Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Ghasia Jerusalem: Makabiliano mapya yaibuka kabla ya maandamano ya wazalendo kuanza
Kumekuwa na mapigano kati ya Wapalestina na polisi wa Israeli nje ya msikiti wa Al-Aqsa huko Jerusalem, kabla ya maandamano ya kitaifa ya wayahudi.
Zaidi ya watu 300 walijeruhiwa, wakati umati wa watu uliporusha mawe na maafisa walirusha magruneti na risasi za mpira.
Hayo yanakuja wakati wa kuongezeka kwa mvutano katika jiji hilo, ambalo limekuwa na machafuko wiki kwa kadhaa.
Mapema, polisi wa Israeli waliamua kuwazuia Wayahudi kutembelea kiwanja ambacho msikiti uko wakati wa matembezi ya siku ya ya Jerusalem ya kila mwaka
Hafla hiyo huadhimisha siku ambayo Israeli iliiteka Jerusalem Mashariki - makao ya Jiji la Kale na maeneo yake matakatifu - mnamo 1967, na kawaida hushuhudia mamia ya vijana wa Israeli wanaopeperusha bendera wakipitia maeneo ya Waislamu, wakiimba nyimbo za kizalendo.
Tukio hilo linachukuliwa na Wapalestina wengi kama uchokozi wa makusudi dhidi yao. Matembezi ya mwaka huu pia yanafanyika katika siku za mwisho za mwezi mtukufu wa Waislamu wa Ramadhan.
Msikiti wa al-Aqsa , ni eneo la tatu takatifu zaidi katika Uislamu, na upo katika juu ya mlima unaofahamika na Waislamu kama Haram al-Sharif (mahala patakatifu) na kwa Wayahudi kama Mlima wa hekalu. Wayahudi wanautambua kama eneo la mahekalu mawili yanayotajwa katika biblia na eneo takatifu zaidi katika dini ya Juda.
Ghasia za hivi karibuni zimefuatia siku kadhaa za makabiliano baina ya polis wa Israeli na Wapalestina katika eneo jirani la wilaya ya Sheikh Jarrah ya Jerusalem Mashariki, huku kukiwa na uwezekano wa kuziondoa familia za Wapalestina kutoka kwenye nyumaba zao huko na walowezi jambo linalosababisha hasira kwa Wapalestina.
Mahakama ya juu zaidi ya Israel ilikuwa inatarajiwa kusikiliza kesi ya muda mrefu Jumatatu kuhusiana na eneo hilo, lakini kikao cha mahakama kiliahirishwa kutokana na ghasia.
Nini kilitokea katika msikiti wa al-Aqsa?
Polisi wa Israeli walisema maelfu ta Wapalestina walijipanga kama uzio katika jengo usiku wakiwa wamejihami kwa mawe na chupa za vilipuzi vya moto wakijiandaa kwa makabiliano wakati wa siku ya maandamano ya siku ya bendera ya Jerusalem ambayo yalikuwa yamepangwa kuanza saa kumi za jioni.
Maafisa waliamrishwa kuingia ndani ya eneo la msikiti "kuzima ghasia kwa kutumia mbinu za kutawanya maandamano " Jumatatu asubuhi baada ya kituo cha polisi kushambuliwa na mawe kutupwa kuelekea karibu na barabara iliyopo karibu, iliongeza.
Kwa zaidi ya saa moja, polisi walifyatua maguruneti ya plastiki dhidi ya Wapalestina ambao waliwatupia mawe na vitu vingine.
Video zilizotumwa kwenye mitando ya kijamii zinaonesha umati wa watu ukikimbia kutafuta maficho na guruneti zikianguka ndani ya msikiti.
Wakati wa makabiliano nje ya kuta za mji wa kale -Old City walls, gari lilipigwa kwa mawe kabla ya kugonga kizuizi cha barabarani na kumgonga mwanaume mmoja.
Shirika la Kipalestina la Red Crescent limesema kuwa Wapalestina 305 walijeruhiwa katika makabiliano hayo, na kwamba 228 wengine walipelekwa hospitalini kwa matibabu. Saba kati yao wako katika hali mahututi.
Waziri Mkuu wa Israel, Benjamin Netanyahu, aliwatetea polisi.
"Hivi ni vita baina ya uvumilivu na kutokuwa na uvumilivu, kati ya ghasia zilizo kinyume na sheria na sheria ," alisema. "Watu wanaotaka kuchukua haki zetu na kutulazimisha kwa kipindi kuwa imara, kama vile wanavyofanya maafisa wa polisi."
Rais wa Mamlaka ya Wapalestina Mahmoud Abbas alilaani hatua za Israeli.
Vikosi vya uvamizi vya Israeli kwa ukatili vinavamia na kuwapiga waumini katika msikiti wa uliobarikiwa wa Al-Aqsa Mosque na mazingira yake ni changamoto kubwa kwa jamii ya kimataifa ," alisema msemaji wake Nabil Abu Rudeineh.
Makabiliano ya Jumatatu yalichochewa na machafuko ya mwishoni mwa juma baina ya Wapalestina na polisi wa Israeli katika msikiti wa al-Aqsa ambayo yalisababisha kujeruhiwa kwa mamia ya watu.
Makabiliano baina na Wapalestina na Waisraeli yaliripotiwa katika mji wa kaskazini mwa Israeli wa Haifa, na karibu na mji wa Ukingo wa magharibi wa Ramallah.
Mfalme Abdullah II wa Jordan, ambayo ni msimamizi wa maeneo matakatifu ya Waislamu na Wakristo ya Jerusalem amelaani "ukiukaji wa Israeli na vitendo vya kuzidisha ghasia katika msikiti uliobarikiwa wa al-Aqsa ".
Jordan ilipata mamlaka ya uangalizi wa maeneo hayo matakatifu ilipotwaa maeneo West Bank na Jerusalemu Mashariki katika vita vya Masharika ya Kati vya mwaka 1948, na iliruhusiwa kuendelea na kazi hiyo baada ya eneo hilo kuangukia mikononi mwa Israeli mwaka 1967.
Pande zinazohusika katika mazungumzo ya Mashariki ya Kati - Marekani, Muungano wa Ulaya, Urusi na Umoja wa Mataifa-pia zimeelezea hofu yao kubwa juu ya ghasia, na kuzitaka pande zote husika kuonesha subira.
Kwanini Jerusalemu ni eneo muhimu
Mji, wenye maeneo matakatifu, ni eneo ambalo limekuwa mahala panapozozaniwa kwa karibu miongo yote ya mzozo baina ya Israel na Wapalestina.
Kando na umuhimu wake wa kidini yapo pia madai ya taifa - Israel ilitwa eneo la Jerusalemu Mashariki na inauchukulia mji wote kama mji wake mkuu, ingawa hili halitambuliwa ni nchi nyingi.
Wapalestina wanadai nusu ya eneo la Mashariki kama mji mkuu wa taifa lao wanalotumaini kuwa nalo.