Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Fahamu namna unavyoweza kutambua ikiwa mtoto wako anapitia unyanyasaji
Unyanyasaji dhidi ya mtoto unachukuliwa kuwa matendo mabaya au nia ya kumdhuru mtoto ama kisaikolojia, kihisia, kingono au kimwili ama kutelekezwa na anayemtunza hadi kufikia miaka anayochukuliwa kuwa mtu mzima kwa nchi nyingi ikiwa ni miaka 18.
Anayemtunza anaweza kuwa mzazi au mtu mwingine wa familia au anayetoa huduma ya aina hiyo kama vile makocha wa michezo, mwalimu, mtu asiyemfahamu na kadhalika.
Pia ni muhimu kufahamu kuwa kumuonea mtu hakuko kwenye kundi hili lakini kunachukuliwa kama aina ya kuwasilisha aina mbalimbali za unyanyasaji.
Na kitendo kinaweza kuwa au kutokuwa cha kusababisha ghasia na kinaweza kutokea popote pale.
Baadhi ya Unyanyasaji ni pamoja na:
Unyanyasaji wa kimwili
Hii inatokea iwapo mtoto anapojeruhiwa kimwili au kuwa katika hatari ya kudhuriwa na mtu mwengine. Mfano, kumchoma, kumpiga mangumi, mateke au kumuuma, kumtupa mtoto au kumfunga na kamba na kadhalika.
Unyanyasaji wa kingono
Huu ni kushiriki kitendo chochote kile cha ngono ma mtoto kama vile kumpapasa, kumuingia kimwili, kumtumia vibaya au kumuweka katika hatari ya ponografia ya watoto, kumtumia ujumbe wa simu, barua pepe au mwingine wowote ambao unahisisha suala la ngono kwa namna yoyote ile. Kumuonesha mtoto viunge vya siri vya mwingine au hata kuwa na matani mabaya naye.
Unyanyasaji wa kiakili
Unyanyasaji wa kiakili kuna maanisha kuwa kuingia heshima au kudhuru kujithamini au ukuaji wake kihisia. Inajumuisha unyanyasaji wa maneno kama kuendelea kumdharau mtoto au kumkosoa pamoja na kumtenga, kumpuuza, kumkataa, kumtishia, au kumkemea.
Unyanyasaji wa kitiba
Hii inatokea ikiwa mtu atatoa taarifa za uwongo kuhusu afya ya mtoto na kudai kwamba anahitaji kupata matibabu na kumuweka katika hatari ya kujeruhiwa au kupata matibabu pasipo a haja.
Kumtelekeza
Kumtelekeza mtoto ni kushindwa kumpa mahitaji yake muhimu kama vile chakula, makazi, upendo, usimamizi, elimu au matibabu ili kumhakikishia afya njema.
Mambo kidogo ya msingi kuhusu unyanyasaji dhidi ya mtoto
- Upo wa aina mbalimbali
- Katika baadhi ya nchi duniani, kumuadhibu mtoto wako kwa kumchapa kunachukuliwa kama unyanyasaji dhidi ya mtoto
- Inaweza kuwa vigumu kubaini kama mtoto anapitia aina fulani ya unyanyasaji lakini ishara kama vile upweke, kulalamika sana kunaweza kusaidia
- Mtu ambaye anatekeleza unyanaysaji wakati mwingine pia naye huenda anahitaji usaidizi mfano kama vile mzazi ambaye ana msongo wa mawazo.
Ishara za unyayasaji zinaweza kujuisha:
Unaweza kuzichukulia ziifuatazo kama dalili lakini ni muhimu kujua kwamba sio lazima ziwe hizi hasa kwasababu kuna mengi mtoto anaweza kupitia.
Pengine kuwa na jeraha kwenye sehemu kama vile jicho, mgongoni, kuvunjika mifupa, vidonga kuchomwa na kadhalika.
Majeraha yanaweza kuwa zaidi ya moja pengine mgongo wote, mikononi au miguuni.
Kukataa kwenda sehemu au kuanza kulia kabisa wakati anatakiwa kufanya jambo fulani kama vile kwenda shuleni, au sehemu ambayo unyanyasaji unaweza kutokea au akakulilia sana wakati unaondoka nyumbani na ukirejea anakurukia na kukumbatia hasa, hataki hata kumuona uliye muacha naye mchana kutwa.
- Anaonekana kuwa na hofu akiwa na mtu fulani
- Pia kuwa muangalifu zaidi kama ambaye kuna kitu anakitarajia kitatokea kisichopendeza
- Kuonekana kutokuwa na haja ya kitu fulani, kuwa na wasiwasi au kuwa mwoga
- Kutokuwa na ukaribu kabisa na anaye mtunza
- Kujiondoa kwa marafiki na wengine
- Kukimbia nyumbani
- Kuota ndoto za ajabu usiku
Pia wakati mwingine, mtu mzima aliye naye kama yeye ndio mwenye kumnyayasa, unaweza kumuona ya yafuatayo:
Kuwa mkali kweli kweli akiwa na mtoto
Kuonesha tabia ya ajabu kama vile kutokuwa na mipaka na mtoto
Badala ya kumrekebisha, kila wakati anakuwa na hasira naye na kumtia hofu
Wataalam wa watoto wanashutumu aina yoyote ile ya unyanyasaji dhidi yam toto lakini ifahamike kwamba kuna baadhi ya wazazi wanaotumia kiboko kama njia moja ya kumrudi mtoto. Lakini, ili isiwe unyanyasaji mzazi au mwangalizi anatakiwa asipitishe kipimo cha adhabu ya aina hiyo.
Ni muhimu pia unaposhuku pengine kuna kitu ambacho mtoto wako anapitia kisicho cha kawaida, ni muhimu kuanza kufuatilia taratibu ili kujua ukweli badala ya kupuuza, unaweza kuja kujuta baadaye.
Cha msingi zaidi katika ukuaji wa mtoto mwenye afya njema kiakili, kimwili, kihisia na kisaikolojia ni kila mmoja katika jamii kuwajibika.