Msikiti wa Al-Aqsa: Makumi wajeruhiwa katika makabiliano mjini Jerusalem

Maelezo ya video, Wapalestina wakabiliana na polisi wa Israeli mjini Jerusalem
Iliyochapishwa
Muda wa kusoma: Dakika 2

Wapalestina 163 na maafisa sita wa polisi wa Israel wamejeruhiwa baada ya ghasia kuzuka mjini, madaktari wa Palestina na polisi wa Israel wamesema.

Watu wengi walijeruhiwa katika Msikiti wa Al-Aqsa, ambako polisi wa Israeli walifyetua risasi za mpira na vilipuzi vya mikononi huku Wapalestina wakirusha mawe na chupa.

Hali ya taharuki imepanda kufuatia hofu ya kufurushwa kwa Wapalestina katika ardhi inayodaiwa na walowezi wa Kiyahudi.

Shirika Red Crescent limefungua hospitali ya muda uwanjani kuwatibu waliojeruhiwa.

Jengo la Al-Aqsa liko eneo la kale mjini Jerusalem na Waislamu wanaliita al-Haram al-Sharif huku Wayahudi wakiliita Temple Mount.

Eneo hili mara kwa mara linakumbwa na ghasia, ambazo zilizuka tena usiku wa Ijumaa baada ya maelfu ya watu kukusanyika kwa ibada ya Ijumaa ya mwisho ya mwezi mtukufu wa Ramadhan.

Polisi wa Israel walisema wametumia nguvu kupita kiasi "kurejesha utulivu" kufuatia "maandamano ya maelfu ya waumini" baada ya sala za usiku.

Afisa wa Aqsa ametoa witoa wito wa utulivi kwa kutumia vipaza sauti vya Msikiti huo. "Polisi lazima wasitishe mara moja kuwarushia waumini guruneti, na vijana lazima watulie na kusalia kimya!", Shirika la habari la Reuters liliwanukuu wakisema.

Watoaji huduma za dharura wa Shirika la Red Crescent la Palestina wamesema watu 88 waliojeruhiwa wamepelekwa hospitali baada ya kupigw ana risasi za mpira. Polisi wanasema maafafisa sita waliojeruhiwa wanahitaji huduma za matibabu.

Clashes near Al Aqsa Mosque, 7 May

Chanzo cha picha, Reuters

Maelezo ya picha, Wapalestina 163 na polisi sita wa Israel wamejeruhiwa baada ya ghasia kuzuka.
Israeli police walk near the Dome of the Rock during clashes with Palestinians, 7 May

Chanzo cha picha, Reuters

Maelezo ya picha, Polisi wa Israeli katika eneo linalogombaniwa na Waislamu na Wayahudi

Jmaii ya kimataifa pia imetoa wito wa kusitishwa kwa ghasia hizo za Ijumaa, baada ya taharuki kuzuka kufuatia tishio la kufurushwakwa famili aza Kipalestina katika wilaya ya Shaikh JarrahMashriki mwa Jerusalem.

Msemaji wa Wizara ya mambo ya nje wa Marekani amesema Washingnton "ina wasi wasi kuhusu ghasia zinazoshuhudiwa". Muungano wa Ulaya, kwa upande wake umelaani ghasia hizo ukisema "waliohusika pande zote mbili lazima wawajibishwe".

Mshirikishi maalum wa Umoja wa Mataifa katika Mchakato wa Amani wa Mashariki ya Kati Tor Vennesland, ametoa wito kwa pande zote mbili "kuheshimu hadhi ya jiji la kale la Yerusalem kwa kwa maslahi ya amani na utulivu."

Ruka X ujumbe
Ruhusu maudhui? (Mitandao ya kijamii)

Mkala hii imebeba madhui yaliyotoka kwenye mitandao ya kijamii. Tunaomba ruhusa yako kabla kitu chochote hakija pakiwa, sababu wanaweza wakawa wanatumia Cookies na tekinolojia nyingine. Unaweza ukasoma sera sera ya kutumia cookies katika mitandao ya kijamii kabla ya kukubali. Kutazama maudhui haya chagua accept and continue

Onyo: Imetoka kwingine na inaweza kuwa na matangazo

Mwisho wa X ujumbe

1px transparent line

Umoja wa Mataifa umesema Israel inastahili kusitisha mpango wa kuwafukuza wakazi na kujiepusha na "utumiaji wa nguvu" dhidi ya waandamanaji.

Mahakama ya Juu Zaidi ya Israel itasikiza kesi ya mzozo wa muda mrefu wa kisheria siku ya Jumatatu.

Israel imekalia eneo la Mashariki ya Yerusalem tangu mwaka 1967 wakati wa vita vya Mashariki ya Kati na inachukulia eneo hilo kama mji wake mkuu, ijapokuwa halijatambuliwa na sehemu kubwa ya jamii ya kimataifa.

Wapalestina wanadai Mashariki ya Yerusalemu kama mji wao mkuu ujao azma ya kupata uhuru itakapotimia.

Temple Mount map