wanafunzi 7 na mwalimu wafariki katika tukio la ufyatuaji risasi shuleni nchini Urusi

School No 175 in Kazan where the attack happened

Chanzo cha picha, Getty Images

Iliyochapishwa
Muda wa kusoma: Dakika 1

Takriban watu 8, miongoni mwao watoto wa shule, wameuawa kwa kupigwa risasi katika shule moja katika mji wa Urusi wa Kazan, ripoti zinasema.

Mwalimu mmoja pia amefariki katika tukio hilo kilomita 820 (maili 510) mashariki mwa Moscow.

Watu wawili waliripotiwa kufyatua risasi na mvulana mwenuye umri wa miaka 17 anasemekana kuzuiliwa.

Mlipuko ulisikika na haijulikani ni nini kilitokea kwa mshambuliaji wa pili. Kazan iko katika jamhuri ya Waislamu wengi ya Tatarstan.

Polisi waliojihami vikali na magari ya ambulansi walionekana nje ya shule hiyo, na video moja katika mitandao ya kijamii ilionyesha watoto wengine wakiruka kutoka madirisha kutoroka pamoja na watu waliojeruhiwa kuhamishwa.

Rais wa Tatarstan Rustam Minnikhanov aliwaambia waandishi wa habari nje ya shule hiyo kuwa ni janga na kwamba watoto 12 na watu wazima wanne walikuwa wakitibiwa hospitalini. "Gaidi huyo amekamatwa. Ana miaka 19. Yeye ni mmiliki wa silaha aliyesajiliwa," alisema.

Video moja kwenye mitandao ya kijamii ilimnasa kijana mmoja akiwa amelala chini akionekana kuzuiliwa nje ya jengo hilo.

Ruka X ujumbe
Ruhusu maudhui? (Mitandao ya kijamii)

Mkala hii imebeba madhui yaliyotoka kwenye mitandao ya kijamii. Tunaomba ruhusa yako kabla kitu chochote hakija pakiwa, sababu wanaweza wakawa wanatumia Cookies na tekinolojia nyingine. Unaweza ukasoma sera sera ya kutumia cookies katika mitandao ya kijamii kabla ya kukubali. Kutazama maudhui haya chagua accept and continue

Onyo: Imetoka kwingine na inaweza kuwa na matangazo

Mwisho wa X ujumbe