Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Simulizi ya bibi wa miaka 106 aliyekataa kuitwa 'mzee'
Bi. Eileen Kramer mwenye umri wa miaka 106, anaonekana kuendelea na kazi zaidi licha ya umri aliokuwa nao.
Ameandika simulizi yake akiwa nyumba ya kuwaangalia wazee, anachapisha vitabu na ameingia katika mashindano makubwa ya uchoraji nchini Australia.
Baada ya miongo kadhaa ya kuishi nje ya nchi, Bi Kramer alirudi nyumbani Sydney akiwa na miaka 99. Tangu wakati huo, alishirikiana na wasanii kutengeneza video kadhaa kuonesha kipaji chake na mapenzi yake ya kucheza muziki.
Bi Kramer bado anacheza muziki - akiwa na neema, na kuonyesha miondoko ya kushangaza akiwa anatumia anatumia sehemu ya juu ya mwili wake.
Katika picha zake za miaka ya hivi karibuni, akiwa anacheza kwa kupendeza.
"Tangu niliporudi Sydney nimekuwa na kazi nyingi sana -Nilishiriki katika maonesho matatu makubwa ya muziki katika taasisi ya kitaifa ya sanaa ijulikanayo kama NIDA.
"Nilishiriki matamasha mawili makubwa huko Adelaide na Brisbane, Nimekuwa katika filamu , na nimefanya maonesho kadhaa madogo, nimeandika vitabu vitatu na leo nina muda wa kuzungumza na wewe!" amesema hayo akiwa nyumbani kwake.
Mara nyingine anaulizwa anapata wapi nguvu - na siri yake ni ipi inayomfanya aweze kucheza akiwa na umri mkubwa kiasi hicho.
Jibu lake huwa nimekataa neno "uzee" na "umri" katika misamiati yake. Na alinikataza nimuita mzee katika mazungumzo yetu.
"Ninasema: Mimi sio mzee, Nimekuwa hapa muda mrefu tu na kujifunza mambo kadhaa.
"Huwa sihisi kile ambacho watu wanasema au wanataka tujihisi wakati tukiwa wazee.
Tabia yangu iko hivi tangu nikiwa mtoto."
Miaka ya hivi karibuni Bi Kramer amekuwa mahiri katika umati wa watu kwa mitindo ya densi, amefanya kazi kadhaa za kucheza muziki katika maisha yake.
Alikuwa katika mpango wa kutengeneza video yake ya densi lakini hali ya kujifungia ndani iliyotokea Sidney ilivuruga mpango wake. Lakini si kwa muda mrefu. "Sikuweza kutoka nje kwenda kwenye eneo la kufanyia video, badala yake nliandika kitabu", alisema huku akicheka. "Hii ni hadithi kuhusu jinsi tulivyotengeneza filamu."
Eneo la kutengenezea filamu ni maalum kwa Bi Kramer. Lipo ndani ya Moreton Bay, mtini katika kitongoji cha Sydney cha Glebe.
Harufu ya miti, muonekano wa Moreton bay na sauti za ndege wakicheka huku wamekaa ni vitu vilivyo mshawishi Bi Kramer kurudi Sidney.
''Miti iliboresha mitindo yangu ya kudensi'' alisema.
" Umewahi kuona...? unajisikia kama uko katika ikulu ya hadithi ya kusadikika. Inanikumbusha enzi za utoto"
Maisha yenye kupendeza
Alikuwa mlimbwende wa kupiga picha nusu uchi mpaka kuwa mwanamitindo mpaka kuwa mzee zaidi -mwenye umri wa miaka 104 - aliyetunukiwa tuzo kubwa ya sanaa ya uchoraji nchini Australia.
Alizaliwa mjini Sydney, Bi Kramer alipata mafunzo ya kucheza muziki na baadae akawa anafanya maonesho Australia kwa miongo kadhaa.
Alisafiri mpaka India, na baadae kuishi Paris na baada ya hapo kuhamia New York -ambako aliishi mpaka alipokuwa na miaka 99.
Tasnia yake ya kucheza ilitamba katika mabara manne katika karne moja na mara zote ni jambo ambalo alilipenda.
"Kuwepo na wachezaji katika maisha yangu yote, sijawahi kuwa mpweke," amesema.
"Sio kama mimi, baadhi waliolewa na kuwa na watoto au kurudi Ulaya.Lakini niliweza kuhimili hekaheka za wacheza dansi katika maisha yangu yote."
Aliishi sana mji wa Paris wakati wa ujana wake , bi Kramer anasema namna pekee aliyokuwa anaweza kulipa kodi ni kuwa msanii wa ulimbwende.
"Ilikuwa kazi hatari lakini nilijua wateja na tabia zao ," alisema.
Kupiga picha bila nguo lilikuwa si jambo kubwa kwake kwa sababu ilikuwa ni kwa ajili ya sanaa.
Alijifunza kazi hiyo kutoka kwa wasanii maarufu wa Paris.
Alijifunza pia kucheza mtindo wa kucheza kabla ya kuhamia New York.
Aliporejea Australia, alifurahia kuwa kuna baadhi ya mambo ambayo yalikuwa hayajabadilika kama vile - kuona watu wakila samaki na viazi vya kukaanga na mambo mengine ambayo yalikuwa tamaduni yao kubwa.
Ushauri mzuri ambao aliwahi kupokea ulitoka kwa bi. Bodenwieser, muasisi wa muziki aina ya ballet, ni kuhusu mahusiano ya muda mfupi wakati wa ziara za maonesho ya muziki.
"Mwanamke anaweza kupata mwanaume mara moja kwa jinsi atakavyosimama na sio kwa wale wanaopita," amesema. "Tumewaumiza moyo baadhi!"
Leo hii msaidizi wake, Sue Healey, ameelezea kufanya kazi na bi Kramer kuwa sawa na kuishi historia.
"