hiyo. Inawezekana kwamba wakati serikali mpya ya Taliban inaweza hata kutaka kuwazuia, kuna namna ambayo shughuli zao zinaweza zisitambuliwe
Dr Sajjan Gohel kutoka taasisi ya Asia Pacific anatarajia kuwa washiriki wa sasa wa 200-500 wa al-Qaeda wanaodhaniwa kuwa huko Kunar wataongezeka.
"Utekaji nyara wa Taliban wa mkoa wa Kunar una thamani kubwa ya kimkakati kwani una eneo lenye changamoto kubwa na mabonde yenye misitu mingi. Tayari, al-Qaeda ina uwepo huko ambayo itatafuta kupanuka."
Ikiwa hiyo itatokea, basi itakuwa kazi ngumu kwa Magharibi kudhibiti.
Kwa miaka 20 iliyopita imekuwa ikitegemea sana NDS, huduma ya ujasusi ya Afghanistan, na mtandao wake wa watoa habari wa kibinadamu pamoja na timu za Marekani, Uingereza na vikosi Maalum vya Afghanistan.
Yote ambayo sasa yamekwenda, na kuifanya Afghanistan kuwa "shabaha ngumu" katika suala la ujasusi.
Ikiwa kambi za mafunzo ya ugaidi zinatambuliwa na zipo, basi chaguzi za Washington zinaweza kushuka kwa mashambulio ya mbali ya ndege zisizo na rubani au mashambulio ya kombora, kama zile zilizomkosa Osama Bin Laden mnamo 1998.
Mengi, anasema Dk Gohel, itategemea iwapo mamlaka ya Pakistani inaweza kuzuia au kuwezesha kusafiri kwa wapiganaji wa kigeni kupitia eneo lao kwenda Afghanistan.