Ladiifa Annaadi: Mwanamke wa kwanza Misri kuwa rubani

Ladiifa Annaadi

Chanzo cha picha, Wikipidia

Iliyochapishwa

Mwishoni mwa mwaka 1933, mwanaharakati wa haki za wanawake Huda Shacraawi alituma ujumbe wa pongezi kwa msichana aliye na miaka ishirini, akisema, "Umeipa heshima nchi yako, umeinua matamanio yetu na kuinua maendeleo.

Ladiifa Annaadi akiwa na miaka 26 alikuwa mshindi wa mashindano ya ndege nchini Misri. Alikuwa mwanamke wa kwanza Muislamu kutoka nchi ya Kiarabu kuwa rubani.

Ladiifa Annaadi ni nani?

Alizaliwa Cairo mnamo mwaka 1907, Ladiifa Anadi alikuwa binti wa baba ambaye alifanya kazi katika mashine ya uchapishaji ya kifalme na akajiunga na masomo rasmi ambayo yalikuwa na idadi ndogo ya watoto wa rika lake wakati huo.

Wakati alikuwa katika shule ya kati, Ladiifa alisikia kuhusu safari za ndege. Hilo lilikuwa jambo jipya akilini mwake hadi alipoamua kulitimiza.

Mnamo mwaka wa 1932 shule ya anga ya Misri ilianzishwa huko Almaada.

Lakini ili kuanza mafunzo, ilibidi waulizwe maafisa wawili wa polisi ili kuona ikiwa jamaa zake walikuwa tayari kulipia masomo.

Ladiifa alikwenda kwa usimamizi wa shule ya mama yake, ili kutimiza sharti la kwanza na kwa bahati akapata kazi shuleni na kuwa katibu mukhtasi ili aweze kulipa bili. Baba yake hakujua kwamba alikuwa ameenda shule.

Ladiifa alihudhuria madarasa mawili kwa wiki mapaka alipopata mafunzo ya saa 67 aliyoyapata kwa walimu wa Misri na wageni.

Mnamo 1933, Ladiifa alipokea leseni ya kurusha ndege na kuwa mwanamke wa kwanza wa Misri kupata leseni na msichana wa pili ulimwenguni.

Ladiifa alikuwa mtu wa 34 kupata leseni nchini Misri.

Mwezi Desemba mwaka 1933, mashindano ya kurusha ndege kwa kasi yalifanyika nchini humo yaliyohusisha marubani kutoka nchi zaidi ya 60

Ladiifa alimaza mchuano huyo. Alimshangaza kila mmoja kwa kuwa mtu wa kwanza kufikia mashindano. Wakati wote alikuwa akiongoza dakika moja mbele.

Lakini ushindi wake ulikataliwa kwa madai kuwa alikiuka masharti ya shindano hilo na akapatiwa tuzo na mshindani wake kutoka Ufaransa.

Ladiifa akawa maarufu kwani alikua mwanamke wa kwanza kuwa rubani nchini Misri.

Salam Musa anaandika katika makala yake ya Al-Majalla Al-Jadida, Januari mwaka 1934 kuwa: ''Lakini Misri ilipigana dhidi ya tamaduni hizi na kushinda vita. Baki nyumbani..pamoja na hayo alikuwa na uthubutu wa kuishangaza dunia.''

''Wanawake wako mstari wa mbele.....na ndicho tunachokiona katika maendeleo ya Ladiifa Anadi ni ishara kwa kila raia wa Misri.''

Ladiifa alisema kuwa baba yake alighadhabika sana alipobaini hili na hakuamini ujuzi wake mpaka siku moja alipoamua kumbeba kwenye ndege na kuvuka piramidi. Safari hiyo aliielezea Ladiifa kuwa ilikuwa bora zaidi katika maisha yake.

Ladiifa amefungua milango kwa mustakabali wa vizazi vijavyo vya wasichana wa Misri, akiwemo Linda Masood, Aziz Maxram, Aida Takla na wengine.

Ladiifa alihamia Uswizi, ambako aliishi mpaka mwaka 2002, ambapo alifariki akiwa na umri wa miaka 95.