Jinsi mtandao gushi unavyochochea propaganda za kuiunga mkono China

Mtandao uliosambaa wa zaidi ya akaunti za mitandao ya kijamii gushi 35 unachochea propaganda zinazounga mkono ajenda za Uchina na kujaribu kuwaharibia sifa wale wanaoonekana kuwa wapinzani wa serikali ya uchina, kulingana na utafiti.
Lengo ni kuondoa uhalali wa nchi za magharibi na kuinua ushawishi wa China na sura yake nje ya taifa hilo, imesema ripoti ya taasisi kituo cha habari -Centre for Information Resilience (CIR).
Utafiti huo, ulioshirikishwa kwa BBC, ulibaini kwamba mtandao gushi wa utambulisho wa vyombo vya habari ulisambaza vibonzo vinavyoonesha miongoni mwa mambo mengine, tajiri wa kichina anayeishi uhamishoni Guo Wengui, mkosoaji wa China.
Watu wengine wenye utata waliooneshwa kwa njia ya vibonzo hivyo ni pamoja na "mfichua siri" mwanasayansi Li-Meng Yang, na Steve Bannon, mwanastratejia wa kisiasa wa Donald Trump.
Kile mmoja wa watu hawa binafsi amekuwa akishutumiwa kusambaza taarifa za upotoshaji, zikiwemo taarifa za uongo kuhusu ugonjwa wa Covid-19.

Baadhi ya akaunti -zilizosambaa kwenye mitandao ya Twitter, Facebook, Instagram na YouTube - hutumia utambulisho gushi wenye picha za kutungwa, huku nyingine zikionekana kudukuliwa baada ya awali kutumwa kwa lugha nyingine.
Hakuna ushahidi thabiti kwamba mtandao huo una uhusiano na serikali ya Uchina, lakini kulingana na CIR, ambacho ni kikundi kisichotafuta faida kinachofanya kazi ya kukabiliana na taarifa za upotoshaji, mtandao huo unafanana na mitandao inayounga mkono China ambayo awali ilifutwa naTwitter na Facebook.
Mitandao hii ilisambaza propaganda zinazounga mkono Uchina sawa na zile zinazofanywa na wawakilishi wa serikali ya Uchina na vyombo vya habari vya taifa.
Mengi kati ya maudhui yanayoshirikishwa kwa umma na mtandao huo yanaihusu Marekani, na hususan kuhusu masuala yanayoleta mgawanyiko kama vile sheria za umiliki wa silaha na siasa za ubaguzi wa rangi.
Moja ya ajenda zinazosukumwa na mtandao huo zimeionesha Marekani kama nchi ambayo inarekodi mbaya ya haki za binadamu.
Jumbe kutoka akaunti gushi zilitumia mauaji ya George Floyd miongoni mwa mifano, pamoja na ubagizi wa rangi dhidi ya raia wa Marekani wenye asili ya Asia.

Baadhi ya akaunti zilikanusha mara kwa mara ukiukaji wa haki za binadamu katika jimbo la Xinjiang, ambako wataalamu wanasema China iliwafunga takriban Waislam milioni moja kinyume na matakwa yao, zikitaja shutuma hizo kama "uongo uliotungwa na Marekani pamoja na nchi za magharibi".
"Lengo la mtandao huu linaonekana kuwa ni kuzichafua nchi za Magharibi na kukuza ajenda na fikra zinazounga mkono Uchina ," alisema Benjamin Strick, mwandishi wa ripoti ya CIR.
Mtandao ulifichuliwaje?
CIR ilibaini kampeni za alama ya reri au hashtags ambazo zilipendeelwa na mitandao iliyotambuliwa awali, na kufichua akaunti zaidi ambazo zinaonesha ishara ya kuwa sehemu ya harakati za ushawishi.
Ishara zilizokuwa zinaangaliwa ni pamoja na viwango vya juu vya shughuli za kuchochea kauli za propaganda na matumizi yanayojirudia rudia ya kampeni za alama za za leri au hashtags.
Akaunti mpya zilizobuniwa, majina ya watumiaji wa akaunti hizo ambayo yalionekana kutungwa, na akaunti zenye wafuasi wachache pia zilikuwa ni moja ya sababu za kuchunguzwa.

Chanzo cha picha, BENJAMIN STRICK / CIR
Watu bandia
Mwingi kati ya utambulisho wa akaunti za mitandao hii ilitumia picha zilizobuniwa - aambayo ni mbinu mpya inayowezesha kompyuta kubuni picha halisi za watu ambao hawapo.
Kinyume na picha za utambulisho za watu halisi zilizoibiwa , picha zilizotengenezwa na AI generated images, ambazo hubuniwa na aina ya mashine inayoitwa StyleGAN, haziwezi kupatikana unapozitafuta kwenye mtandao.
Matumizi ya picha gushi kwenye utambulisho katika kampeni ya habari za upotoshaji limekuwa ni jambo la kawaida na kumbi za mawasiliano ya mtandao zinakuwa na wasi wasi zaidi juu ya akaunti zinazoshukiwa.
Kwa kawaida, ukusanyaji wa picha za utambulisho huonesha mbinu mbali mbali za muonekano wa picha kwa mfano mtu kuweza kubadilisha mpangilio wa picha yenye we na macho.

Chanzo cha picha, BENJAMIN STRICK / CIR
Dalili nyingine ni kwamba kunakuwa na kufifia karibu na mwisho wa nywele, meno kuwa katika kona zisizo za kawaida, na kifaa kilichofifia kwenye uso.
Nyingi kati ya akaunti za Facebook zinaaminiwa zilizoaminiwa kuwa za mtandao huo zilikuwa na majina ya Kituruki.
Akaunti hizi huenda wakati mmoja zilikuwa zinamilikiwa na watu halisi lakini baadaye zilitekwa au kuuzwa na kupewa picha mpya za utambulisho.

Chanzo cha picha, BENJAMIN STRICK / CIR
CIR ilishirikisha utafiti kumbi za mitandao ya habari ya kijamii husika.
Facebook imeziondoa akaunti zilizoelezewa na utafiti kwenye ukumbi wake.
Msemaji wa Facebook alisema: "Katika mwezi wa Septemba 2019, tuliuondoa mtandao wa shughuli gushi ambao ulituma taarifa kuhusu mtindo wa maisha na kuchocheakuweka ''likes'' za kisiasa, mitandao hiyo ilikuwa ni ya Kichina.
Mtandao huu haukuwa na mawasiliano ya watu na tunaendelea kushirikiana na watafiti na wenzetiu katika sekta ya mitandao ya kijamii kuibaini na kuzuwia majaribio yake ya kurejea, kama akaunti hizo zilizotajwa katika ripoti ."
YouTube pia ilifunga akaunti katika mtandao huo kwa kukiuka miongozo ya kijamii ya YouTube.
Twitter nayo imesema kuwa sasa imeondoa takriban akaunti zote zilizotambuliwa na CIR, pamoja na mingine kadhaa inayohusika na mienendo inayofanana na hiyo. Ilisema uchunguzi wake bado unaendelea.
"Tutakapotambua harakati za kampeni ambazo tunaweza kuzihusisha na shughuli za taifa - ziwe zinaongozwa ndani au nje ya nchi-tunazifichua kwenye kumbukumbu ya umma.














