Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Virusi vya corona: Marekani yaunga mkono ruzuku ya hakimiliki ili kuongeza usambazaji wa chanjo
Marekani imeunga mkono hatua ya Shirika la biashara dunaini (WTO) ya kuondoa kwa muda hakimiliki kwa ajili ya virusi vya corona.
India na Afrika Kusini walipendekeza mpango, ambao walisema utaongeza uzalishaji wa chanjo kote duniani.
Lakini watengenezaji wa madawa wanadai kuwa huenda hatua hiyo isiwe na ufanisi uliotarajiwa.
Mwakilishi wa Marekani wa masuala ya biashara Katherine Tai alisema kuwa "kipindi cha dharura kinahitaji hatua za dharura ".
Bi Tai amesema kuwa Marekani sasa itaanza mazungumzo ya mashauriano katika WHO kujaribu kupata ruzuku, lakini akatahadharisha kuwa hii inaweza kuchukua muda.
Mataifa mia moja kati ya mataifa 164 wanachama wa WTO wanasemekana kuunga mkono uamuzi huo na jopo la hakimiliki linatarajiwa kujadili suala hilo mwezi ujao.
India na Afrika Kusini walikuwa ndio sauti kuu katika kundi la nchi zipatazo 60 ambazo kwa miezi sita iliyopita zimekuwa zikijaribu hakimiliki ya chanjo iwekwe kando.
Hatahivyo, walikutana na upinzani mkubwa kutoka kwa utawala uliopita wa rais wa Donald Trump, Marekani na Muungano wa Ulaya. Bw Biden alipendekeza ruzuku wakati wa kampeni ya urais ya mwaka 2020.
Akizungumzia kuhusu hatua ya hivi punde ya Marekani, Kamishna wa Muungano wa Ulaya Ursula von der Leyen alisema " EU iko tayari kjadili mapendekezo yoyote ambayo yatashugulikia mzozo katika hali ya ufanisi na uhalisia".
Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron amebadili msimamo wake, sasa anasema kuwa "anaunga mkono kabisa hatua ya ruzuku ".
Msemaji wa serikali ya Uingereza amesema Uingereza ina "fanya kazi na wajumbe wa WTO kutatua suala hili " na "iko katika mazungumzo na Marekani na wajumbe wa WTO ikusaidia kuongezeka kwa uzalishaji na kusambaza chanjo za Covid-19 ".
Mkuu wa shirika la afya duniani ameliita tangazo la Marekani "kipindi kisichoweza kusahaulika " katika mapambano dhidi ya Covid-19.
Unaweza pia kusoma:
Matarajio ya ruzuku yamesababisha kuongezeka kwa hisa katika makampuni ya madawa ya Pfizer, Moderna na Novavax.
Hakimiliki ni pamoja na ubunifu, kama vile uvumbuziambavyo hulindwa na mmiliki, hati miliki na nembo za biashara . Hii inazuia haki za kunakili na kumruhusu mbunijfu kulipwa fedha.
Wenye akilimiliki hutoa viwanda vyao vya uvumbuzi, umiliki wa kipindi kifupi juu ya uzalishaji kulipia garama za utengenezaji na kuwashawishi wawekezaji.
Makampuni ya Biotech yanadai ulinzi mkubwa wa hakimiliki umetoa motisha kwa makampuni kutengeneza chanjo za corona kwa kipindi ambacho hakijawahi kushuhudiwa.
Ruzuku itamaaninisha nini?
Iwapo itaidhinbishwa, wanaoiunga mkono wanasema, ruzuku itaruhusu uzalishaji wa chanjo kuwa mwingi na kutoa dozi za bei nafu kwa nchi masikini.
Nchi nyingi zinazoendelea zimedai kuwa sheria ambazo nchi zinahitaji kuzifuata kulinda hakimiliki ni kikwazo cha kuongeza uzalishaji wa chanjo na bidhaa nyingine zinazohitajika katika kukabiliana na janga.
Mkuuwa WHO, Tedros Adhanom Ghebreyesus, ameutaja uamuzi wa Marekani kuwa "wa kihistoria" na akasema kuwa ni "kipindi ambacho hakitasahaulika katika vita dhidi ya Covid-19".
Shirika lisilo la kiserikali la madaktari wasio na mpaka MSF - limesema kuwa hatua hiyo "inaongeza upoatikanaji wa kutosha na wa muda wa dawa hizi za kunusuru maisha kutokana na janga la Covid-19 linaloendelea kuathiri dunia."