Aliyejirusha akitaka kujitoa uhai ampa ulemavu wa milele

گریس اسپنس گرین
Iliyochapishwa

Grace Spence Green, 22, alikuwa na imani kubwa kwamba hatma yake ya maisha ni yenye kufurahisha. Alikuwa akipenda sana kupanda milima, mwenye kufurahia maisha na shauku ya kupata shahada ya udaktari.

Siku moja wakati ana kwenda kufanya manunuzi, Grace alikumbana na kile ambacho kingebadilisha mkondo wa maisha yake kabisa. Fuatilia simulizi ya Grace ya 'sekunde kadhaa tu zilizobadilisha maisha yake kabisa'.

Siku ya tukio

Oktoba 2018, Grace alianza mwaka wake wa nne katika shule moja ya utoaji mafunzo ya tiba. Anakumbuka alikuwa amemaliza miezi miwili kama tarajali katika hospitali moja huko England, akiwa anaendelea vyema katika wadi ya wanawake.

Siku ya tukio, rafiki ya Grace alikuwa ameenda kumchukua kutoka eneo la Middleton kumpeleka London ambako alitarajiwa kutoa mafunzo ya upandaji mlima kwa watoto wa darasa moja.

Lakini pia walitaka kununua vitu kidogo kwenye duka kubwa la manunuzi na hapo ndipo walipoamua kupanda treni kuelekea huko.

Kwasababu lifti haikuwa inafanyakazi, wakalazimika kupitia njia ndefu kufika lango la dukani.

"Nilihisi kana kwamba kwa sekunde kadhaa nilikuwa ninatembea na ghafla nikajiona ninaamka. Ilikuwa kitu kibaya kweli nilichopitia, kupoteza fahamu."

Wakati anatembea, Grace hakujua kumetokea nini lakini akapata fahamu dakika nane baadaye na alichoweza kuona ilikuwa ni mwanga tu mbele yake.

"Nilihisi kama niko kwenye ndoto yaani kama nipo juu ya anga, mwanga wa ajabu ukiwa unanimulika," na ikamchukua Grace dakika kadhaa kubaini kwamba yeye mwenye kipindi hicho alikuwa anapiga mayowee huku akijiambia, "Mungu Wangu! Siwezi kuhisi miguu yangu."

"Siwezi kuhisi miguu yangu".

Kwa Grace ambaye alikuwa anatafuta shahada na matibabu alijua kuna kitu kibaya kimemtokea.

"Nilihisi miguu yangu haifanyi kazi. Ilikuwa ni kama nusu ya upande wangu wa chini haufanyi kazi."

"Nakumbuka nilipopata fahamu na kuanza kuangalia angalia, niliona polisi… pia nikaanza kuhisi kuna mtu mwingine aliyelala kando yangu,"amesema.

Na hapo ndipo mwanamke mmoja alimuarifu kuwa mwanamume mmoja aliyekuwa amejirusha kutoka ghorofa ya juu, alimuangukia.

Hapo ndipo Grace akajua kwamba mtu huyo aliyejirusha kutoka ghorofa ya juu, amemuangukia.

Safari ya kukubali hali yangu

Baada ya kufikishwa hospitalini nilisikia mazungumzo ya madaktari yaliyoonesha wasiwasi mkubwa juu ya hali yangu.

"Siwezi kuhisi miguu yangu." Sikuweza kudhibiti mwili wangu, yaani hata kujua aliyekuwa ananishughulikia ilikuwa tabu." Grace amesema.

گریس اسپنس گرین

Grace aliyekuwa mwanafunzi wa chuo cha matibabu cha King's College alipelekwa hospitali ya Royal London ambako alifanyiwa upasuaji wa uti kwa saa nane alikolazwa kwa wiki 10 kabla yakuruhusiwa kurejea nyumbani.

Miongoni mwa matibabu aliyopokea ni kufanyishwa mazoezi ya viungo na kila jioni alijaribu kusongesha mwili wake kuanzia kwenye kidole cha mguuni.

Grace anakumbuka "matatizo aliyopitia": Nakumbuka kipindi kile daktari akijaribu kutikisa kidole changu cha mguuni kwasababu sikuwa nahisi chochote, kuna kipindi niliamua kuzima simu yangu kabisa, na kulala nikitamani nisiamke tena, nilipata msongo wa mawazo."

Unaweza pia kusoma:

Lakini baada ya muda, alianza kuona uhalisia wa mambo: "Unapoona uhalisia wa jambo fulani, inakuwa huna budi zaidi ya kulikubali ingawa inakufanya kuwa na machungu mengi sana kwasababu siwezi tena kuwa kama nilivyokuwa. Ni hali ngumu sana kuipitia".

" Madaktari walimuarifu Grace kuwa hataweza tena kutembea.

"Bila shaka ilikuwa moja ya siku mbaya zaidi katika kipindi hicho cha mwaka. Nakumbuka nikiwa natembea na kiti cha magurudumu mvua ikaanza kunyesha. Nilitamani dunia ipasuke niingie ndani. Sikuwahi kufikiria kuwa kuna jema lolote linalonitokea maishani mwangu".

Grace alikuwa amepooza kutoka kifuani kwenda chini.

Sina hasira na aliyenifanya kilema.

"Kila mmoja sio mdaktari si umma walikuwa wanazungumzia tukio hilo tena kwa hisia kali kweli.

گریس اسپنس گرین

"Katika hali ambayo kila mmoja alikuwa ananielezea vile nastahili kuhisi kwasababu ya tukio hilo, nikawaza hakuna anayejua hasa nini napitia, ilikuwa kitu kigeni sana maishani mwangu".

Lakini baada ya muda, Grace alianza kusikiliza hisia zake na kugundua kuwa hana hasira na aliyemwangukia.

"Nilifuatilia hisia zangu kwa miaka miwili na kugundua kwamba sina hasira kwa mwanamume aliyeniangukia na kunifanya kuwa kilema milele. Badala yake nilikuwa nina mhurumia."

Grace, alielezea BBC kwamba hakuwa na hisia zozote mbaya juu ya mwanamume huyo kwasababu "kumuwekea kisasi kungemzuia kusonga mbele".

Badala yake, Grace aliamua kuelekeza hasira zake na huzuni yake kufikiria ni kitu gani anachoweza kufanya kubadilisha maisha yake, kuelezea watu yaliyokuwa yanamkera kama vile sio ruhusu kusukuma kiti chake cha magurudumu bila ruhusa yake.

Mwanamume aliyemuangukia, Bethnal Green, alihukumiwa kifungo cha miaka minne gerezani.

Grace anasema aliamua kuwa mtulivu kwasababu "kama mwanamume huyo angeanguka chini bila shaka yoyote angefariki dunia papo hapo. Kwahiyo mimi nilikuwepo kunusura maisha ya mtu".

"Je naweza kutimiza ndoto yangu ya kuwa daktari"?

" Swali langu la kwanza kujiuliza lilikuwa, "Je naweza kutimiza ndoto yangu ya kuwa daktari".?

Huo ndio ulikuwa wasiwasi wake mkubwa.

Sasa hivi, Grace yuko mwaka wake wa mwisho chuo kikuu.

Anasema kuwa chuo anachosomea kimekuwa mfano mwema kutimiza ndoto yake.

"Sijui ningefanya nini kama ndoto yangu haingetimia kwasababu ndio kichocheo kikubwa cha motisha wakati nakabiliana na changamoto".

Unaweza pia kutazama:

Maelezo ya video, Joyce Shujaa